Tuesday, February 21, 2012

Denti anaswa gesti :YADAIWA ALIKUWA AKIUZA MWILI..




DENTI mmoja aliyefahamika kwa jina la Rehema mwenye umri wa miaka 15, hivi karibuni alinaswa gesti akidaiwa kufanya biashara haramu ya ukahaba.

Rehema alikamatwa katika gesti moja iliyopo maeneo ya Buguruni Malapa jijini Dar kufuatia operesheni iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum na baadae kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alisema binti huyo hawezi kufunguliwa mashitaka kwenye mahakama hiyo isipokuwa anatakiwa kupelekwa kwenye mahakama ya watoto iliyopo Kisutu jijini.

Hata hivyo, baadae binti huyo aliyekuwa amevaa kichangu aliachiwa huru na alipozungumza na mwandishi wetu alidai kuwa, akiwa kwa wazazi wake huko Mwanga mkoani Kilimanjaro alichukuliwa na mwanamke mmoja aliyemtaja kwa jina la Vero kwa lengo la kuja kumtafutia kazi.

“Baada ya kufika Dar, sikutafutiwa hiyo kazi matokeo yake niliwekwa kwenye gesti iliyopo Buguruni Malapa na kufanyishwa ukahaba,” alisema binti huyo.
Akaongeza kuwa, kutokana na mazingira magumu anayoishi akipatikana mtu wa kumsafirisha hadi kwao, atashukuru.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...