Sunday, February 12, 2012

MREMBO ABAKWA NA WASANII WAWILI WA BONGO FLEVA...



MREMBO mmoja mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina moja maarufu la Veni (19), amesema amebakwa na wasanii wawili wenye majina makubwa ndani ya muziki wa Bongo Fleva..


Akizungumza katika mahojiano, mlalamikaji huyo alisema kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na mmoja wa wasanii hao (jina linahifadhiwa kwa uchunguzi) kwenye saluni moja maeneo ya Kinondoni Studio, Dar akinyoa nywele ambapo mkali huyo kunako steji naye alitinga kwa huduma hiyo.


MSANII AENDA KUNYOA KIDUKU
Veni alidai kuwa, msanii huyo aliyekwenda kunyoa ‘kiduku’ alimuomba namba ya simu ili awe mmoja wa washiriki katika video ya ngoma yake mpya aliyokuwa akiiandaa.
“Sikuwa na pingamizi kwani napenda kuonekana kwenye runinga hivyo nilimkubalia na siku ilipowadia aliniita kwenye mazoezi,” alisema Veni.


LIFTI YAMPONZA
Mrembo huyo alidai kuwa kila walipomaliza mazoezi, msanii huyo akiwa na mwenzake (naye jina linahifadhiwa kwa uchunguzi), walikuwa wakimpa lifti hadi maeneo ya nyumbani kwao Kinondoni Studio.


“Nakumbuka ilikuwa Januari 5, mwaka huu, yule msanii niliyezoeana naye aliniambia tupitie nyumbani kwa huyo mwenzake, nilipoingia ndani, wote kwa pamoja walinikamata wakanivua nguo kwa nguvu huku wakipandisha sauti ya muziki ili kelele zangu zisisikike kwa majirani.
“Nilishtuka kumuona yule msanii niliyezoeana naye akivaa kondomu kisha akaniingilia kwa kadiri alivyoweza.


“Alipomaliza alimwachia mwenzake ambaye naye aliniingilia bila kujali kilio nilichokuwa natoa kuwaomba wanisamehe kutokana na maumivu makali niliyokuwa nayasikia.
“Waliporidhika, walinichukua wakaniingiza kwenye gari na kwenda kunishusha kituoni Kinondoni Studio kisha wakaondoka zao.

SAKATA LATINGA POLISI
UTAMU: Ulikwenda kuripoti polisi?
Veni: Niliogopa kutokana na vitisho walivyonipa wakiniambia nikitoa siri wataniua, lakini nilipowaza unyama siku moja nilimweleza kaka yangu ndipo akanichukua hadi Polisi Oysterbay, nikapewa PF3 kwa ajili ya matibabu na jalada la kesi namba OB/RB/561/2012 -UBAKAJI.


UTAMU: Watuhumiwa walishakamatwa?
Veni: Waliitwa polisi ila walipofika nikaambiwa nitoke nje, baadaye nilipoitwa nikapewa maagizo kuwa nije siku ya pili lakini kila nikienda naambiwa uchunguzi unaendelea hivyo bado nasubiri.


BLOG HII iliwasiliana na mmoja wa wasanii hao aliyedaiwa kuzoeana na mrembo huyo ambaye alikiri kumfahamu Veni, lakini akakana kumbaka huku akidai nyuma ya tukio hilo kuna njama nzito za kubambikiwa kesi ili afungwe hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi.

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...