Sunday, February 12, 2012

Lulu amsahau mwanaume wake wa kwanza...





Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MAKUBWA! Pamoja na umri mdogo wa miaka 18, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameacha watu midomo wazi baada ya kusema kuwa  amemsahau mwanaume wake wa kwanza aliyevunja naye amri ya sita katika vitabu vitakatifu, yaani uasherati...


Lulu ambaye ametupia sokoni muvi yake mpya ya Foolish Age aliliambia The Biggest IQ, HOT POT Wikienda kuwa, mbali na kutokumkumbuka mwanaume huyo, hakumbuki pia alianza sanaa hiyo akiwa na umri gani...


“Kusema kweli sikumbuki kabisa mwanaume wangu wa kwanza na usiniulize nilikuwa na miaka mingapi kwani sikumbuki chochote ‘coz’ ni siku nyingi sana na mambo yanabadilikika kila siku,” alisema Lulu akikinzana na maelezo yake aliyoyatoa hivi karibuni kuwa bado hajatolewa ‘usichana’ wake.


Pamoja na staa huyo mkali wa muvi kutajiwa baadhi ya wanaume waliowahi kudaiwa kutoka naye, aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa hamkumbuki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...