Wednesday, February 1, 2012

Johari awa tipwatipwa ghafla...



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinnqd2W3ob0mKXcZ-O0k3WCruiIQ8i1mntLkqRLw3SFimUvJW4xD56_WQEh4eoCg4ZRHaFREVV2DTIghrTr2Gi3qaXdt_UQA2xVTBpc08zTB3xO9cIcGtCnZRpAAHUORq46JQHKJ31pB6q/s640/100_5723.JPG
Blandina Chagula ‘Johari’.

MUIGIZAJI wa filamu hapa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ hivi karibuni ameonekana kuwa tipwatipwa ghafla kiasi cha kuwafanya watu wamshangae.

Hali hiyo inakuja huku kukiwa na nukuu za msanii huyo kwamba alikuwa akitafuta dawa ya kuwa mnene kwani alikuwa hafurahii muonekano wake.

Akizungumzia uwezekano kuwa labda kapata dawa hiyo, Johari alisema anajishangaa kwani kunenepa huko kumemjia ghafla bila kutumia chochote.

“Yaani huwezi amini mimi mwenyewe najishangaa kuwa hivi, watu wamekuwa wakiniambia na hata nilivyojiangalia kwenye kioo nimebaini nimekuwa bonge kuliko nilivyotegemea,” alisema Johari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...