Thursday, November 17, 2011

BIDHAA ZA FREEMASONS ZATUA BONGO




JAMII ya siri (secret society) yenye nguvu kubwa duniani, Freemasons, inazidi kutimiza agano la kufanya mapinduzi ya kuitawala dunia kwa kupenyeza bidhaa zake kutumiwa na wana wa ulimwengu kuliko nyingine zote.

Nchi ya Tanzania a.k.a Bongo, tayari imeshaingiliwa na Freemasons, kwani bidhaa zake zimeshatua na kutumiwa na idadi kubwa ya Watanzania pasipo watumiaji wengi kujua.

Blog hii ilibaini kuwa bidhaa za Freemasons zilizomwagwa Bongo ni chakula pamoja na vifaa mbalimbali vya mapambo na mavazi.

Imebainika kuwa bidhaa za chakula ni aina fulani ya unga wa ngano kutoka nje, sukari, maji ya kunywa yanayozalishwa na kiwanda cha mfanyabiasha maarufu wa Tanzania, baadhi ya juisi za boksi na kadhalika.

Habari zinasema kuwa mfanyabiashara mwenye kiwanda kinachozalisha maji hayo yenye uhusiano na Freemasons, anatajwa kuwa memba mtiifu wa jamii hiyo ya siri, pia ni mmoja wa mawakala wa imani hiyo, wenye nguvu kubwa ndani ya Jakayaland.

Mitandao mbalimbali inafafanua kuwa bidhaa nyingine za Freemasons mbali na chakula, yapo mabegi ya kusafiria na mikoba ya kike, pochi za kuhifadhia fedha, mikanda ya kiume na kike, vifaa vya kuhifadhia funguo ambavyo ni rahisi kuving’amua kutokana na nembo zake.

Vifaa vingine vinavyotumiwa lakini ni bidhaa za Freemasons ni saa, cheni, pete, kalamu na sarafu mbalimbali.
Tayari wataalamu wa mambo ya Freemasons, marehemu Sheikh Yahya Hussein na mwanaye, Maalim Hassan Yahya Hussein, walishafafanua kwamba alama ya nyoka kwenye noti ya shilingi 500 ni nembo ya jamii hiyo ya siri.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa Watanzania wengi wanaponunua bidhaa za Freemasons wanakuwa hawajui kwa sababu ya kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu nembo za jamii hiyo.

Ripoti za mitandao ya intaneti ambazo zinasherehesha maandiko kuhusu ujio wa Dini ya Shetani katika nyakati za mwisho, zinaeleza kuwa lengo la Freemasons kusambaza bidhaa hizo ni kukamilisha njama za kuitawala dunia.

Inaelezwa kuwa Freemasons ipo kwenye mapambano makali na muda ili kuhakikisha dunia nzima, watu wote wanamuabudu mkuu wa jamii hiyo ya siri anayeitwa Lucifer kabla ya ujio wa Yesu (Nabii Isa).

Waumini wa dini za Kiislam na Kikristo, wanaamini katika nuru pamoja na kiyama baada ya Yesu kurudi, hivyo Freemasons inataka imani hiyo ife kwa kuuhadaa ulimwengu, ikitumia falsafa za utandawazi ili walimwengu wote waelekee kwa Lucifer (Shetani a.k.a Jini Mkuu).

Kwa mujibu wa Maalim Hassan, lengo la Freemasons ni kuitawala dunia kwa kupenyeza bidhaa zake, kuhakikisha ulimwengu unakuwa na serikali moja pamoja na sarafu moja.

“Shabaha yao ni kuifanya dunia nzima ielekee kwao, dunia yote itatawaliwa na Lucifer, kwa hiyo Waislam na Wakristo wanapaswa kuwa macho kwa sababu wafuasi wao wanazidi kuongezeka na ni tabaka lenye nguvu,” alisema Maalim Hassan na kusherehesha maandiko kwamba nyakati za mwisho dunia itakuwa kwenye hatari ya kutawaliwa na Shetani.

Maandiko yanafafanua kuwa zama za Shetani kuitawala dunia, watu wasiokuwa wanaumini wake, hawatapata huduma muhimu za kijamii kwa sababu bidhaa zote zitakuwa chini ya mamlaka ya Jamii ya Siri.

Inaelezwa kuwa mwanachama wa Dini ya Shetani, atatambulika kwa chapa yenye namba 666, hivyo kabla ya kuhudumiwa ni sharti akaguliwe na akutwe nayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...