Wednesday, November 9, 2011

UZINDUZI WA ALBAMU YA ‘TWANGA’ ULIVYONOGA



Mwanamuziki wa Twanga ‘Dogo Rama’ (katikati) akiongoza mashambulizi jukwaani.

Mpiga ‘drum’ mahiri wa bendi hiyo, James Kibosho, akiwajibika.

UZINDUZI  wa albamu ya 11 ya Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ iitwayo ‘Dunia Daraja’, uliofanyika jana katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ulikuwa si mchezo. Yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyonaswa na kamera yetu katika tukio hilo.
Mkali wa kucharaza nyuzi, Jojo Jumanne, akifanya vitu vyake.

Shabiki mwenye midadi aliaramia jukwaa.

Msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba ‘The Great’ (kulia) akifurahia jambo na mwandishi wa Global Publishers, Brighton Masalu ‘Mpekepeke’.

Muumin Mwinjuma naye akiwapagawisha mashabiki (hawapo pichani).

Sehemu ya mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo wakitupia macho jukwaani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...