Monday, November 14, 2011

Comedy ZONE

Jamaa fulani toka USA alipiga simu kwa mama yake aliyekuwa kijijini Mkuu Rombo...

Jamaa: "Hallooo mama, habari... Samahani sana... Huku kwabahati mbaya nmepata maambukizi ya UKIMWI... Nimeona ni bora nije tu kuishi huko kijijini..."

Mama: "Uuuuuuwi... Jamani mwanangu nakuomba saaana usije..."

Jamaa: "Kwa nini mama...?!"

Mama: "Ukirudi nyumbani, utamuambukiza mkeo..

Mkeo atamuambukiza mdogo wako,

Mdogo wako atamuambukiza mfanyakazi wa ndani,

Mfanyakazi wa ndani atamuambukiza babako,

Babako atamuambukiza dadangu,

Dadangu atamuambukiza mumewe,

Mumewe ataniambukiza mimi,

Mimi nitamuambukiza shamba boy,

Shamba boy atamuambukiza shangazi yako wa marangu,

Na huyo shangazi yako siku hizi ni malaya wa kutupa hivyo atamuambukiza mumewe na kijiji kizima,

Na kijiji kitaiambukiza nchi nzima,

Nchi ntasambaza dunia nzima...

Kwahivyo in the name of GOD plz OKOA kijiji chetu, NAKUOMBA USIJE MWANANGU, fia tu huko huko!!!"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...