Friday, November 11, 2011

BALAA BULUU: MKE WA MTU ANASWA AKIJIUZA

 NI AIBU! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Salama Hamza ambaye anadaiwa kuwa ni mke wa mtu amezua tafrani baada ya kunaswa laivu katika maeneo ya wadada wanaofanya biashara ya kukodisha miili almaarufu  machangudoa...

Inaelezwa kuwa, Salama ni mke halali wa Hamduni Omar ambaye anaingiza siku kwa kufanya kazi ya ulinzi katika kampuni moja jijini Dar es Salaam, yenye makao yake Ilala na kwamba wawili hao wameweka makazi yao Tandika.


 Mtiti mzima ulichukua nafasi Jumatatu ya wiki hii, saa tatu na dakika zake asubuhi, pande za Kinondoni ambapo ilielezwa kuwa Salama alikuwa akiuza ‘sukari’ usiku wa kuamkia siku hiyo, lakini kwa bahati mbaya alilewa na ‘kuzima’ hadi alipozinduka asubuhi hiyo na kufumwa na shemeji yake.


Kuna vurugu huku Kinondoni Kwamanyanya, njooni mchukue habari. Mke wa mtu amefumwa na shemeji yake, yaani ni changudoa kabisa anayejiuza hapa kila siku,” alisema mtoa habari huyo kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.

Kama kawa, kama dawa,  kufuatilia matukio na kuyaandika, hivyo bila kupoteza muda, kikosi kazi kiliingia mtaani kama ‘maninja’ ili kujionea.

Kutokana na utulivu kuwa sifuri, mapaparazi wetu waliamua kuanza na zoezi la kupiga picha kwanza kabla ya kupata maelezo kutoka kwa pande zote...


SHEMEJI MTU ALALAMA
Wakati purukushani kati ya Salama na shemeji yake zikiendelea, jamaa huyo alisikika akimlaumu kwa kitendo cha kumsaliti kaka yake kwa vile anafanya kazi ya ulinzi usiku.

Kwa uchungu, kijana huyo alimwambia Salama: “Yaani kuhudumiwa kote na kaka hutosheki, kweli nimeamini kunguru hafugiki. Kwa usalama wako simama turudi nyumbani. Sitakubali kabisa kwa kitendo hiki unachomfanyia ndugu yangu.”

Baada ya kuonekana kunaweza kutokea hali ya hatari, mashuhuda waliamua kumshika Salama na wengine wakamsihi jamaa atulize jazba kwa kuwa ni mambo yanayoweza kumalizika kifamilia.

Akizungumza na gazeti hili, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dulla alisema: “Ndugu zangu, sina haja ya kujipendekeza, huyu ni shemeji yangu kabisa. Ameolewa na kaka yangu wa damu ambaye anafanya kazi ya ulinzi. Nimeshtuka sana kumuona hapa muda huu, tena akiwa hivi (nusu utupu).

“Salama huwa havai nguo za namna hii? Nimezoea kumuona na khanga mbili au baibui tu; sasa hapa hamuoni kaka yangu anaonewa? Anatumia vibaya nafasi anayoipata wakati kaka akiwa kazini, sikubali. Hawezi kumuua ndugu yangu.”


MASHUHUDA WATIA NENO
“Huyu dada ana kawaida ya kuja maeneo haya na machangudoa wenzake kila siku usiku, ila huwa anaondoka kati ya saa 10 na 11 alfajiri, lakini jana alipotoka kwa babu (akimaanisha kwa mlinzi anayetoa huduma ya sehemu ya kufanyia ngono chapchap) alifika hapa na kuagiza kiroba.


Alipomaliza akaongeza kingine, halafu zikafuata bia. Alikunywa sana hadi akalala kwenye kiti. Alipoamshwa hakusikia. Sasa asubuhi hii huyu jamaa alifika hapa na kuagiza supu ya utumbo, nikaona anamkazia macho kabla hajamvaa.

“Chakushangaza huyo dada (Salama) naye akaanza kukimbia.

Tukadhani labda alimuibia au alimtoroka, kumbe ni shemeji yake,” alisema dada mmoja aliyekuwa eneo la tukio bila kufafanua yeye ni nani na jina lake.


MSIKIE SALAMA ‘WALUWALU’
UTAMU: Unamfahamu huyo kaka?

SALAMA: Ndiyo, ni jirani yetu tunakaa naye Tandika.
UTAMU: Siyo shemeji yako?

SALAMA: Hapana, ni muongo, sijui kwa nini ananiingilia kwenye anga zangu. Mbona dada yake Ashura anajiuza Buguruni (Dar) hamfuatifuati?
UTAMU: Kwa hiyo wewe si mke wa mtu?

SALAMA: Aku! Sijaolewa mimi, ananisingizia tu.
Penye wengi hapaharibiki neno, mashuhuda waliokuwa eneo la tukio waliwashauri wawili hao wachukue teksi na kwenda nyumbani kwao Tandika ili wakayazungumze kifamilia, jambo ambalo walikubaliana nalo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...