Wednesday, November 16, 2011

Comedy ZONE


Jamaa mmoja aliingia corner bar Sinza na kumwambia muhudumu ampe safari 3 za baridi... Jamaa akapiga bia zake tatu mfululizo thn akaagiza zingine tatu akazipiga tena akaomba zngine tatu... 

Yule muhudumu akamwambia.. Samahani, naona unakunywa safari baridi... Kwnn nisikupe moja moja ili zicpoe?! Jamaa akamwambia.. Ofcoz ni ngumu kwa ww kuelewa!!! Sisi tumezaliwa mapacha watatu, mmoja yuko Australia, mwingine marekani... Tuliwekeana ahadi kuwa kila jmoc lazima tunywe bia si chini ya round 3 pamoja kwa kila mtu alipo... Kwa hyo sasa hivi wenzangu wanakunywa hivi hivi huko waliko.... 

Mhudumu akampongeza sana mteja wake kwa kutimiza ahadi waliyojiwekea...

Kwa hiyo kila jmoc jamaa akawa anaende pale kona bar na kupiga hizo safari tatu tatu round zaidi 3...

Kuna wikend moja jamaa akaenda na kuagiza safari mbili mbili tu.... Baada ya round kama tatu, yule mhudumu akaamua kumuuliza... Vp?! Mwenzako mmoja kafariki nn.. Mbona leo unaagiza mbili mbili?! 

Jamaa akajibu huku akiwa kaanza kuwa TILALILA... 
"Daah, leo nmekunywa dawa za malaria kwa hyo hapa ni wenzangu tu ndo wanakunywa, mi sinywi leo!!!"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...