Sunday, November 6, 2011

Comedy ZONE

Bibi kizee mmoja alikuwa anasafiri kwenye basi usiku, siti ya nyuma yake alikaa SHAROBARO mmoja...

Wakati safari inaendelea akawa anainama chini ya siti yake anachukua kopo lake la castle na kulipeleka mdomoni(kama anakunywa kitu) kila mara...

SHAROBARO akawa anatamani ile bia huku akimuone wivi yule bibi anavyofaidi maisha kwa kukandamiza castle kwenye basi. Jamaa akaamua amuibie angalau apige pafu mbili halafu arudishe haraka lile kopo kabla bibi hajashtuka...

Basi SHAROBARO akamtym bibi wakati analitoa mdomoni na kuliweka chini, kwa haraka akapitisha mkono chini ya seat, akachukua lile kopo akanywa funda moja kuuubwa...!!!!

Baada ya hapo akasikika anapiga makelele na kutema mate kama mtu anayetaka kutapika.... Ebwaana daaah, umbe yule bibi alikuwa anaumwa Kifua kikuu na alichukua kopo lile la castle kwa ajili ya kutemea makohozi.....!!!!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...