Ray na Wema wakiwa juu ya steji.
VINCENT Kigosi 'Ray' na Wema Isaac Sepetu hivi karibuni walizua jipya, tena laivu wakiwa juu ya steji baada ya Ray kukosea jina na kumwita WEMA Jokate...
Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilijiri ndani ya Viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kulikuwa na ile ‘iventi’ ya Serengeti Fiesta 2012.
Awali, Ray akiwa ameshika ‘maiki’ alimwita Wema aende stejini ili akaoneshe umahiri wake katika kukata mauno.
Hata hivyo, staa huyo alifanya nyodo baada ya kuambiwa ageuke nyuma ili mashabiki wake waone makalio yake yaliyomdatisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.
Katika hali iliyowashangaza wengi, Wema alisuasua kutekeleza ‘amri’ hiyo na ndipo Ray alipojichanganya na kumwita Wema Jokate (Mwegelo).
Jina hilo lilimkasirisha sana mwanadashosti huyo hivyo kwenda kumnyang’anya ‘maiki’ Ray ili kuuleza umati jinsi alivyokasirishwa na kitendo cha kuitwa Jokate.
Wakati Wema akinyang’anyana maiki kwa Ray, alisikika akiwaka kwamba staa mwenzake huyo alimdhalilisha kwa kumwita jina ambalo mmiliki wake hataki hata kumsikia achilia mbali kumwona.
Hali hiyo ilisababisha mahali hapo kuchimbika hadi pale DJ Zerro aliyekuwa ‘akiskrachi’ mashine alipoweka muziki mkubwa ili kuwapotezea kwani wangepewa muda zaidi wa kujibizana, pangechimbika zaidi.
Hili ni tukio lingine la aina yake ambapo staa anaitwa kwa jina la ‘adui’ yake na kusababisha hali kuwa tete.
Mwanzoni mwa mwaka huu, wakati mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema akifanya mahojiano na mastaa wa Bongo, Irene Uwoya na Wema Sepetu, alikosea jina na kumwita Uwoya, Jacqueline Wolper hali iliyoibua hasira kwa staa huyo akidai hafanani na Wolper hata kwa asilimia thelathini.
Kama hiyo haitoshi, katikati ya mwaka huu, wasanii wa Bongo Movie walifanya ziara ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Wakiwa mjini Moshi, Kilimanjaro, mwenyeji wao alifanya utambulisho ambapo kwa bahati mbaya alipofika kwa Uwoya, alimtaja kwa jina la Wolper, staa huyo akazua tafrani akidai lazima staa mwenzake huyo (Wolper) atakuwa amemroga ili jina lake lisahaulike katika jamii.
No comments:
Post a Comment