GWIJI wa Hip Hop ambaye pia ni Mtayarishaji wa muziki na Mjasiriamali nchini Marekani, Andre Romelle Young maarufu kwa jina la Dr. Dre ndiye msanii wa Hip Hop anayetengeneza fedha nyingi kwa sasa. Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, Dr. Dre anaongoza akiwa ametengeneza kiasi cha dola milioni 110 zaidi ya shilingi bilioni 173 za Kitanzania kwa mwaka 2012. Anayemfuatia ni mwanmuziki Sean John Combs maarufu kama P. Diddy anayetengeneza kiasi cha dola milioni 45 zaidi ya shilingi bilioni 70 za Kitanzania. Wa tatu ni msanii Shawn Corey Carter maarufu kama Jay-Z anayejiingizia kiasi cha dola milioni 38 sawa na shilingi bilioni 59.9 za Kitanzania.
Orodha ya majina ya wasanii walioingia 20 bora ni kama ifuatavyo:
1. Dr. Dre – Dola milioni 110 sawa na shilingi bilioni 173.3
2. Diddy – Dola milioni 45 sawa na shilingi bilioni 70.9
3. Jay-Z – Dola milioni 38 sawa na shilingi bilioni 59.9
4. Kanye West – Dola milioni 35 sawa na shilingi bilioni 55.1
5. Lil Wayne – Dola milioni 27 sawa na shilingi bilioni 42.5
6 Drake – Dola milioni 20.5 sawa na shilingi bilioni 32.3
7. Birdman – Dola milioni 20 sawa na shilingi bilioni 31.5
8. Nicki Minaj – Dola milioni 15.5 sawa na shilingi bilioni 24.4
9. Eminem – Dola milioni 15 sawa na shilingi bilioni 23.6
10. Ludacris – Dola milioni 12 sawa na shilingi bilioni 18.9
11. Pitbull – Dola milioni 9.5 sawa na shilingi bilioni 14.9
12. Rick Ross – Dola milioni 9 sawa na shilingi bilioni 14.2
12. Wiz Khalifa – Dola milioni 9 sawa na shilingi bilioni 14.2
14. Snoop Dogg – Dola milioni 8.5 sawa na shilingi bilioni 13.4
15. 50 Cent – Dola milioni 7.5 sawa na shilingi bilioni 11.8
16. Swizz Beatz – Dola milioni 7 sawa na shilingi bilioni 11
16. Pharrell – Dola milioni 7 sawa na shilingi bilioni 11
16. Young Jeezy – Dola milioni 7 sawa na shilingi bilioni 11
19. Mac Miller – Dola milioni 6.5 sawa na shilingi bilioni 10.2
20. Akon – Dola milioni 6 sawa na shilingi bilioni 9.5
20. Timbaland – Dola milioni 6 sawa na shilingi bilioni 9.5
20. Tech N9ne – Dola milioni 6 sawa na shilingi bilioni 9.5
No comments:
Post a Comment