Sina uhakika aliyeipiga video hii aliwezaje kuvumilia kuona ushenzi huu, na akaamua kuirekodi ili kutaka kufikisha ujumbe halisi kwa watu ili kupunguza ile kasumba ya mabishano kuwa “anatunga visa na hadithi...” (ama pengine kweli alishafanyiwa ubishi kiasi cha kudhamiria kuonesha kithibitisho hiki) AU, alikuwa anafurahia kinachotendeka na ikiwa mwenyewe anaona ni sahihi na hili ndilo moja ya soko lake la ngono za watoto
Naomba anisamehe kwa kumwazia hivi, ila ninaendelea kuamini kuwa sababu ya niliyoitaja awali ndiyo muhimu zaidi iliyomsukuma kufanya hivi kwa lengo la kuujulisha na kuutahadharisha umma kuhusu yanayoendelea katika jamii.
Wahenga walituambia, “Kubeba mimba si kazi, kazi ni kulea mwana” pia, “Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu” na vile vile, “It takes a village to raise a child”. Tukiyaonea haya, tusiyajadili, tutaendelea kukuza jamii iliyoharibika!
NAOMBA RADHI. NINATANGULIZA SAMAHANI.
HII NI KWA WALE AMBAO WAMENITUMIA EMAIL WAKIDAI KUWA HAWAIONI VIDEO.......SASA NADHANI INAONEKANA VIZURI......
Siioni video
ReplyDelete