FIESTA 2012 UWANJA WA SAMORA IRINGA ILIVYOCHUKUA NAFASI
Lina mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na Tausi mmoja wa mashabiki waliojitokeza katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, linalofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa ambapo wasanii mbalimbali wanafanya vitu vyao jukwaani wakiburudisha mashabiki wa mkoa wa Iringa, Lina ameweza kufanya mambo makubwa na kuwaimbisha mashabiki wake ukizingatia kwamba anatoka mkoa huo
Meneja Masoko wa kampuni mya Push Mobile Rugambo Rodney akitangaza washindi wawili wa pikipiki walioshinda habati nasibu hiyo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Iringa kwenye uwanja wa Samora huku wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongofleva wakionyesha uwezo wao katika muziki na kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika kwenye uwanja huo, katika picha aliyeshika kipaza sauti ni mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds B12
Amini akiimba jukwaani katika tamasha hilo
Msanii Rich Mavoko akiwa ameruka hewani wakati akicheza pamoja na wanenguaji wake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Iringa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linex akiimba kwa hisia kali jukwaani katika onesho la muziki la Serengeti Fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa , msanii huyo mwenye uwezo wa kutawala jukwaa amefanikiwa kukata kiu ya mashabiki wa muziki wake
MATUKIO FIESTA 2012 MBEYA
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh. Dkt. Norman Sigallah akishuhudia wakati Rugambo Rodney meneja masoko wa kampuni ya Push Mobale akichezesha bahati nasibu ya gari aina ya Virtz inayochezaeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ikishirikiana na Push Mobile katika tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh. Dkt. Norman Sigallah akishuhudia wakati Rugambo Rodney meneja masoko wa kampuni ya Push Mobale akichezesha bahati nasibu ya gari aina ya Virtz inayochezaeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ikishirikiana na Push Mobile katika tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine
FIESTA 2012 MBEYA ‘HAKUNAGA’
Msanii chipukizi kupitia zoezi zima Serengeti Fiesta 2012 Supa Nyota kutoka mkoani Mbeya aitwaye Neey Lee akiwaimbisha mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Sokoine.
Tamasha la serengeti fiesta 2012 lafanyika jijini mwanza,mmoja ajishindia gari aina ya vits...
Mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits,Bahati Joseph akionesha ufunguo wake aliokabidhiwa mbele ya umati wa watu (hawapo pichani) uliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,jijini Mwanza.
Mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Pichani kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile Bwa,Rugambo Rodney akikambidhi ufunguo wa gari hiyo Mkazi wa Mwanza,Bahati Joseph akiwa mwenye furaha tele.Pichani nyuma wanaoshuhudia ni Mwakilishi wa bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Bwa.Bakari Maggid pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba
Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba akisoma namba ya mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kati ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile Bwa,Rugambo Rodney na shoto ni mmoja wa wakilishi wa bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Bwa.Bakari Maggid wakishuhutia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.Mshindi wa gari hiyo aina ya Vitz alitajwa kuwa ni Bahati Joseph,mkazi wa jiji la Mwanza,mjasilia mali.
Baadhi ya mashabiki wakiwa wamejitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,linalofanyika kwenye uwanja wa ccm Kirumba.
Msanii wa bongofleva,Bob Junior a.k.a Shombe shombe akitumuiza na densa wake jukwaani
Pichani kulia ni msanii Recho kutoka THT akiwa sambamba na densa wake wakionesha umahiri wa kuimba jukwaani mauno kwa mbalii hivi.
Sehemu ya timu ya amsha amsha ya tamasha la serengeti fiesta 2012,kulia ni Dj Fetty,Bonge,Mully
Msanii wa kike anaekuja kwa kasi Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu
Sehemu ya umati wa watu ukishangweka vilivyo usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba.
Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki akiwa amepozi na mashabiki wake kabla ya kupanda jukwaani usiku huu.
Msanii Ney wa Mitego kama kawa akikamua kwa hisia mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi ndani ya uwanja wa ccm kirumba.
Msanii Ommy Dimpoz pozi kwa pozi akitumbuiza jukwaani na kundi lake
Mwanadada machachari kabisa awapo jukwaani,Mwasiti akiimba jukwaani usiku huu.
Mzee wa Miduara katika anga ya muziki wa kizazi kipya,IT akiimba jukwaani.
Masharobaro ndio habari ya mujiniiiii….! Bob Junior na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti fiesta 2012 usiku huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya aka Bongofleva,Prof Jay akishusha mistari yake kama kawa mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.
Pichani kati msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Barnabas a.k.a Baba Steve akiimba jukwaani usiku huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba,ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likirindim kwa shangwe za hapa na pale.
Ilikuwa ni full Burrudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
Wa pili kulia ni Dj Fetty akionesha umahiri wake wa kucheza mdundo wa sebene huku akichombwezwa na muigizaji wa filamu,Steve Nyerere,kushoto ni Aunt Ezekiel ,Wema Sepetu na JB wakimpa sapoti Fetty.
Ngosha a.k.a The Swagadon a.k.a Fid Q na mengineyo uyajuayo,ndio kwanza yuko jukwaani akiangusha mistari yake tata kwa mashabiki,usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba,wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kuunguruma.