‘We Talking Money You Talking Nonsense’ huenda ikawa kauli nzuri kuelezea hiki walichokifanya P-Square kwa sasa. Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.
Peter ameshare picha hizi nne ambazo wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’
Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”
No comments:
Post a Comment