Mwanamuziki mahiri ndani ya kundi la Quartie Latin aitwae Cindy, linaloongozwa na nyota wa muziki wa dansi kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akiimba jukwaani usiku huu mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi (hawapo pichani),kwenye tamasha la usiku wa Tusker Carnival ndani ya viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Mwanamuziki Koffi Olomide akijimwaya mwaya kwa madaha kabisa jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Tusker Carnival,huku akishangiliwa na umati mkubwa watu uliohudhuria tamasha hilo.
Wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wiki usiku huu kwenye onesho la Mwanamuziki wa Kimataifa,Koffi Olomide,wakiwa wametulia tulii huku wakiburudishwa na rhumba live kabisa.
Pichani juu na chini ni Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide sambamba na skwadi lake la Quartie Latin
Koffi Olomide akimtambulisha rafiki yake mkubwa jukwaani,Mkurugenzi wa Clouds Media G Joseph Kusaga,ambaye ndiye aliyemleta hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker,ambapo pia mwanamuziki huyo alimshukuru sana Joseph kusaga kwa ukarimu wake.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,akizungumza machache na kuwashukuru sana wadhamini wa onesho hilo sambamba na wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye onesho hilo ambalo limefana kwa kiasi kikubwa.
Koffi Olomide akimtambulisha mwanamuziki wake mahiri Cindy mbele ya mashabiki wake.
Wapenzi na washabiki wa Muziki wa Dansi wakiendelea kushuhudia yaliyokuwa yakijiri jukwaani kama waonekanvyo pichani.
Koffi Olomide akiimba jukwaani na madansa wake kwa umahiri mkubwa
sehemu ya umati wa washabiki wa onesho la Tusker Carnival wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri jukwani.
Koffi Olomide akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon ambao ndio wadhamini wa onesho lake,anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Medai Group,Joseph Kusaga.
Pichani juu na madensa wa Koffi Olomide wakiwajibika jukwaani vilivyo
Cindy akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake (hawapo jukwaani? usiku huu.
Sehemu ya umati wa mashabiki wakifuatilia onesho.
Palinogaje sasa na madensa wa Koffi Olomide.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SBL,Steve Gannon akielekezwa jambo na Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide kabla ya kupanda jukwaani.
Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya SBL,ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho la mwanamuziki huyo,aliyefanikiwa kuzikonga nyoyo za washabiki wake kwa kiasi kikubwa usiku wa leo kwenye viwanja vya lidaz,Kinondoni jijini Dar.Koffi Olomide siku ya jumapili atatumbuiza kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mwanamuziki Kalala JR akiliongoza jahazi lake la Twanga Pepeta jukwaani usiku huu.
Wanamuziki wa Bendi ya Skylight wakionyesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa kwenye Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Wanamuziki wa Bendi ya Diamond Musica wakifanya mambo yao jukwaani kwenye Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Madansa wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiwachengua Mashabiki wao wakati wa muendelezo wa Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru (katikati),Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Nandi Mwiyombela na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacoma Tanzania,Kelvin Twissa wakibadilishana mawazo wakati wa muendelezo wa Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ilikuwa ni shangwe na furaha kwa wafanyakazi wa kampuni ya SBL pamoja na Wadau wao,wakati Mopao Mokonzi Koffi Olomide alipokuwa akitumbuiza jukwaani.
Wadau.
Shangwe kwa Mashabiki wa Muziki wa Dansi jijini Dar.
Mdau akigonga vitu huku akiwa kaweka pochi yake mkononi.