Monday, April 9, 2012

VIONGOZI WA SERIKALI WAGUSWA NA MSIBA WA KANUMBA



Waziri Sita akisaini kitabu cha maombolezo.

Mama Tunu Pinda akisaini kitabu cha maombolezo.

Martha Mlata akisaini kitabu cha maombolezo.

Idd Azan akisaini kitabu cha maombolezo.

Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo.

Baadhi ya waombolezaji wa msimba huo.

Watu waliendelea kumiminika kwenda kuomboleza nyumbani kwa marehemu kanumba.

Picha ya marehemu Kunumba ikiingizwa nyumbani kwake.

Viongozi mbalimbali wa chama na serikali leo wamejitokeza katika msiba wa aliyekuwa nguli wa sanaa ya maigizo nchini marehemu Steven Charles Kanumba uliopo eneo la Vatican Sinza jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao kwa nyakati tofauti wamemzungumzia Kanumba kama nyota iliyozimika ghafla katika tasnia hiyo kwani kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuitangaza Tanzania kwenye nyanja ya filamu za Bongo.

Miongoni mwa viongozi wa serikali waliofika katika msiba huo mpaka kamera yetu inaondoka eneo la tukio ni Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samweli Sita, Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga, Martha Mlata (Mbunge viti maalum CCM) na  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Idd Azani.

 Wengine ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa  Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw.Nape Nnauye, mkewa wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda na  Ridhiwani Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...