Thursday, April 19, 2012

AFUNGWA KWA KUFICHA ‘COCAINE’ KWENYE PILIPILI HOHO



Stanley Okpara mhusika wa madawa hayo aliyefungwa.

Shehena ya pilipili hoho iliyokuwa ipokelewe uwanja wa ndege.

Pilipili kufunguliwa yakutwa madawa ya kulevya.

Pilipili zote kumbe zilikuwa na madawa.

STANLEY OKPARA (42) raia wa Sierra Leone ametupwa jela nchini Uingereza kwa kujaribu kuingiza humo madawa aina ya cocaine yakiwa yamefichwa katika mzigo wa pilipili hoho.

Mtu huyo alikamatwa na maofisa wa uhamiaji alipojaribu kuyachukua madawa hayo yaliyokuwa uwanja wa ndege wa Manchester kutoka Nigeria tarehe 25 Februari mwaka huu.

Pilipili hizo zilizokuwa ndani ya maboksi zilikuwa na madawa yenye uzito wa gramu 200 ambayo yalikuwa na thamani ya kiasi cha Paundi 13,000 kwa bei ya mitaani ambazo ni sawa na shilingi milioni 33 za Tanzania, walisema maofisa wa serikali.

Okpara, mkazi wa Getrude Close, Salford, alifungwa kwa miaka saba na Mahakama ya Bolton Crown jana kwa kosa la kuingiza madawa yaliyopigwa marufuku nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...