Thursday, January 5, 2012

WAZUNGU WAWILI HATIANI KWA MAUAJI YA MWEUSI UINGEREZA


Gary Dobson (kushoto) na David Norris watuhumiwa katika kesi ya mauaji ya Stephen Lawrence.
Stephen Lawrence enzi za uhai wake.
•Ni baada ya miaka 18 kupita
BAADA ya miaka 18, miezi 8 na siku 12 ya upelelezi wa kesi kuhusu mauaji ya kijana mweusi mjini London aitwaye Stephen Lawrence, wanaume wawili wamepatikana na hatia.
Watu hao, Gary Dobson na David Norris, walitiwa hatiana na jopo la mahakama baada ya  kesi hio kupitia ushahidi wa kitaalamu.
T-shirt aliyokuwa amevaa marehemu Stephen Lawrence siku alipouawawa.
Wataalamu wa uchunguzi wa damu na alama kama hizo waligundua alama ya damu kwenye  koti la Dobson ambayo bila shaka isingepatikana bila kumkaribia marehemu.
Wakati akiondolewa mahakamani, aliliambia jopo kuwa wamemhukumu mtu asiye na hatia. Hukumu itasomwa leo.
Wazazi wa marehemu Stephen, Doreen na Neville, waliangua kilio jopo lilipotangaza kuwa watuhumiwa wamepatikana na hatia.
Duwayne Brooks, rafiki mkubwa wa Stephen Lawrence aliyekuwa naye waliposhambuliwa, alituma ujumbe kupitia mtandao wa Tweeter akisema, hatimaye, sheria imetendeka.
Mamake Dobson, Bi.Gary Dobson, aliyeiambia mahakama kuwa mwanawe alikuwa nyumbani wakati wa mauwaji, aliangua kilio mahakamani kufuatia tangazo la watuhumiwa kupatikana na hatia.

Wazazi wa marehemu Stephen, Doreen na Neville Lawrence wakati wakifuatilia kesi hiyo mwaka 1995.
Upelelezi wa kwanza uliofanywa na polisi ulishindwa na kusababisha polisi ya mji wa London kutuhumiwa kama idara inayoendesha ubaguzi wa rangi.

Stephen Lawrence alikuwa mwenye umri wa miaka 18 alipouawa kwa kisu akiwa karibu na kituo cha basi cha Eltham, kusini mwa London,  April mwaka 1993.
Polisi waliwatambua watu watatu ambao baadaye walitajwa katika ripoti ya uchunguzi kama washukiwa wakuu.

Hadi wakati huo kulikuwepo mfululizo wa mapungufu ya polisi kwa kushindwa kukusanya ushahidi wa kutosha mara mbili, ambapo wa kwanza uliowasilishwa na wazazi  wake Stephen Lawrence, Doreen na Neville Lawrence.

Lakini katika kuichunguza kesi hiyo kwa mda wa miaka minne, wataalamu wengine wa kupeleleza ushahidi waliweza kugundua ushahidi ulioweza kuwaunganisha washukiwa na mauaji - ushahidi ambao ulikuwa mikononi mwa polisi kwa kipindi kirefu.

Ushahidi huo wa alama za damu, nyuzi za nguo na unywele wa marehemu - vilipatikana kwenye nguo za washukiwa zilizokamatwa tangu mwaka 1993.

Wataalamu wa upelelezi wa ushahidi walifanikiwa kugundua ushahidi huo kwa kutumia mitambo ya kisasa ambayo wakati ule haikuwepo.

Dobson, mwenye umri wa miaka 36, na Norris miaka 35, walikanusha madai ya kuua. Walidai damu hio ilichanganyika na nguo zao kutokana na kuchanganywa na ushahidi kupitia kipindi cha miaka mingi.

Wapelelezi walitumia muda kuchunguza jinsi ushahidi huo ulivyozungushwa na jinsi ulivyohifadhiwa kuondoa shaka ya uwezekano wa kuchanganywa kama walivyodai watuhumiwa.

Gary Dobson alikamatwa na kufungwa jela mnamo mwaka 2010 kwa kushiriki biashara ya kuuza mihadarati. Yeye ni miongoni mwa kundi dogo la wanaume waliohusishwa na uhalifu mmoja baada ya mahakama ya rufaa kutupa ombi lake la rufani mnamo mwaka 1996.

Katika mahojiano marefu na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), mamake Stephen Lawrence, Doreen,  alisema: "Siwezi kuwasamehe vijana waliomuua mwanangu Stephen. Wao hawaoni  kama wametenda uovu wa aina yoyote.”

Hukumu inatazamiwa kutolewa leo.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA www.guardian.co.uk

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...