MAPACHA wazee zaidi duniani jana (Jumatano) walisherehekea kutimiza miaka 102 tangu wazaliwe. ‘Wawili’ hao ni Ena Pugh na Lily Millward, ambao ni Waingereza, walisherehekea siku hiyo wakiwa pamoja ambapo walikabidhiwa vitabu vya Rekodi za Dunia vya Guiness kwa kuvunja rekodi hiyo.
Wanawake hao mapacha walizaliwa mwanzoni mwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na hadi sasa bado wanakutana katika kufanya manunuzi na kuongea kwenye simu karibu kila siku ambapo Millward alisema vicheko na utani ndivyo huwaongezea nguvu ya kuendelea kuishi.

“Tulikuwa tukifanya kazi shambani siku nzima, jambo ambalo lilitufanya tupendane na kuwa katika afya njema,” aliongeza Millward.
Pamoja na umri wao mkubwa, mapacha hao bado wanaweza kusafiri katika mabasi na kwenda sokoni bila matatizo.
No comments:
Post a Comment