Thursday, May 3, 2012

NAMNA YA KUNYWA MAJI YOYOTE YALIYO MBELE YAKO



Mvua za masika zimeshika kasi. Magonjwa ya kuhara na malaria ndio wakati wake na yanaongeza mrundikano wa wagonjwa mahospitalini bila huruma. Madakitari nao baada ya mgomo sura zao zinaonyesha dhahiri kuwa muda wa kupeana "lifti" umeisha....
Tusikilizane hapa jamani ili tulindane tusiumwe kizembezembe masika hii. Maji yoyote mbele yako yana sura tatu. Yapo yenye umbea wa bacteria, yenye umbea wa chumvi, na yenye umbea wa SUMU pia.... Sasa hebu tuangalie tunayanywaje halafu tusiumwe?

Maji yenye Bacteria.
Maji haya utayaona hayatokani na umbea wowote wenye chanzo toka viwandani. Kifupi maji haya yapo maporini, vijijini n.k. Kwa kutumia tu akili ya kawaida utayatambua kuwa maji haya hayajachanganyika na kemikali za viwandani ila tu ni MACHAFU. Basi weka mazoea ya kutembea na punje za Iodine katika wallet yako na ukikutana na maji kama haya basi tia punje moja tu katika glasi yako kisha subiri dakika tano halafu kunywa na hutaumwa tumbo wala maradhi mengine maana Iodine inaua wadudu wote kwenye maji ya kunywa binadamu. 

Maji yenye Chumvi.
Haya kitaalamu yanaitwa "slow Killer" Maji haya yana chumvi ambayo kwa haraka utahisi ni ile ya kwenye mboga. Sio! Ile ni sumu inayotokana na madini yasiyojulikana ardhini. Sumu ile huua taratibu sana kiasi kwamba hakuna mtu anayeishtukia kwa kuwa ipo siku watu wote wanaokunywa maji hayo hujikuta tu mahospitalini wakiwa na ugonjwa unaofanana na madaktari wanapata taabu kuutambua ugonjwa huo mara moja. Sasa kama unaishi eneo lenye maji hayo basi unaweza ukachuja ile chumvi kwa urahisi tofauti na watu wanaodhani kuwa mpaka upate mitambo mikubwa. Wewe fanya hivi:

1. Chukua beseni la plastic. Jeusi ndio zuri zaidi.
2. Weka maji yenye chumvi ndani yake, ukikosa chukua hata ya bahari au weka maji halafu tia chumvi pakiti nzima koroga.
3. Weka ndani yake jagi au chombo chochote kizito ambacho hakitaelea. Angalia maji ya kwenye beseni yasiingie.
4. Chukua karatasi la nailoni funika juu ya beseni halafu funga kamba pembezono hewa isiingie. weka jiwe dogo saizi ya ndimu juu yake katikati ukikilenga chombo cha ndani.
5. Nenda kaweke beseni lako juani kaa baadya dakika kumi nenda utakuta maji yenye chumvi yanaweka umande juu ya karatasi la nailoni halafu ile jiwe pale katikati inaweka uzito ambao umande huo unachuruzika kulifuata na kudondokea ndani ya chombo chako.

Maji hayo kwenye hicho chombo ukiyaonja hayana chumvi tena! hivyo kadiri unavyotaka kuzalisha mengi ndivyo utakavyopiga hesabu ya ukubwa wa kisima, chombo cha kukingia na muda wa kuanika juani. Ukitaka msaada juu ya hili nipigie 0768 215 956 nije nikusaidie.

Maji yenye sumu.
Eeeh! Huku kuna utata. Upo uwezekano wa kunywa maji yenye sumu. Lakini wewe maji hayo ya nini? Kama upo katika mazingira ya kunywa maji haya basi nakuomba tuonane tuyaongee halafu nitakuelekeza namna ya kuyanywa maji haya. Nafanya hivi kwa sababu sio siri watanzania wameacha ustaarabu wa upendo na ukarimu siku hizi wameanza kuuana kwa kulishana sumu. Sio umbeya, Kakaangu siku moja alipewa maji yenye sumu na mtu ambaye ni "mzazi" wake kabisa. Mawaziri na wabunge nao tumeshuhudia wakifanyiana vituko hivi. Hivyo nitaomba kama yupo mtu anajiona yupo katika mazingira hatarishi ya kunyweshwa sumu anipigie nitamwambia la kufanya ili ayanywe yote bila kudhurika.

Mwisho nawaombeni sana ndugu zangu forward hii e-mail kwa watu wengi zaidi ili tupunguze matatizo yanayoepukika. Mimi nipo mbioni kuwaomba watu wa TV,Redio na Magazeti kunisaidia kuisambaza habari hii pia.

Kwa wale ndugu zangu wanaongoja "Palm Reading" wasubiri mwezi ujao nitazungumzia mstari wa maisha - Life Line. Ila nafikiri mmeona kwa macho jinsi Head line za watendaji wa serikali zinavyowaumbua watu waliong'ang'ania kazi zisizo zao walivyo tumbo joto sasa hivi kama nilivyoandika last time.... Palm reading inaongea UKWELI kuhusu maisha ya mtu. Najua wapo watakaokuja kusomwa viganja vyao sasa niwaambie la kufanya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...