Tuesday, May 22, 2012

AJALI YAUA WATATU MJINI IRINGA



Taxi yenye namba za usajili T620 ANE baada ya ajali ya uso kwa uso na Fuso eneo la kituo cha Mafuta Esso kwenye barabara kuu ya Iringa - Mbeya asubuhi hii.

Fuso yenye namba za usajili T897 AQS baada ya kugongana uso kwa uso na Taxi.

Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani mjini Iringa wakiwa wamebeba moja kati ya maiti za ajali ya Taxi na Fuso iliyotokea eneo la kituo cha Mafuta Eso kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya asubuhi hii.

Wananchi wakiwa eneo la tukio. PICHA ZOTE KWA HISANI YA: http://francisgodwin.blogspot.com/
Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo baada ya Fuso kugongana uso kwa uso na Taxi.
Mashuhuda waliozungumza na mtandao wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi ambako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya unaendelea .
Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo cha mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso na Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limesheheni magunia ya mpunga.
Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea Fuso hilo kuigonga Taxi na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .
Jitihada za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo baadhi ya miili imeharibika vibaya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...