Watu wengi wengi huvaa T-shirts zenye picha yake bila kujua alikuwa ni mpiganaji wa kimataifa aliyepigania haki za wanadamu wenzake duniani badala ya kuleweshwa na madai ya amani na utulivu yanayosemwa kwa ulaghai na viongozi wengi wanafiki duniani.
Mwanaume huyo aliyekuwa aliyekuwa na wajihi wa kuvutia alikuwa raia wa Argentina aliyezaliwa Juni 14, 1928 na akafariki Oktoba 9, 1967 huko Bolivia alikouawa akiendesha mapambano dhidi ya manyanyaso ya watawala.
Umaarufu wa Che Guevara (hutamkwa Che Gevara) ulijitokeza sana duniani alipoungana na wapiganaji wa Cuba waliokuwa wamekimbilia Argentina ili kupanga mapambano dhidi ya utawala wa Fulgencio Batista wa Cuba.
Che – jina maarufu ambalo kwa Kihispania ni “kakitu” --aliungana na kina Castro na kwenda nao Cuba kuendesha mapambano na kuuangusha utawala wa Basitsta mwaka 1959 ambapo baadaye akawa waziri wa viwanda.
Hata hivyo, baadaye aliuacha wadhifa huo na “kutokomea” kwengine ambako aliendeleza mapambano dhidi ya watawala wa kidikteta duniani.
Katika mapambano hayo hakusita kuwachochea watu wasikubali kuwekwa mifukoni na watawala ambao wakishika madaraka au kufika ikulu huwafanya watu wengine wapumbavu.
Mwaka 1967 alifika nchini Tanzania wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere na akajiunga na wapiganaji wa Congo waliokuwa wakiendeleza mapambano dhidi ya utawala wa aliyekuwa dikteta wa nchi hiyo, Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga.
Wapiganaji hao walikuwa ni pamoja na aliyekuja kuwa Rais wa Congo, Laurent Kabila, baba wa rais wa sasa wa nchi hiyo, Joseph Kabila ambaye alikulia na kusomea Tanzania shule ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, makazi yao yakiwa Kunduchi.
Ni Ernesto Che Guevara ambaye watu wengi huvaa T-shirt za picha yake na kuweka ‘stickers’ kibao kwenye magari na sehemu mbalimbali bila kumfahamu picha yake ni maarufu zaidi duniani.
Kwa kifupi picha yake hiyo ilipigwa na Alberto Koda kwenye mazishi huko Havana siku ya kuomboleza watu waliokufa katika meli ya La Coubre iliyotegwa bomu na majasusi wa Marekani na kuua watu kibao.
No comments:
Post a Comment