Wednesday, November 9, 2011

MTOTO AZALIWA NA SEHEMU 4 ZA SIRI


AGANO kwamba nyakati za mwisho, matukio mengi ya ajabu yatadhihirika, linazidi kupata nguvu kutokana na tukio la kusikitisha lililotokea Arusha.

Wakazi wa jiji hilo, wanaliita A-Town na ukifanikiwa kushiriki vijiwe mbalimbali, utabaini jinsi mkoa huo ulivyozizima kutokana na kuzaliwa mtoto mwenye sehemu nne za siri.

Kila kona ya jiji hilo, anazungumzwa mtoto huyo kwa hali ya mshangao. Malaika huyo wa Mungu hajapewa jina lakini mama yake anaitwa Naishooki Logolie, 23, mkazi wa Kijiji cha Injok, Wilaya ya Arumeru, Arusha.


Kutokana na habari ya mtoto huyo kupata umaarufu mkubwa, huku wengi wakitaka kumjua zaidi, Uwazi lilimsaka mtoto huyo na kubaini maajabu mengine kwamba mbali na sehemu hizo za siri pia ana miguu mgongoni.

Kwa ushuhuda wa Uwazi, mtoto huyo ni wa kiume lakini ana sehemu za siri nne, tumboni, mgongoni, ubavuni na kwenye eneo la kawaida.

KAULI YA MAMA MZAZI
Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na Naishooki ambaye alisema: “Mwanangu nilimzaa kwa njia ya upasuaji kwenye Hospitali ya Olturumet, Halmashauri ya Arusha.”

Naishooki alisema hajui ni mtihani gani umempata kwani hakuwahi kuhisi tatizo lolote tumboni. Baada ya hapo, mwanamke huyo aliangua kilio na hakuweza kuzungumza tena.

Mama mzazi wa mtotot huyo.
Mama mzazi wa Naishooki (bibi wa mtoto huyo), Naishiye Logolie, alisema kuwa ni tukio la ajabu mno kutokea.
“Mtoto wangu akiwa mjamzito, hakuwahi kuonesha dalili za tatizo. Tumeshangaa kuona maajabu haya,” alisema Naishiye.

KAULI YA DAKTARI
Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga wa Halmashauri ya Arusha, Dk.Thobias Mkina alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanajaribu kufanya linalowezekana kuokoa maisha ya mtoto huyo.

“Matukio ya kuzaliwa watoto wakiwa na matatizo yanatokea lakini hili kidogo linaonekana kuwa la kipekee sana kutokana na maumbile ya mtoto,” alisema Dr.Mkina.

Alisema kuwa sababu za kitaalamu zinazoweza kusababaisha matukio ya aina hiyo ni matumizi ya dawa zenye kemikali wakati mama akiwa mjamzito.

Dokta huyo aliongeza, wakati mwingine kuna matukio ya kurithi kutoka kwa kizazi cha mhusika.
Hata hivyo alisema uchunguzi unaendelea na wakimaliza kwa upande wao watampatia rufaa kwenda katika hospitali kubwa zaidi.



MTOTO ATELEKEZWA
Taarifa za baadaye zinasema kuwa mtoto huyo aliepelekwa Hospitali ya KCMC, Moshi, Kilimanjaro kwa lengo la kufanyiwa upasuaji lakini wazazi hao baada ya kuambiwa gharama, walimtelekeza wodini.

Pia imejiridhisha kuwa mtoto huyo ametekezwa wodini kwenye hospitali hiyo, huku wazazi wake wakisema kuwa hawawezi kuishi na kiumbe huyo kwa madai kwamba ni laana kutoka kwa Mungu.

Blog hii inawashauri wazazi wa mtoto huyo kurudi KCMC kumchukua mtoto huyo. Kiumbe huyo ni malaika na hana kosa lolote. Uwazi linaendelea kumfuatilia mtoto huyo hatua kwa hatua na litakuwa linatoa ripoti ya maendeleo yake. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...