Bwana misitu wawili walikuwa kwenye doria mbugani, mara mmoja wao akatereza na kujigonga kwenye jiwe kichwani...
Yule mwenzake kuona vile mwenzake hatikisiki ikabidi achukue simu yake na kupiga kituo cha dharula...
Bwana misitu: "Halooooo, hapo ni kituo cha dharula???!!"
Kituo cha dharula: "Ndiyo, tukusaidie nini tafadhari??"
Bwana misitu: "Mimi ni bwana misitu wa mikumi, mwenzangu kadondoka na kufariki dunia..."
Kituo cha dharula: "Poleni sana, nachokuomba utulie na usipanic kabisa... Hapa tunaweza kukusaidia... Cha kwanza inabidi tuhakikishe kama kweli huyo mwenzako amekufa au kapoteza tu fahamu..."
Kabla mhudumu kituo cha dharula hajaendelea akasikia simu imewekwa chini, then mlio wa bunduki mara 2...
Yule jamaa akarudi tena kwa muhudumu na kumwambia,
"EBWANA DAAAAH, KWELI BWANA, KUMBE ALIKUWA HAJAFA, NIMEMKANDAMIZA BUNDUKI MOJA YA TUMBO AKAANZA TIKISIKA, NIKAMMALIZIA NA YA KICHWA MOJA AKATULIA KABISA.... NMESHA HAKIKISHA KUWA AMEKUFA MKUU... NINI KINAFUATA??!!!"
No comments:
Post a Comment