Baadhi ya wakazi wa Kigogo wakiwa juu ya paa la nyumba yao.
Wakazi Tandale wakiwa wamejikusanya kushuhudia mafuriko hayo.
Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Ally mkazi wa Kigogo akitoka ndani ya nyumba yao iliyozungukwa maji ambapo alimwambia mpigapicha wetu kwamba watoto na baadhi ya ndugu zake aliwaacha ndani ya nyumba hiyo.
Wakazi hawa wa Mwananyamala Kisiwani wakivuka eneo hilo wakiwa wamenyanyua baiskeli zao.
Wakazi wa Mwananyamala Kisiwani wakiwa juu ya paa la nyumba yao baada ya kushindwa kutoka kutokana katika nyumba hiyo.
Kina mama wakitoka katika nyumba yao iliyozingirwa maji.
Hawa walishindwa pia kwenda kufanya shughuli wakaishia kusubiri juu ya nyumba yao.
Mama na mwanawe wakitoka ndani ya nyumba yao Mwananyamala.
Kijana mkazi wa Mwananyamala Kisiwani akitoka ndani ya nyumba yao iliyojaa maji.
Mzee wa Mwananyamala Kisiwani akijiokoa na hatari ya mafuriko.
Wakazi wa Mwananyamala Kisiwani wakiwa na godoro lao juu ya paa la nyumba.
Wakazi wa Tandale wakijaribu kujiokoa baada ya kukaa ndani kwa muda mrefu.
Kijana akiwa haamini baada ya kukuta nyumba yao imezungukwa na maji wakati familia yake ikiwa ndani.
MVUA kubwa iliyoanza alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, imesababisha adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili ambapo wengi wao walijikuta katika matatizo makubwa baada ya nyumba zao kuzingirwa na kujaa maji. Mpigapicha wetu alitembelea baadhi ya maeneo ya Mwananyamala Kisiwani, Kigogo na Tandale na kujionea hali mbaya iliyosababishwa na mafuriko hayo ambapo baadhi ya watu walilazimika kupanda juu ya mapaa ya nyumba zao na wengine hawakuthubutu kutoka ndani kabisa kutokana na nyumba zao kuzungukwa na maji.
No comments:
Post a Comment