Tuesday, December 20, 2011

JYOTI AMGE WA INDIA NI MWANAMKE MFUPI ZAIDI DUNIANI


Jaji wa Rekodi za Dunia za Guinness, Rob Molloy (kulia) akizungumza na Jyoti Amge.
Jyoti Amge akiwa nyumbani kwake, Nagpur.
JYOTI AMGE ambaye amefikisha umri wa miaka 18 anategemea kupata habari nzuri hivi karibuni kwani atatangazwa kuwa ndiye mwanamke mfupi zaidi duniani kwa mujibu wa Rekodi za Dunia za Kitabu cha Guinness.

Amge, raia wa India, kutoka Nagpur, ana urefu wa sentimita 62.8, kiwango ambacho ni pungufu ya sentimita saba ya urefu wa Mmarekani Bridgette Jordan mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo tangu mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa Amge hiyo haikuwa rekodi yake ya kwanza, kwani  hadi  anatimiza miaka 18 alikuwa anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa kijana mfupi zaidi duniani, na baada ya kufikisha miaka hiyo sasa anakuwa ni mwanamke mfupi zaidi duniani.


Amge aliyekuwa analengwalengwa machozi na akiwa amevalia nguo zake nadhifu za ‘sari’, aliliita tukio hilo kuwa ni la kuongeza heshima kwa siku ya kuzaliwa kwake na kwamba alijisikia furaha kuwa mtu mdogo zaidi duniani ambaye anatambulika kwa walimwengu.

Mwanamke huyo ambaye anategemea kuwa mcheza sinema anasemekana amepungua urefu wake kwa sentimita moja mnamo miaka miwili iliyopita kutokana na hulka asili ya umbilikimo.

Rekodi ya mwanamke mfupi zaidi duniani inaendelea kushikiliwa na Pauline Musters ambaye aliishi Uholanzi tangumwaka 1876 hadi 1895 akiwa na urefu wa sentimita 61.

…akisali nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...