Haule akipokea kichapo kutoka kwa wananchi.
Askari akiingilia kati kumnusuru kijana Haule.
...Akimwinua Haule.
...Haule baada ya kichapo kutoka kwa raia.
...Askari akitokomea na Haule ili kumnusuru na dhahama hiyo.
...Safari kuelekea kituoni imeiva.
...Songa mbele.
...Haooo.
---
KIJANA mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, jana jioni alipokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kufutia bosi wake kumpigia mayowe ya “mwizi” katikati ya mji wa Morogoro.
Mwandishi wetu alipomhoji kijana huyo alidai kwamba yeye si mwizi bali alikuwa mfanyakazi wa mtu huyo, baada ya kuondoka nyumbani kwake kama wiki mbili zilizopita kutokana na mateso aliyokuwa akimfanyia, alikutana naye mjini na kupigia makelele ya “mwizi” akidai nguo alizovaa aliziiba kwake.
Kufuatia maelezo ya kijana huyo kundi hilo la watu lilimgeukia bosi wa kijana huyo likitaka kumshushia kichapo, lakini jamaa huyo alitoroka.
Polisi waliofika hapo waliondoka na kijana huyo pekee.
No comments:
Post a Comment