Friday, March 30, 2012

MAMA NA BINTIE WATWANGANA KUGOMBEA BWANA






Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam aliyetajwa kwa jina moja la Kesi ameibua timbwili zito baada ya kutwangana na bintiye Eliza wakidaiwa kugombea mwanaume...


NI TANDALE
Tukio hilo ambalo ni aibu isiyopimika lilifunga mtaa nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Tandale Mbuyuni, Dar hivi karibuni baada ya Eliza kumtuhumu mama yake mkubwa kuwa anatembea na bwanaa’ke.

Wakiwa kwenye pilikapilika za kazi zao, waandishi wetu walipigiwa simu na chanzo ambacho kilidondosha habari juu ya sekeseke ambalo lilikuwa linanukia kutokea maeneo hayo la mama na mtoto kutwangana kisa mwanaume.
HOT POT ilipotimba kwenye eneo la tukio, lilikuta umati ukiwa umejazana huku magari, Bajaj, pikipiki na baiskeli zikiwa hazina pa’ kupita.


PAMBANO LAIVU, WATU WASEREBUKA
Wakati wawili hao wakitwangana laivu, baadhi ya majirani, hasa akina mama walikuwa wakishangilia kwa kupiga ndoo kama ngoma huku wakiserebuka kwa furaha.
Ilibidi kuhoji majirani kulikoni watu kutwangana na wengine kufurahia ambapo walidai kuwa wamechoshwa na visa vya mama na mwanaye kuchukuliana mabwana.


MAMA ACHOROPOKA
Hata hivyo, mama huyo alifanikiwa kuchoropoka mikononi mwa bintiye baada ya kuzidiwa na kipigo ambapo alitoka nduki huku watu wakimkimbiza kwa kushangilia.


BINTI HEWANI LAIVU
Akizungumza na Ijumaa baada ya ‘mbaya’ wake kumchomoka huku akibubujikwa na machozi, binti huyo alisema kuwa siku moja kabla ya sekeseke hilo namba ya simu ya mama yake ilimpigia saa 4:30 usiku.

“Cha kushangaza, nilipopokea sauti ya upande wa pili haikuwa ya mama bali ilikuwa ya mwanaume wangu,” alisema binti huyo kwa uchungu.

Alisema kuwa jamaa huyo alikuwa akiongea kwa kujiamini na nyodo akimuuliza mpigaji ni nani na kwa nini alipiga simu usiku huo kwani wao wamelala, hawataki usumbufu.
“Niliielewa vizuri sauti ya bwanaa’ngu kwani tumeishi pamoja muda mrefu na tuna mtoto wa mwaka mmoja na nusu, nilishangaa sana, nilipomuuliza mama unalala na bwanaa’ngu, bila shaka akashtuka na kunijibu kwa kubabaika, “ alisema.

Alisema kuwa siku ya tukio hilo, wakati akiwa nyumbani hapo akimsubiri mama yake huyo ambaye alilala kwa bwanaa’ke huyo, alipigiwa simu na  mwanaume huyo na kumweleza kuwa hivi sasa yupo na mama hivyo yeye akae pembeni.
Baada ya kutia timu nyumbani, ndipo pakachimbika na kuzuka kwa timbwili hilo.
Hadi tunang’oa nanga eneo la tukio mama huyo alikuwa hajarejea nyumbani baada ya kupokea kichapo ‘hevi’.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...