Wiki tatu tangu msanii Steven Kanumba, apoteze maisha katika kifo tata, vionjo vya habari zinazomhusu staa huyo vimekuwa vikibadilika kutoka ladha hii mpaka ile na sasa Uwazi limedokezwa kuwa, marehemu ameacha pete ya ajabu.
Usiulize ameiacha wapi, denti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina la Judith Moris ,21, aliibuka wiki iliyopita na kusema, eti Kanumba alimvalisha enzi zile wakiwa marafiki wa kutupwa.
KWA NINI AMVALISHE?
Haraka ya kutaka kujua hili inaweza isiwe na baraka lakini dokezo la kwanza kutoka kwa binti huyo msomi linaeleza kuwa ni ombi alilomuomba marehemu la kumuwezesha kuwa staa wa Bongo kama alivyokuwa yeye.
Haraka ya kutaka kujua hili inaweza isiwe na baraka lakini dokezo la kwanza kutoka kwa binti huyo msomi linaeleza kuwa ni ombi alilomuomba marehemu la kumuwezesha kuwa staa wa Bongo kama alivyokuwa yeye.
“Mara ya kwanza kuonana na Kanumba ilikuwa mwaka 2010, alikuja kututembelea pale chuo, akaniomba namba na tangu hapo tukawa tunawasiliana.
“Kwa sababu nilikuwa nampenda na ndoto yangu ya maisha nilitaka kuwa maarufu kama yeye, siku moja niliomba anisaidie na mimi niwe staa, akakubali.
“Kuna siku alinipigia simu tukutane Tegeta kwenye mgahawa mmoja (jina tunalihifadhi), tukiwa hapo alinivalisha pete na kuniambia kuwa hiyo itanisaidia kwenye safari yangu ya kuwa staa,” alimeza mate msichana huyo kisha kuendelea na mtiririko wa maelezo.
BAADA YA KUVALISHWA ILIKUWAJE?
Judith alizidi kufungua semi kwa kuweka wazi kuwa, tangu alipovalishwa pete hizo alikuwa akishuhudia mauzauza au miujiza mingi iliyokuwa ikimtokea.
“Kwanza usiku nilikuwa naota ndoto za ajabu, halafu mchana kuna wakati pete ilikuwa inanibana ghafla kwenye kidole, nikimuuza Kanumba ananiambia kuwa nilikuwa eneo la hatari hivyo nilipaswa kuondoka,” alisema Judith.
Aliongeza kuwa, pamoja na kukubali kuivaa, marehemu hakuwahi kumweleza pete hiyo ni ya nini na imetoka wapi, zaidi ya kumsisitiza kuwa, ingemsaidia kufikia ustaa alioutaka.
MIUJIZA YA PETE
Kwa mujibu wa dada huyo ambaye alitinga ofisi za Uwazi Aprili 27, mwaka huu akiwa na pete hiyo mkononi ni kwamba, mbali na kubashiri hali ya hatari lakini imekuwa ikihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kimiujiza.
“Hii pete nimekuwa nikiiacha chumbani nashangaa naikuta sebuleni au hata sehemu ambayo sikuiweka,” Judith alisimulia maajabu ambayo waandishi wetu hawakuyaona licha ya kuwa na pete hiyo kwa zaidi ya saa 12 wakiichunguza.
VIPI APEWE MAMA KANUMBA
Kufuatia kifo cha Kanumba na kuongezeka kwa miujiza ya pete na minong’ono kuwa msanii huyo alikuwa mwanachama wa Freemason, denti huyo ameingiwa na kiwewe kiasi cha kupanga kumpelekea mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa ili aone namna ya kumsaidia.
“Zamani nilikuwa nikipata utata juu ya pete hii, nilikuwa namuuliza Kanumba lakini sasa hayupo unadhani nitafanyaje, ni lazima nimpelekee mama yake huwenda akawa anafahamu namna ya kunisaidia ili nisidhurike,” alisema Judith.
HALI ILIVYO MITAANI
Tangu nyota ya Kanumba ilipozimika ghafla Aprili 7, mwaka huu, mitaani kumekuwa na hali ya sintofahamu juu ya maisha na kifo cha msanii huyo nyota anayedaiwa kuuawa na Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa kusukumwa kufuatia ugomvi wa kimapenzi.
Baadhi ya watu wamekuwa wakidai kutokewa kimazingara na Kanumba, huku uvumi mwingine ukimhusisha msanii huyo na imani za Ki- Freemason kiasi cha kuwepo kwa madai kuwa staa huyo hajafa bali amechukuliwa kimiujiza.
KUTOKA DAWATI LA UWAZI
Pamoja na kuwepo kwa maelezo mengi ya kutisha na kusisimua juu ya matukio ya pete hiyo ambayo imetajwa kuwa na alama za Freemason, dawati limeona vyema kujiridhisha kwanza na madai hayo kabla ya kuyachapisha kwenye gazeti.
No comments:
Post a Comment