Wednesday, May 2, 2012

Uzao wa Lulu na Kanumba utata...



Huku ikiwa bado kifo cha msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba hakijafutika kwenye akili za wengi, limeibuka suala lingine lenye utata kati yake na aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Suala hilo ambalo limekuwa likichukua nafasi kubwa katika mazungumzo ya wadau ni kuhusu uzao wao kwani wanaonekana kushabihiana katika mambo mengi kiasi cha kuacha viulizo vingi.


KufanaNa kwa baba zao
Imebainika kuwa baba wa marehemu Kanumba, Charles Kusekwa Kanumba na baba wa Lulu, Michael Kimemeta wanafanana sana kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuhisi ni ndugu.

Kufanana kwa wawili hao kumekuja baada ya hivi karibuni baba wa Lulu kuibuka na kutoa ufafanuzi kuhusu mwanaye ambaye anakabiliwa na kesi ya kuhusika na kifo cha Kanumba.


Kabila la mama zao
Aidha, mama wa Kanumba, Flora Mtegoa na mama Lulu, Lukresia Karugila wote ni Wahaya na mama Lulu aliwahi kukaririwa akidai yeye na mama wa marehemu ni ndugu.

Hata hivyo, mama Kanumba aliwahi kukanusha kuwa hana undugu na mama Lulu na kusisitiza kutomjua licha ya kusikia tu kwamba ni Mhaya mwenzake.


Wote wamelelewa na mama zao
Historia ya malezi ya Lulu na Kanumba inafanana kwani wote wamekulia mikononi mwa mama zao huku baba zao wakiwa hawana mawasiliano mazuri na wazazi wenzao.

Lulu mpaka anakumbwa na balaa linalomkabili, amekuwa kwenye malezi ya mama yake kwa muda mrefu huku sababu za wazazi wake kuishi mbalimbali zikiwa hazijulikani.

Naye Kanumba mpaka anafikwa na mauti alikuwa akilelewa na mama yake na imeelezwa kuwa alikuwa akiishi na Bi. Flora tangu alipokuwa anasoma darasa la nne.

Mazingira hayo ndiyo yanayoibua utata juu ya uzao wa Lulu na Kanumba ambao inadaiwa walipanga kuja kuoana baadaye. 

Hata hivyo, kufafana kwao katika maeneo mbalimbali hakuwezi kufanya hitimisho la kwamba wana uhusiano wa karibu ila huenda imetokea tu.

No comments:

Post a Comment