Wednesday, May 2, 2012

UJAUZITO WA LULU; MAMA KANUMBA ATOA TAMKO.....





WAKATI ikidaiwa kwamba tumbo la msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ lina kitu ndani yake kinachohusishwa na marehemu Steven Charles Kanumba, mama mzazi wa marehemu, Flora Mtegoa ametoa tamko kuhusiana na tumbo hilo...

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, mama Kanumba alisema kuwa kwa sasa hawezi kutoa uamuzi wowote kuhusiana na tumbo hilo la Lulu mpaka pale atakapopata uhakika wa kile kilichomo ndani yake.

“Tusubiri, kwanza Lulu simfahamu na wala sijawahi kutambulishwa na mwanangu wakati alipokuwa hai, sasa siwezi kusema kitu kwa kuwa sijui kama kweli ni mjamzito,” alisema mama huyo.

Alipobanwa zaidi na mwandishi wetu aliyetaka kujua kama ikithibitika kwamba Lulu ni mjamzito, je, atampokea mjukuu wake au la, mama huyo alimtaka mwandishi kuvuta subira hadi pale mambo yakapofahamika baadaye.

“Sioni mantiki ya kuzungumzia suala hilo kwa sasa, nakuomba tuvute subira kwanza kwa sababu hapo kuna mambo mengi ya kuangalia kabla ya kufanya uamuzi,” alisema.

Mama Kanumba amekataa kuwatambua watoto waliodaiwa kuwa wa marehemu mwanaye baada ya wanawake kadhaa kujitokeza na kudai kuzaa na Kanumba kwahoja kwamba marehemu hakuwahi kumwambia kama ana mchumba au watoto enzi za uhai wake.

Pia, mama huyo ametumia fursa hii kukanusha kuwa mpaka sasa ni wanawake wawili tu waliojitokeza kudai kuzaa na marehemu Kanumba na wala si watano kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment