Tuesday, May 22, 2012

DAWA KIBOKO YA UKIMWI YAANZA KUTUMIKA MAREKANI



Dawa aina ya Truvada yenye uwezo wa kuzuia maambuzi ya virusi ya Ukimwi (HIV).

Dk. Lisa Sterman akiwa na chupa nyenye dawa hiyo.

AINA moja ya dawa iliyothibitishwa kuwa ni kiboko ya Ukimwi na uwezo wa kuzuia maambuzi ya virusi ya Ukimwi (HIV), imepiga hatua muhimu ya kukubalika kutumika nchini Marekani.
Jopo la madaktari washauri wa serikali ya Marekani wameidhinisha matumizi ya dawa hiyo aina ya Truvada kwa watu walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya HIV.
Dawa hiyo, Truvada imekuwa ikitumika nchini humo na watu walio na virusi vya Ukimwi tangu mwaka 2004 lakini ilikuwa haijaidhinishwa.
Utafiti umeonesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwakinga watu wasiokuwa na virusi hivyo dhidi ya maambukizi.
Truvada ilianza kutajwa na kuandikwa katika vyombo vya habari nchini Marekani mwaka 2010 baada ya watafiti wa serikali kugundua kuwa inaweza kuzuia maambukizi ya HIV.
Utafiti wa miaka mitatu umebaini kuwa utumiaji wa dawa hiyo ambayo ipo katika muundo wa vidonge, ili kumkinga mtu na maambukizi, mtumiaji atapaswa (hasa mashoga ambao wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi), watatakiwa kumeza vidonge hivyo kila siku.
Utafiti wa mwaka jana uligundua kuwa Truvada ilipunguza maambukizi kwa asilimia 75 nchini humo baada ya kufanyiwa uchunguzi watu ambao ni patna ambao mmoja alikuwa na maambukizi.
Nick Literski, mfanyakazi katika shamba moja nchini humo ambaye mpenzi wake ana HIV alipofanyiwa utafiti kwa mwaka mmoja aligundulika hajapata maambukizi na alikuwa akilipa Dola za Kimarekani 40 (T sh. 64,000) kwa mwezi, bei ambayo imeonekana kuwa ingefaa kutumika.
Hata hivyo, sasa dawa hiyo inauzwa kwa dola za Kimarekani 900 (Tsh. 1,440,000) kwa dozi ya mwezi mmoja na kwa wale ambao watanunua kwa mwaka itawabidi watoe dola za Marekani 11,000 (T sh.11,600,000) hivyo kusababisha taasisi moja nchini humo iitwayo The AIDS Health Care Foundation kupinga gharama hizo na kudai kuwa ni kubwa mno.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 1.2 nchini Marekani wana maambukizi ya HIV.

No comments:

Post a Comment