Tuesday, May 8, 2012

AKIMBIWA NA MUME BAADA YA WATOTO KUVIMBA VICHWA





Sophia Rashid.

“HAYA ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si kazi ya binadamu, nasikitika kwa sababu mume wangu amenitelekeza baada ya kuona watoto wamevimba kichwa,” hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sophia Rashid , 22, mkazi wa Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambaye anauguza wanaye wawili wanaosumbuliwa na uvimbe wa kichwa.

Mama huyo alisema watoto wake hao aliwazaa wakiwa na matatizo ya kuvimba vichwa kutokana na kujaa maji, hali ambayo inamfanya akose raha.

“Kwangu sasa imekuwa ni matatizo makubwa mwanangu Omari mwenye miaka minne na Maulid mwenye miezi kumi wanasumbuliwa na ugonjwa mmoja ambao umesababisha baba yao kuwakimbia,” alisema mama huyo akiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) Muhimbili.

Aliongeza kuwa, tangu alipofika hospitalini hapo wiki mbili zilizopita, amekuwa akipata msaada kutoka kwa maofisa wa ustawi wa jamii wa Moi lakini ndugu zake hawafiki kabisa kumjulia hali.
Daktari mmoja hospitalini hapo aliyezungumza kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini alisema kuwa, hali hiyo huwapata watoto kutokana na kuwa na upungufu wa madini ya pholic acid na mjamzito kukosa lishe bora wakati wa ujauzito.

MSAADA
Kutokana na matatizo hayo mama huyo anaomba kusaidiwa na mtu yeyote aliyeguswa na masaibu yake kifedha, chakula, mavazi, dawa pamoja na kipimo cha TC Scan ambacho alidai kuwa kipo katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam na gharama yake ni shilingi 258,000 kwa mtoto mmoja.
Atakayependa kumsaidia mama huyo atumie simu namba 0716755384 au afike Hospitali ya Muhimbili, Moi kwenye wodi A.

No comments:

Post a Comment