Friday, April 27, 2012

MAHABA: Ni MARA 100 kuwa SINGLE kuliko kuwa na mpenzi PASUA KICHWA...





Kila mtu angeyaheshimu mapenzi, angejua jinsi ya kulinda hisia za mwenzi wake. Angeelewa maana ya kupenda, asigekuwa na shaka pale anapopendwa. Angeishi ndani ya mwenzake, hivyo kuumizana kusingekuwepo, migogoro mikubwa na kuachana isingetokea.
Migogoro mingi inatokea kwa sababu wengi wameyageuza mapenzi kama mchezo (game), hawajui kuwa saikolojia inaonya vitendo vya kuucheza shere moyo wa mtu. Kumfanyia hivyo mtu mwenye hisia za ndani na za kweli katika kupenda unaweza kuua bila kukusudia.
Katika sehemu ya kwanza ya makala haya wiki iliyopita, nilieleza kuwa kama hujawa tayari kupenda, kunyenyekea na kuheshimu ni vizuri ukakaa pembeni kwa sababu unaruhusiwa kucheza game na mtu lakini ni kosa kubwa kucheza game na moyo wa mtu.
Hata hivyo, nilitaka kila mtu awe makini anapokuwa anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu.
Anapaswa kujihakikishia upendo kutoka moyoni badala ya kujaribu. Wengi walioingia kwa mtindo wa kupima kina cha maji, walilia kwa kusaga meno.
Lipo tabaka ambalo linakuwa limejitosheleza kuwa mapenzi hamna lakini wanang’ang’ania, matokeo yake wanauguza jeraha la moyo kwa muda mrefu. Wengine wakajipa ugonjwa wa moyo. Ni vizuri kuwa makini mno ikiwa unahitaji kupata thamani halisi ya penzi.
Pigania kuhifadhi moyo wako. Uweke katika himaya salama. Usijidanganye kwa penzi lisilo na uelekeo.
Lenye sura ya upande mmoja. Wewe unapenda, yeye anakuchora, presha inakupanda na kushuka mwenzako hana habari hata kidogo, tena ikiwezekana atakucheka kama katuni.
 Kuna watu hawaoni hili umuhimu, mpenzi maana yake ni msiri wa maisha yako. Unapokuwa umelala fofofo hujitambui, ubavuni kwako yupo yeye. Anaweza kukufanya lolote wakati wewe unaogelea ndotoni. Mpende akupendaye, vinginevyo utakumbana na maumivu yafuatayo;
HATOKUSIKILIZA IPASAVYO
Mapenzi ni hisia. Ni rahisi kwako kujua kwamba uliyenaye anakupenda kwa dhati  mnapokuwa mnazungumza. Je, anakusikiliza kiasi gani?
Mtu ambaye hana mapenzi na wewe, hata umwambie kwa lugha gani hawezi kukuelewa. Tena inawezekana ulizungumza naye jana kwa herufi kubwa, lakini leo jua limechomoza anarudia yale yale.
Inawezekana ulimuonya kuhusu tabia ambazo zinakufanya heshima yake ipotee. Hakatazwi kuwa na marafiki wa jinsia nyingine, lakini mazoea yake siyo mazuri kiasi kwamba wanaweza kutembea barabarani wameshikana viuno. Ikiwa unamueleza habadiliki, huyo hakupendi.
Hakusikilizi kwa sababu hana hisia na wewe.

Itandelea...

No comments:

Post a Comment