Tuesday, February 21, 2012

LAANA: Wake za watu wavua nguo HADHARANI



DUNIA imekwisha! Kitendo cha wake za watu kuvuana nguo hadharani tena mbele ya watoto kilichojiri hivi karibuni mjini hapa, kimetafsiriwa kuwa ni laana...

NI TUKIO LA AIBU
Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilijiri Jumapili iliyopita kwenye sherehe ya kumtoa nje mtoto aliyekuwa anatimiza siku 40 tangu alione jua, lilisababisha bibi wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina moja la Bi Matha kuangua kilio kwa kushindwa kuvumilia uchafu huo.

Katika shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Bi Matha, mtaa wa Kibodya jirani na Msikiti wa Mwembesongo mkoani hapa, ilipambwa na matukio makuu matatu.

Tukio la kwanza lilikuwa ni Maulidi ya kumtoa nje mtoto huyo lillilofanywa na Madrasa ya Alhasaniyyah ya Msikiti wa Kingo mjini hapa ambapo watu walikula nyama ya mbuzi, maandazi na chai.

Tukio la pili ni baada ya masheikh waliofika kumuombea dua mtoto huyo kuondoka eneo hilo, mama wa mtoto aliyetajwa kwa jina moja la Amina kwa kushirikiana na mashosti zake, walianza shughuli ya kusasambua kwa kuligombea sanduku la zawadi za mama mtoto ambapo zoezi hilo liliongozwa na bendi ya matarumbeta.

‘KUFULI’ NJE
Wakati wakiendelea kusasambua, mmoja wa wanawake hao, alipanda juu ya meza ambapo baadhi ya mashosti zake walimvua khanga aliyokuwa amevaa hivyo kumfanya aache wazi sehemu zake nyeti.

HAIJAWAHI KUTOKEA
Katika tukio hilo ambalo halijawahi kutokea, wanaume walikuwa wakitokwa udenda huku watoto nao wakishuhudia uchafu huo wa mama zao.

Tukio la tatu lilikuwa ni disko la usiku maarufu kama kigodoro, huku ndiko kulifanyika matukio ya laana kubwa ambapo vitendo vya ngono vilichukua nafasi kubwa.
Baada ya kuwepo kwa mvutano mkubwa baina ya ‘memba’ wa familia hiyo ambao hawakukubaliana na shughuli hiyo ya kusasambua, ‘polisi’ wa Ijumaa alizungumza na wahusika mmoja baada ya mwingine.

BIBI WA MTOTO ANASEMAJE?
Bi Matha ambaye alishindwa kuvumilia vitendo hivyo vilivyoitia aibu familia na kufikia hatua ya kukosa amani, aliliambia Ijumaa kuwa hakupendezwa na vitendo vilivyofanywa na binti yake kuruhusu mashosti zake kuvuana nguo kwenye shughuli ya mjukuu wake.

BABA AFUNGUKA
Kwa upande wake baba mzazi wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina moja la Abdallah alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimkataza mke wangu jambo hilo lakini alikaidi kwa kujitetea kwamba naye huwa anawachangia wenzake kwenye matukio kama hayo hivyo ilikuwa zamu yake kuchangiwa. 

“Kwa kuwa shughuli ilikuwa inafanyika kwa mama yake nikawa sina uwezo wa kuzuia, lakini niseme tu kwamba mimi nina hofu ya Mungu ndiyo maana niliamua kumtoa mwanangu kwa kumsomea dua ya Maulidi.”

MAMA ASHANGAA
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Amina Said alijitetea kuwa anashangaa watu kugeuza suala hilo kuwa ‘mjadala wa kitaifa’ wakati ni jambo la kawaida.

DINI INARUHUSU?
Ili kusikia kauli ya viongozi wa dini  kuhusiana na tukio hilo, Ijumaa lilizungumza na ustadhi wa madrasa ya Alhasaniyyah, Sheikh Thenei Jaafar ambapo alikiri kusononeshwa na kulaani vikali tukio hilo.

No comments:

Post a Comment