LILE sakata la mfanyabiashara nguli wa kuuza mbao jijini Dar es Salaam kunaswa akiwa na denti kitandani, limechukua sura mpya baada ya kuwepo madai kwamba mzee huyo amepigwa faini ya shilingi milioni 3 na kukubali kuzilipa...
Kwa mujibu wa chanzo (kilichoomba hifadhi ya jina), faini hiyo ilipigwa kwenye eneo la tukio ambapo mfanyabiashara huyo alisema atailipa bila shaka ilimradi mambo yasiende mbele.
Habari zaidi zinaweka wazi kuwa ilibidi familia ya denti huyo ijiridhishe kwamba, kweli mwanaume huyo amekubali kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kumuwekea karatasi jeupe na kalamu yenye wino mweusi ili aweke makubaliano hayo katika maandishi.
“Jamaa (muuza mbao) alipopigwa faini ya shilingi milioni tatu, akakubali, akaletewa karatasi na kalamu ili amwage wino kama ushahidi,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na familia ya denti huyo.
Amani lilimuuliza jirani huyo kuwa kiasi hicho cha fedha kitafidia kitu gani katika fumanizi hilo?
“Aaa, kuna mambo mengi, sijui kwa familia ya binti huyu, lakini kama ni sisi kwetu, zingepangika sawasawa mpaka senti ya mwisho.
“Mfano, aibu ya familia mtaani itakuwa shilingi laki 9. Unajua lazima mtaa mzima ulijua. Halafu kumvua nguo binti, ule nao ni usumbufu, ni shilingi laki 5.
“Haiishii hapo, kuna kumsababishia maumivu, yule ni binti hata kama amefikisha miaka 18, lakini lazima kuna maumivu, ni shilingi laki 7. Haya, kuna shilingi laki 9 kwa ajili ya wajomba watatu.
“Angekuwa ameolewa, fedha yote ingekwenda kwa mumewe, lakini sasa lazima wajomba wapate wao. Laki tano zinazobaki anapewa mama, pole kwa binti yake kutendewa vibaya. Binti yeye yake ni ile laki 5 ya maumivu,” kilisema chanzo hicho.
UTAMU ilifika nyumbani kwa akina Fatty (binti aliyenaswa na kigogo huyo) kwa lengo la kutaka kuzungumza na mama yake mdogo aliyeendesha zoezi hilo, lakini mtu aliyekutwa nyumbani hapo, alisema mlezi huyo alitoka kwa shunghuli zake za kila siku.
Utamu: “Nani yupo ambaye ni msemaji wa familia?”
Aliyekutwa: “Mh! Kusema ukweli hayupo.”
Utamu : “Tumesikia kuwa mwanaume aliyenaswa akiwa na Fatty amepigwa faini ya shili…”
Aliyekutwa: “Sikilizeni, mimi sijui lolote lile, huna haja hata ya kumalizia kusema.”
Januari 26-Februari 01, 2012 ukurasa wa blog hii kulikuwa na habari yenye kichwa; KIGOGO AFUMWA NA DENTI. Katika habari hiyo, mfanyabiashara maarufu wa kuuza mbao jijini Dar, Kyando (pichani) alinaswa chumbani akiwa na msichana aitwaye Fatty ambaye anadaiwa ni mwanafunzi.
No comments:
Post a Comment