Thursday, August 25, 2011

IRENE ANDERSEN MWANAMAMA MTUNISHA MISULI ANAYEOGOPEKA

IRENE ANDERSEN ni mwanamama aneyetisha katika utunishaji misuli kutoka nchini Sweden.

Ni mwanamke anayetisha kwa sababu mchezo huu wa kutunisha misuli umezoeleka kuwa ni kwa ajili wa wanaume tu. Inashangaza kuona mwanamama mwenye misuli mikubwa kama Irene.

Mchezo wa kutunisha misuli kwa akina mama ulianza mwishoni mwa miaka ya 1970 ambapo wanawake walianza kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya utunishaji misuli.   Irene ni mmoja wa waanzilishi wa mchezo huo.

Irene alizaliwa Denmark mwaka 1966, baadaye alihamia Sweden akiwa na umri wa miaka miwili pamoja na wazazi wake.

Alikulia Malmo na baadaye kuhamia Gothenburg wakati akiwa na umri wa miaka 20. Amekuwa akitumia muda wake mwingi katika 'gym' akifanya mazoezi makali ili kujenga mwili wake huu wa maajabu.

Irene mwenyewe alikuwa na haya ya kusema: "Nimekuwa nikijifunza maisha yangu yote... Wakati nikiwa mdogo, nilianza na jazz ballet na judo na nilipokuwa na umri wa miaka 15 ndipo nilipoanza mchezo wa kutunisha misuli.

Rafiki yangu alikuwa anamiliki gym na ndiye aliyenifanya niupende sana mchezo huu. Tangia hapo, nimekuwa nikifuatilia kila kitu kinachohusiana na mchezo wa kutunisha misuli kwa wanawake".

Vilevile Irene anaweza michezo ya Kick na Thai boxing, hivyo tunawashauri kutomtania  mwanamama huyu pindi muwapo mitaani na mmchukulie kama wanawake wengine.



Zifuatazo ni picha mbalimbali za mwanamama Irene:









No comments:

Post a Comment