Monday, August 1, 2011

AFANDE LIVE...

PICHA za utupu za afande wa kike aliyetambuliwa kwa jina la Mary kutoka Kituo cha Polisi wilayani Nyamagana, jijini Mwanza zimedakwa na Amani.

Picha hizo zinamuonesha afande huyo akiwa hana nguo zaidi ya ‘kufuli’ tu, amepozi juu ya kitanda huku akionekana kumkodolea mtu pembeni yake.

Hata hivyo, moja ya picha hizo, inamuonesha WP Mary akiwa katika sare ya kazi ofisini na pembeni yake kukiwa na mafaili yenye kumbukumbu mbalimbali.

Baada ya kuzinasa picha hizo, gazeti hili lilifanya uchunguzi kwa miezi kadhaa ili kujiridhisha pamoja na kumpata mhusika kuthibitisha kama pichaa hizo ni za kwake na alipiga kwa lengo gani.

Hivi karibuni mwandishi wetu alimbamba askari huyo katikati ya Jiji la Mwanza akiwa ameongozana na mwanaume aliyemtambulisha kuwa ni mchumba wake.

WP huyo aliposomewa mashitaka yake ikiwa ni pamoja na kuoneshwa picha hizo, aligwaya na kuhoji jinsi zilivyopatikana huku akijaribu kukwepa tuhuma kwa kusema sura ni yake lakini kiwiliwili siyo.

Katika hali isiyotarajiwa WP huyo alipiga mkwara akidai kwamba, ishu hiyo inafahamika hata kwa wakubwa wake wa kazi, hivyo haimsumbui  wala kumpandisha mapigo ya moyo na kusisitiza atajiwe chanzo cha picha hizo kudakwa na Amani.

Alipoelezwa kuwa ni kosa kwa mwandishi wa habari kutaja chanzo chake cha habari, ndipo alipokiri kuwa, picha hizo ni zake lakini akagoma kueleza alizipiga kwa lengo gani.

Akionekana kuhamanika usoni na kukumbwa na taharuki, askari huyo alimsihi mwandishi kutozitumia gazetini picha hizo kwa kuwa zitamsababishia kufukuzwa kazi wakati anategemewa na familia kubwa.

“Picha ni zangu kweli naomba unisaidie, zikitoka gazetini nitafukuzwa kazi, maana ninawasomesha wadogo zangu na wazazi wangu wananitegemea,” alilalama WP Mary.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na askari wake kupiga picha za utupu alionesha kushtushwa, akasema ikibainika ni kweli afande huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Kama ni kweli kapiga picha za utupu, hiyo ni kinyume cha maadili, askari anapaswa kuwa mfano kwenye nidhamu, ikithibitika tutamchukulia hatua za kinidhamu,” alisema Kamanda Sirro.

3 comments:

  1. Be a soldier, president,or judge, a woman is always a woman, they posses a larger amount of weakness,do not judge her as if she is an angel, and gud thing is to put yourself on her shoes 1st n then judge.

    ReplyDelete
  2. sio fresh global publisher walivyofanya wengi wanafanya hivyo just for fun tu!kama hivyo kapigwa na mpenz wake maskin kweny cm ili ajione alivyoumbika maskin so kwa bahat mbaya m2 akiznasa ndo wanaharibiana,sasa dada wa wa2 maskin akifukuzwa kaz ss gazet ndo lnajenga ama linabomoa 2cfikirie kuandika habar 2 kwa ma2mbo ye2 yenye uhakika tuwaangalie wasiokuwa na uhakika kwanza!,,,imenikera sana!

    ReplyDelete
  3. tabia yenu sawa na mashetani.mnabomoa wala hamjengi.mtalipia kila tendo lenu global

    ReplyDelete