Thursday, October 25, 2012

HOT HOT MAGAZETINI LEO...


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

DUNIA IMEKWISHA: KICHANGA CHAOKOTWA KIKIWA KIMETUPWA CHINI YA MLIMA KIVES




Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuuangalia mwili wa kichanga hicho

Hizi ni picha tulizozipata kwenye mtandao wa Jamii Forum zikiwa na maelezo: MAJONZI, HUZUNI, NA SIMANZI ZIMETAWALA LEO MAENEO YA KIJENGE JUU KATA YA KIMANDOLU ILIYOKO MKOANI ARUSHA BAADA YA KITOTO KICHANGA KUKUTWA KIMETUPWA CHINI YA MLIMA KIVESI. 

Hakuna maelezo kuwa kichanga hicho kinekutwa hai kwakuwa mtu aliyeweka picha ametumia maneno kama ‘mwili’ wa mtoto huyo kumaanisha kuwa hakuwa hai. .


Mtoto mwenye umri wa siku moja wa jinsia ya kike akiwa amewekwa kwenye ndoo na kutupwa



Afisa wa polisi akiuchukua mwili wa mtoto huyo uliofungwa na kanga na kutolewa na msamaria mwema muda mfupi baada ya kutaarifiwa kuhusu tukio hilo

P-Diddy APATA AJALI.......


P-Diddy amepata ajali maeneo ya Beverly Hills hotel Los Angeles Marekani....
Baada ya gari lake kupata ajali na kumsababishia majeraha mbalimbali kwenye mwili wake..











KITCHEN PARTY YA AUNT EZEKIEL YAFANYIKA MLIMANI CITY




 Aunt akiwa kazini......
Mashosti wako kiafrika zaidi.

Aunty akitambulisha mashosti zake

MADEE AJITOA TIP TOP CONNECTION...


MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha pande za Manzese, Hamad Ally ‘Madee’, kutoka kundi la Tip Top Connection, inadaiwa kuwa amejitoa katika kundi hilo, na sasa anataka kufanya muziki kivyake na sababu za kujitoa kwake bado hazijulikana.

Chanzo chetu cha habari kilichozungumza nasi, kwa sharti la kutotajwa kwa jina lake kilidai kuwa wiki iliyopita msanii huyo alikuwa kwenye mzozo na mmoja wa wasanii wa kundi hilo lakini waliweza kupatana ingawa jamaa bado anaonekana kutopenda kile kilichotokea lakini bado kuna vitu vingine vya ndani zaidi vilivyosabisha hadi jamaa kuamua kujiweka pembeni.

Chanzo hicho kilichopo karibu na wasanii hao hakikusita kueleza kuwa ndani ya kundi hilo kuna matatizo mengi, kwani hata kuondoka kwa baadhi ya wasanii waliokuwa hapo kulisababishwa na matatizo hayo ambayo yamemfanya Rais huyo manzese kujiengua, ingawa bado kuna mvutano mkubwa unaoendelea ili kumrudisha kundini jamaa huyo bila taarifa za mkwaruzano huo kutoka nje. 

Tuesday, October 23, 2012

WATUHUMIWA WA UCHOMAJI MAKANISA MBAGALA WAPANDISHWA KIZIMBANI TENA





WATUHUMIWA wa kuharibu na kuchoma moto makanisa huko Mbagala jijini Dar es Salaam, mapema leo wamefikishwa mbele ya Hakimu Binge Mashabala wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Watuhumiwa hao watano wamesomewa mashtaka matano na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, yanayowahusisha na njama za kutenda makosa, kuvunja majengo, uharibifu na wizi wa vifaa vya makanisa na kusabisha hasara ya milioni 550/=. 

Washitakiwa hao, Shabani Hamisi, Issa Abdullah, Kambi Haji, Hamadi Mahambo na Wajabali Julius, walikana makosa hayo na kesi kuahirishwa hadi Oktoba 30 mwaka huu.

JALADA LA KESI YA LULU MICHAEL LAPELEKWA KISUTU KUANZA KUSIKILIZWA UPYA!!!



MSANII  wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, amehoji Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu lilikofikia jalada la kesi.

Lulu aliuliza swali hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Stuarti Sanga baada ya Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi wake haujakamilika.

Baada ya Sekwao kueleza hiyo, Lulu alinyoosha mkono na kuhoji jalada la kesi inayomkabili lilikofikia.

Hakimu Sanga alimuuliza Wakili Sekwao iwapo anauliza jalada halisi au la kudurufu. 

Wakili Sekwao alimwambia Hakimu Sanga kuwa, anaulizia jalada halisi.Hakimu Sanga alimwambia Lulu kuwa jalada halisi limekwisharudi  na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu itakapotajwa tena.

Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwa Kanumba, Sinza, Dar es Salaam.

Monday, October 22, 2012

Harusi ya video vixen/model Cynthia Masasi na Richard Mziray

Mr and Mrs Mziray


Jana ilikuwa ni siku mpya kwa former video vixen/model, Cynthia Masasi aliyefunga ndoa na Richard Mziray. Baada ya kubadilisha status na kuwa Mrs Mziray, mrembo huyo ana ujumbe huu mfupi:

“Aaaaaaaaaaw im the luckiest woman in the whole world! Thank u all for the lovely msgs I AM NOW MARRIED to my Best Friend, The man of my dream! Thank GOD for everything! So i have to make this CLEAR. Cynthia Masasi-Mziray is SAFE & SOUND! I have not been in jail for one sec LEO, Sasa napigiwa simu back2back kwamba kuna watu wanasema wameniweka ndani na wanafuraha sana! To clear things up ni kwamba niko home na nina bbq na wakwe walikuwa wananikabidhi jiko “Kimila za Kipare” So jela sijapelekwa na dada yeyote naona wameona wajipe promo kidogo! 

Harusi yangu IMEWACHANGANYAA huo ndio ukweli! So thanks to yall for ur calls msgs and ur concerned abt my safety! NIKO POA BALAA NA MUME NIMPENDAE MPAKA KUFAAA! LOVE YALL MY TRUE PPL..”

 


Kitu cha chopper kikiwasubiri maharusi
Congrats Cynthia


TUMEANZIA KANISANI ....AZANIA FRONT!!....WAMEEELEKEA AIRPORT KUPAA MAWINGUNIIII... REFRESH ZE PAGE...UENDELEE KUENJOY!!




INSTAGRAM!!..
.KUTOKA KWA FLAVIANA MATATA

 HAPA WAKIELEKEAMAWINGUNI ;)







Mamaake ndo alimkabidhi



























u may kisss ze bride!!
                              KUONA ZAIDI YALIYOJIRI DUMBUKIA HAPO CHINI, KUNA RED CARPET NA SWAG ZA HAPA NA PALE

ONJA!!!! :: CYNTHIA & RICHARD RECEPTION

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...