Sunday, October 23, 2011

AISHA MADINDA KULIPWA MILIONI 500!!!


Kampuni ya Global Publishers Ltd, inayochapisha magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda, Risasi na Amani iko tayari kumlipa kiasi cha shilingi Milioni mia tano, mnenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ ikiwa atatoa uthibitisho kwamba, picha za utupu alizopigwa nchini Afrika Kusini ni za kutengenezwa, soma data chini.

Ofa hii imekuja siku mbili baada ya gazeti moja la michezo na burudani linalotoka mara mbili kwa wiki kuchapisha makala kuhusu Aisha akikanusha kuwa, picha zile si zake na kwamba zilitengezwa na mbaya wake kwa lengo la kumchafua jina.
...kulia kwake ni unga..bila shaka ulimpotezea kumbukumbu

Hata hivyo, katika makala hayo, Aisha alishindwa kuthibitisha picha hizo ni za kutengeza, zilitengnezwa wapi na lini na vigezo gani vinavyoonesha picha hizo ni za kutengeneza.

Ushahidi wa Global kuwa, picha hizo ambazo za mnato na video ni za Aisha mwenyewe upo wazi na hakuna shaka yoyote.

Moja ya ushahidi huo, katika picha za video, kuna sehemu Aisha anaongea kwa tambo akiwaponda watu wanaomfuatafuata na kumsema vibaya.
...sasa hapa inakuwaje picha hizi zikitoka gazetini...!!!!
Tunamnukuu: “Wanasema eti nimeishiwa, nimekosa nauli ya kurudi Tanzania, waende basi kwa huyo Asha Baraka wakaseme, maana wamezidi kwa maneno.”

Hata hivyo, sehemu kubwa ya picha za mnato na video hizo zinaonesha wazi kwamba, Aisha alikuwa tayari kupigwa picha hizo, kwani kuna wakati alikuwa akitazama kamera na nyingine akiwa ameweka pozi.
......aaa jamani...niacheni ki mpango wangu!!!!

Aidha, ushaidi mwingine kuwa picha hizo ni Aisha, mara baada ya kutua Bongo akitokea Afrika Kusini, alimwangukia bosi wake, Asha Baraka akimwomba radhi kwa yote aliyoyafanya Afrika Kusini ambapo ililiripoti likiwa na kichwa cha habari; NATESEKA.

Katika habari hiyo, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alinukuliwa akisema kuwa, anaamini Aisha aliteleza na hivyo ameamua kumsamehe na kumrudisha kundini kuendelea kupiga mzigo kama kawa.
....ntajua ntakachowaeleza watanzania....

Tunamnukuu Asha Baraka: “Mimi kwa Aisha ni kama mama au dada yake, na ninavyojua, mtoto anapojisaidia kiganjani mzazi huwezi kuukata mkono bali utausafisha kisha kuyaacha mambo yaendelee. Vivyo hivyo kwa Aisha, kafanya kosa lakini hakuna kosa lisilostahili msamaha, kwahiyo asamehewe.

“Atakachokifanya Aisha ni kuomba radhi kwa mashabiki wake na katika kila sehemu ambayo tutafanya shoo atafanya hivyo kabla ya kuanza kutumbuiza.”
.......ni mzimu wangu tu huu...siyo mimi..!

Pia, katika kuonesha ubinadamu, mwisho wa habari hiyo Mhariri aliwaomba Watanzania wasahau yaliyopita kuhusu Aisha na aombewe kwa Mungu ili amwepushe na mitihani mingine nkatika maisha yake.

Katika hali ya kushangaza sana, baada ya kimya cha muda mrefu, Aisha ameibuka katika gazeti hilo akidai kwamba picha zile zilikuwa za kutengeneza hali iliyozua maswali miongoni mwa wasomaji wetu.

Habari hiyo, ambayo ilionekana Aisha alikuwa amelenga kuwafanya Watanzania waamini Ijumaa linaandika habari za ‘mezani’ alisema, yupo mwanaume mmoja aneyemsumbua kimapenzi kwa muda mrefu, ambaye ndiye aliyemfanyia unyambisi huo.
......mimi siyo Aisha niangalieni vizuri...!!!!!

“Huyo anayenichafua alikuwa ananitaka kimapenzi nikamkatalia na siwezi kumkubalia, hata kwa mtutu simpi mwili wangu ng’o, kuamua kunitangazia sifa chafu si suluhisho la mimi kumkubali, zaidi ya kumuona kichekesho kwani katika jamii ya watu wastaarabu hafai, namfananisha na ‘nungayembe’ la kiume,” alisema Aisha katika sehemu ya habari hiyo.

Aidha, aliongeza: “Picha za ngono zilizoenea kila kona ya nchi, zinazonihusu mimi si za kweli, amefanya hivyo kwasababu ‘nilimpiga za uso kavukavu bila chenga’, siwezi kupoteza muda wangu kubishana naye, nitakuwa nampandisha chati, lakini ajue hata kwa mtutu hapati kitu kwangu.”

Katika juhudi za kulishusha ‘grade’ gazeti hili, sehemu ya habari hiyo ilisomeka, ‘Anadai amekuwa akikabiliwa na tuhuma za kupiga picha za ngono na utupu zilizosambazwa sehemu mbalimbali hasa katika magazeti ya udaku, ambapo kiuhalisia si zake.
....baada ya mitungi, mikasi....Aisha akiwa na Khumalo
Katika hatua nyingine, mapema wiki hii, kijana Khumalo aliyefanya naye uchafu huo nchini Afrika Kusini, amelitumia waraka pepe (e-mail) gazeti hili akiomba msahama kwa Aisha.

Alisema anakiri kumtenda vibaya (kupiga na kulikisha picha hizo) mnenguaji huyo, lakini anamuomba amsamehe na waanze ukurasa mpya.
..email ya Khumalo kwa gazeti hili akimuomba radhi Aisha...(click to enlarge)

Aidha, katika waraka pepe huo ulioandikwa kwa Kimombo, Khumalo aliomba radhi kwa Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka huku akitangaza nia yake ya kutaka kumuoa Aisha.

Kitendo cha Aisha kwenda kukanusha habari hiyo kwenye gazeti lingine, tunaamini kinalenga kutushusha na kupunguza imani ya wasomaji dhidi yetu.

Siku zote tumekuwa tukisimama katika ukweli, hatukurupuki kuandika habari za kutunga wala zisizo na ushahidi wa kutosha.
Kukubali kwake kupiga picha zile na kuomba radhi kunathibitisha moja kwa moja kwamba ni kweli picha ni zake, lakini kukataa baadaye katika chombo kingine ni kutufanya Global waouonekane waongo.

Zipo picha nyingi zaidi za utupu ambazo tumetunza kwenye maktaba yetu, hatukuzitumia kwasababu za kimaadili hasa kutokana na ukweli kwamba ni chafu zaidi ya tulizochapisha.

Kwa yeyote ambaye ameanza kuingiwa na imani kwamba picha zile ni za kutengeneza, tunamkarisha katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam, ajionee mwenyewe.Na kwa mliombali na Dar, tumelazimika kuweka kwenye mtandao huu baadhi ya picha hizo ambazo hatukuwahi kuziweka pamoja na kipande cha video alichochukuliwa siku ya tukio.

KWAKO AISHA
Kukiri kwako mbele ya bosi na mashabiki wako, kulitafsiri kukubali kupiga picha zile zilizo kinyume na maadili ya Kitanzania na ulikuwa ukihitaji kusamehewa, hivyo kukanusha, kunashusha uelewa wako, kwani unaonekana mtu wa kutapatapa.

Fahamu kwamba, habari hiyo imetukera na tunakutaka ujaribu kuwa muungwana na uelewe kwamba kuna Mungu ambaye bila shaka anajua ukweli zaidi pengine ya tuliouripoti.


Kama ni kweli uliona umeonewa, chondechonde toa uthibitisho tukupe hayo mamilioni ya shilingi ili uuage umaskini na kuachana na unenguaji. 

VIDEO YAKE JE?

WEWE MSOMAJI, NI KWELI PICHA HIZI NI ZA KUTENGENEZA? AISHA ANASINGIZIWA? NANI WA KULAUMIWA KATIKA SAKATA HILI?

Comedy ZONE

Jamaa moja maisha yali kuwa magumu sana hata ela yakula alikuwa hana akaamua kwenda kujinyonga ile kafunga kamba islael ana mtokea aka muambia "oya nafasi zimejaa huko mbinguni subiri kukiwa nanafasi takuambia" ghafla akapotea .jamaa aka chukua kamba yake akawa ana rudi nyumban kufika nyumban akaendele kulala njaa baada ya mwez akaokota mahela meng sana akawa aana panga jinsi ya kuzitumia (nijenge nyumba ninunue gari nisomeshe watoto) ghafla islaeli katokea " oya nimekuijia sasa hivi watu hamna huko mbingun "jamaa akafa na mahela aka yaacha duh!!!

BAIKOKO YAPAGAWISHA MASHABIKI, SINZA, DAR...

Kinadada wakikatika, mmoja akiwa amekalia chupa.

Mashabiki wakifanya kufuru kukonga nyoyo zao.

KUNDI la ngoma ya Baikoko lenye asili yake mkoani Tanga, usiku wa kuamkia leo limewachizisha mashabiki ndani ya Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya mashabiki walibanjuka na kuwa kivutio kwa watazamaji.

Mwanadada akiwa amelala kwa hisia baada kunogewa na mirindimo ya Baikoko.

 Mfanyabiashara wa Soko la Makumbusho jijini Dar, Pius Ruta (Mzee wa Pamba), akicheza Baikoko na ‘kifaa’ chake.

Wapiga ngoma na manyanga wakiwachizisha mashabiki.

Comedy ZONE

Sharobaro m1 ali2miwa sms na galfrnd wake, kutokana kwa wingi na urefu wa sms ilidisplay *some text missing*!!!

Sharobaro c akazani ni neno la kimahaba afu ukizingatia english shallow akajitutumua nae ajione yupo kwenye uwanja wa mapenzi akareply...
*some text missing too dear*.

MANCHESTER CITY 6, MANCHESTER UNITED 1

Manchester City's Italian Striker Mario Balotelli (3rd L) Celebrates Scoring His Second Goal With Team-mates
Mshambuliaji wa timu ya Manchester City, Mario Balotelli (wa tatu kushoto) akishangilia na wenzake baada ya kufunga goli la pili katika mechi ya Ligi Kuu ya England kati ya Manchester United na Manchester City kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester leo.

Timu ya Man U leo imevuna aibu baada ya kuchapwa mabao 6-1 na timu ya Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu ya England  kwenye Uwanja wake wa Old Trafford, Manchester leo.

Saturday, October 22, 2011

WEMA, DIAMOND WAMWAGANA: FULL DATA



NGOMA ikilia sana ujue inakaribia kupasuka na lisemwalo lipo kama halipo, basi li njiani laja! Hatimaye Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, wamemwagana rasmi, The Udaku Master ‘eituzedi’ ya mkasa mzima.

Ilikuwa ni Jumanne, saa mbili usiku, Diamond ‘Platinum’ aliita vyombo vya habari katika Hoteli ya Lion Sinza jijini Dar es Salaam na kufunguka:


“Washikaji, nimewaita hapa nifunguke mbele yenu kuwa nimemmwaga rasmi yule demu (Wema) kwa sababu hapatani na mama yangu (Sandra Sammy).

ALINILAZIMISHA NITENGANE  NA MAMA
“Kwanza Wema amekuwa akinilazimisha nitengane na mama yangu, yaani nimrudishe kule Tandale tulipokuwa tukiishi mwanzo , halafu mimi na yeye tuishi Sinza (Madukani), jambo ambalo sipo tayari kulifanya.


“Mimi na mama tumetoka mbali, hakuna kama yeye, alikuwa akishinda njaa ili mimi nisome, alinilea kwa shida sana, hata siwezi kuelezea kwani nikikumbuka huwa natokwa machozi, kwa hiyo siwezi kumtelekeza kwa sababu ya Wema.
“Hata katika muziki, nakumbuka nilishamuibia pete yake ya dhahabu nikaenda kuiuza ili nirekodi muziki na alinivumilia.

NI WAKATI WA MAMA ‘KUINJOI’
“Piga ua, huu ni wakati wa mama yangu kula na ‘kuinjoi’ matunda ya mwanaye, mapenzi hayawezi kusababisha nimtende vibaya. Natamka rasmi huyu demu nimemmwaga bwana.”

SWALI LA MWANDISHI WA IJUMAA
“Mlianza mapenzi muda mrefu na ni wiki mbili tu zimepita tangu ulipomvisha pete ya uchumba, je, hukujua kwamba mambo kama haya yangetokea?


DIAMOND AKAJIBU
“Sikuligundua hilo mapema na pia si unajua mambo ya ujana tena? Ukweli ni kwamba tukio hili limenikumbusha kuwa ujana ni jalala linalotupwa kila aina ya takataka.”

UPANDE WA WEMA
Baada ya Diamond kumwaga unga na ishu hiyo kuwa gumzo jijini Dar usiku kucha, kama ilivyo desturi ya gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa nchini, asubuhi na mapema (Jumatano), mapaparazi wake wa kuheshimika walimsaka Wema ili kupata mzani wa habari hiyo.


NDANI YA HOTELI YA LAMADA
Kutokana na uzito wa habari yenyewe, Ijumaa lilisaga lami hadi Hoteli ya Lamada Ilala, chumba namba 35 flati ya Mikumi ambapo Wema alikuwa kambini kwa ajili ya kurekodi filamu.

HALI ILIKUWA HIVI
Baada ya kubisha hodi, ‘mkaribisha wageni’ alikuwa  Elizabeth Michael ‘Lulu’, alifungua mlango ambapo Wema alishuhudiwa akinyanyuka na kwenda kuosha uso, aliporejea na kuwaona ‘polisi’ wa Ijumaa wakifunga ‘makamera’ yao alipaza sauti na kufuatiwa na kilio: “Maweee! Nimeachwa? Nyiii….nyiiiii.”


Lulu: Nyamaza Wema usikie kilichowaleta.
Ze UTAMU: Mambo vipi Wema?

Wema: Hata salamu yenu sitaki, niambieni nimeachwa?
Ze UTAMU: Poa, ili mgonjwa apone lazima achomwe sindano inayouma au ameze vidonge vichungu. Iko hivi Wema; jana pale Lion Hotel, Sinza,  Diamond alitangaza rasmi kukutema kwa sababu eti umekuwa ukimlazimisha kumtenga mama yake ili muishi peke yenu, yeye hayupo tayari kufanya hivyo, je, hili unalizungumziaje?


Wema: (kilio) siko tayari kuzungumza chochote.
Ze UTAMU: Tafadhali waambie mashabiki wako umeipokeaji taarifa hii?

Wema: Amenidhalilisha, nitaweka wapi uso wangu? Anyway, niacheni nitawatafuta baadaye niongee.
Lulu: Dada Wema, funguka tu kile unachokijua, itakusaidia watu wajue ukweli.
Wema: No, please. Waondoke tu nitawatafuta baadaye.


UTABIRI
Ili kuthibitisha kuwa kile kinachoandikwa na Magazeti  uhakika asilimia zote, wakati hayo yanatokea, tayari gazeti tumbo moja na hili, Risasi Mchanganyiko toleo namba 844 la Jumatano wiki hii lililokuwa na kichwa cha habari: WEMA, DIAMOND HAKUNA NDOA, lilitabiri na kuweka vigezo kuwa Wema na Diamond hawatadumu.

Aidha, Gazeti la Risasi Jumamosi iliyopita, ukurasa wa 16 kulikuwa na habari yenye kichwa; ETI WEMA, MAMA MKWE WAKE HAWAIVI.
Diamond alionesha kutokubaliana na madai hayo, lakini yaliyotokea yameweka wazi.


WADAU WANASEMAJE?
Kwa mujibu wa wadau walioinyaka habari hiyo walilieleza kuwa haijawahi kutokea Wema akamwagwa na midume kwani yeye ndiye huwa anawamwaga.
“Ama kweli mtenda akitendewa…safari hii kaachwa yeye!” alisema mmoja wa wadau hao.


ANATAMANI DUNIA IRUDI NYUMA
Uchunguzi  ulibaini kuwa usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii, Wema hakupata usingizi kwa kuwa alishanusa dalili za tukio hilo.

“Ukweli Wema hakulala kabisa, alikuwa akijigeuza mara kwa mara na kutaja jina la Diamond huku akilia, alipoulizwa kulikoni alijibu: “Natamani dunia irudi nyuma ili lile tukio la kuvishwa pete ya uchumba pale New Maisha Club wiki mbili zilizopita lifutike,” alisema mmoja wa wasanii aliyekuwa naye kambini hapo.

GADDAFI: MWANZO MWISHO...


Mwili wa Kanali Muammar Gaddafi baada ya kuuawa na wapiganaji jana.
                       Kanali Muammar Gaddafi enzi za uhai wake.


ALIYEKUWA kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi ameripotiwa kuuawa na wapiganaji wanaoongozwa na Baraza la Mpito nchini humo (NTC), baada ya mji wa nyumbani kwake, Sirte kunyakuliwa na vikosi hivyo jana.

Kifo cha Kanali Gaddafi (69) kilitangazwa rasmi na Waziri Mkuu wa Serikali ya mpito nchini humo, Mahmoud Jibril, muda mfupi baada kiongozi huyo aliyeitawala Libya kwa miaka 42 kuuawa.

Awali, msemaji wa NTC nchini Libya, Kanali Ahmed Bani alisema Kanali Gaddafi aliuawa na mwili wake ulipelekwa katika mji wa Misratah, bila kutoa ufafanuzi kamili kuhusu mazingira ya kifo hicho.

Taarifa za kuuawa kwake zilitolewa huku zikiambatanishwa na picha zinazoonyesha sura inayoonekana kuwa ni ya kiongozi huyo, katika muonekano wa nywele zake laini na ndefu wastani na uso uliotapakaa damu na majeraha.

Kanali Gaddafi anakuwa kiongozi wa kwanza kuuawa tangu kuanza vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya kiarabu mwanzoni mwa mwaka huu, yaliyowaondoa madarakani Rais Ben Ali wa Tunisia na Hosni Mubarak wa Misri.

Kifo hicho kimetangazwa ikiwa ni miezi tisa tangu kuanza kwa upinzani mkali dhidi ya Serikali yake Februari mwaka huu, ambapo aliapa kwamba asingeondoka nchini Libya na kwamba yeye na wafuasi wake wangepambana hadi tone la mwisho la damu.

Kanali Gaddafi ambaye wakati wa utawala wake aliwahi kujipa wadhifa wa “mfalme wa wafalme wa Afrika” alikuwa akisifika kwa ukali wa sauti yake na maneno makali ya kuhamasisha na kueleza misimamo yake katika hotuba zake.

Mapambano hayo yameishia katika mji wa nyumbani kwake, Sirte ambao umekuwa na upinzani mkali kwa vikosi vya wapiganaji wa NTC ambavyo vililazimika kupambana kwa miezi kadhaa hadi waasi walipofanikiwa kuuteka jana.

Kanali Bani alisema mtoto wa Kanali Gaddafi, Mutassim ambaye walikuwa pamoja katika mji wa Sirte aliuawa na wapiganaji hao wa NTC.

Msemaji huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa kiongozi huyo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya katika miguu yake yote na kichwani.

“Aliuawa katika mapambano na wapiganaji wetu. Kuna picha zinazoonyesha hayo,”alisema.

Alijificha kwenye karavati

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, Kanali Gaddafi alidhibitiwa baada ya kukutwa  amejificha katika karavati la barabarani, yeye pamoja na baadhi ya walinzi wake.

Kwa upande wake, kamanda wa wapiganaji wa baraza hilo, Abdul Hakim Belhaj pia alithibitisha kuwa Kanali Gaddafi alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kukamatwa.

Makamu Mwenyekiti wa NTC, Abdul Hafiz Ghoga alithibitisha mbele ya waandishi wa habari kuwa Gaddafi aliuawa katika mji wa Sirte.

“Tunatangaza kwa dunia kuwa Muammar Gaddafi aliuawa katika mikono ya wanamapinduzi,” alisema Ghoga.

Katika mtiririko wa matukio yaliyokuwa yakirushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni, kituo cha televisheni cha al-Jazeera kilionyesha picha za mwili wa Kanali Gaddafi ukiburuzwa katika eneo alilouawa.

Filamu za video zilizochukuliwa kwa simu za mkono zilionyesha kile kilichoonekana kuwa maiti ya Gaddafi iliyolowa damu. Mwili wake baadaye uliburuzwa na wapiganaji na kupakiwa nyuma ya gari aina ya pick-up.

Nato na Marekani zilieleza kuwa haziwezi kuthibitisha taarifa za kuuwawa kwa kiongozi huyo ambaye hajaonekana tangu NTC ilipoikamata Tripoli.

Watu washangilia mitaani

Wakati huohuo, katika mji wa  Benghazi na miji mingine nchini humo, watu walionekana kukusanyika mitaani na kushangilia taarifa hizo za kuuawa kwa Gaddafi.

Viongozi mbalimbali duniani pia wamezungumzia kuhusu taarifa hizo za kuuawa kwa Kanali Gaddafi ambaye amewahi kuwa mpinzani mkubwa wa mataifa ya Ulaya na Marekani kutokana na misimamo yake dhidi ya mataifa hayo.

Miongoni mwa viongozi hao ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon ambaye alisema ni siku maalum ya kukumbuka maovu yote yaliyofanywa na Gaddafi.

Alisema watu wa Libya wako katika nafasi nzuri ya kujenga nchi imara na yenye demokrasia.

“Ninafurahi kazi ambayo Uingereza imesaidia katika kuuondoa utawala wa Gaddafi,”alisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Alain Juppe amepongeza kufikiwa mwisho kwa utawala wa miaka 42 ya Gaddafi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon pia alisema kwamba kifo cha Kanali Gaddafi kinatoa mwanya wa “historia mpya kwa Libya”.

“Watu wanatakiwa watambue kuwa huu ni mwisho wa mwanzo. Sasa ni wakati wa Walibya wote kushikamana na kuwa kitu kimoja. Ni wakati wa kuponya majeraha na kujenga upya taifa. Si wakati wa visasi,” alisema Ki-Moon.

Balozi wa Libya nchini Uingereza, Mahmud Nacua alisema kuwa kuawa kwa Gaddafi kunamaanisha Libya inaelekea kwenye mustakhabali bora wa baadaye.

Wasifu wa Kanali Muammar Gaddafi

Alikuwa mtoto wa wafugaji wa Kibedui, mwenye maisha ya utata, lakini ambaye alitukuzwa sana, huku mataifa ya Magharibi yakimuona mtu wa hatari wakati wote.

Muammar Muhammad Gaddafi aliitawala Libya kwa zaidi ya miaka 40. Hadi mwanzoni mwa Machi 2011, alikuwa akiamini ndani ya moyo wake kwamba watu wake walikuwa wakimpenda na kwamba walikuwa tayari kumlinda hadi kufa kwa ajili yake.

Lakini wakati huo, tayari Gaddafi alikuwa ameshatumia njia za kikatili kuyazima maandamano dhidi yake, maandamano ambayo baadaye yaligeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa, watu zaidi ya 30,000 waliuawa kwenye vita hivyo. Mara nyingi sana, Gaddafi alitoa matamko makali wakati wa vita hivyo, ila linalojuilikana zaidi ni lile la kuwaita wapinzani wake kuwa ni panya.

Kwa kila hali, yaliyotokea ni mambo ambayo Gaddafi hakuyatarajia asilani. Mtoto huyu wa wafugaji wa Kibedui aliyezaliwa mwaka 1942, alikuja kuibuka kama mkombozi wa Walibya, alipompindua Mfalme Idriss hapo mwaka 1969.

Kuanzia hapo akaanza kujenga kile alichokiona mwenyewe kuwa ni mfumo wa kidemokrasia wa moja kwa moja. Alianzisha kamati za umma zilizoamua juu ya mustakabali wa umma na wa Serikali. Aliuita mfumo wake wa kisiasa na kiuchumi kuwa ni wa kisoshalisti, alioufafanua kwenye kijitabu chake cha Kijani.

Historia yake kiufupi

Alizaliwa mwaka 1942 katika eneo la Jangwa, kwenye mji wa Sirte, katika familia ya baba Mohamed Abdulsalama Abuminiar na mama Aisha Ben Niran. Alijiunga na Jeshi la Libya  mwaka 1965.
Alifanya mapinduzi ya Serikali yasiyo ya umwagaji damu na kumuondoa mfalme Idris katika utawala wake mwaka 1969 na kuwa mtawala wa Libya akiwa na umri wa miaka 27.

Alikuwa maarufu kwa nguo anazopenda kuvaa na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.

Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am. Umoja wa Mataifa (UN) ulikubali kuondoa vikwazo dhidi ya Libya.

Baada ya miezi kadhaa, Serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za Magharibi.

Gaddafi ni mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake, kwa mujibu wa Saas Djebbar, mtaalam wa siasa za Libya.
Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.

Alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi alipokuwa mafunzoni Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya. Alipanga mapinduzi ya Septemba 1, 1969 akiwa katika mji wa Benghazi.

Alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa uliojumuisha kanuni za Kiislamu na mfumo ulio tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.

Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.

Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, alikuwa akitumia makazi maalum kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.Hema hiyo pia ilitumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.

Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.

Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za Bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.Aliwahi kuvunja na kufuta Wizara za nchi hiyo pamoja na bajeti zao, isipokuwa Wizara chache ikiwemo ya Ulinzi, Fedha na Mambo ya Nje.Licha ya uchumi wa Libya kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje, mabadiliko bado yanakwenda taratibu.

Vuguvugu la mageuzi dhidi yake lilipoanza mwanzoni mwa mwaka huu, aliapa kuwafuata wanaompinga nyumba hadi nyumba, mlango kwa mlango, hatua iliyoibua hasira na kuchochea harakati za kijeshi dhidi yake.

Baada ya baadhi ya askari kutangaza kujitoa katika jeshi lake na kuanzisha uasi, aliapa kwamba atapambana hadi tone la mwisho la damu litakapomwagika. Alisisitiza kwamba kamwe hatakimbia kutoka katika ardhi ya Libya, atafia katika ardhi ya mababu zake.

Taarifa zilieleza jana kwamba aliuawa baada ya kukutwa akiwa amejificha katika daraja dogo kwa ajili ya kupitisha maji barabarani (karavati).

Mara baada ya kuuawa, wapiganaji wa Baraza la Mpito waliokuwa katika mapambano dhidi yake walibaini kwamba alikuwa na bastola iliyotengenezwa kwa dhahabu tupu.

WEMA DIAMOND SASA BASI; WEMA AVUA PETE RASMI....




Aliyekuwa mchumba wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, mlimbwende Wema Isaac Sepetu ameivua rasmi pete ya uchumba kufuatia kupigwa chini na msanii huyo...

Ishu hiyo ya kusikitisha, ilijiri Jumatano ya Oktoba 19 mwaka huu, saa chache baada ya kujiridhisha na taarifa za kuachwa kwake.

Wema aliivua pete hiyo ya dhahabu na kuibwaga sakafuni akiwa ndani ya chumba nambari 35, Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam ambako amepiga kambi na wenzake kwa ajili ya kurekodi filamu.

Aidha, baada ya tukio hilo, msanii nyota wa muvi za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliiokota na kuivaa kwenye kidole husika huku akisema ‘anaosha nyota’.

“Hee, ngoja niivae miye nioshee nyota, jamani! Mh,” alisikika akisema Lulu licha ya kwamba wakati huo, Wema alikuwa akibubujikwa machozi.

Mpaka mapaparazi wetu wanaondoka eneo la tukio, Wema alikuwa bado akilia huku akisema anajuta kuvishwa pete na Diamond ambaye amemuacha njia panda.

Alisema katika maisha yake hajawahi kuachwa, Diamond amemfanyia tukio la ajabu sana na haamini masikio yake achilia mbali macho.

Jumapili ya Oktoba 2 mwaka huu, ndani ya Maisha Club, jijini Dar es Salaam, Diamond alimvisha Wema pete ya uchumba tukio ambalo lilishuhudiwa na mashabiki wao kibao.

Oktoba 18 mwaka huu, ndani ya Hoteli ya Lion, Sinza jijini Dar es Salaam, Diamond aliwaambia waandishi wa habari kwamba, ameamua kummwaga Wema kufuatia jaribio lake la kutaka kumtenganisha na mama yake mzazi.

Kwa maana hiyo basi, Wema amedumu na pete katika kipindi cha siku 16 tu....

Comedy ZONE

Jamaa mmoja alikuw na uume mkubw mno yapata inchi 25 hv...so alikuw anapt shda sana akaamua kwnd kwa mganga japo aupunguze had inch 10..mganga akamwambia inabd amtongoze mtt wa padri n kila mtoto wa padri akisema NO..thn uume utapungua inch 5...jamaa akatoka akamfuata stella(mtt wa padri)..stella akasema NO..kurud hm akakuta uume wake umebak inch 20..kesho yake akamrudia tena,stella akasema NO..kurud hm akakuta uume umebaki inch 15..akaona bdo mara mja ili abak na inch 10..kesho yake akamfuata tena stella..,stella akajb kw hasira unatak nirudie mara ngap nimekwambia NO..NO..NO..NO..,Kurud hom akajikuta ana shmo la inch tano..

NANI CHANGU??! MASTAA WA KIKE BONGO...



Mastaa wa kike Bongo wanaojiita wasichana wa mjini wamebandikwa lebo ya micharuko huku wakitumia vibaya mwavuli wa sanaa kufanyia uchangudoa au umalaya.


Ili kujua nani mwenye sifa ya uchangudoa na nani msafi, ZE UTAMU limefanya uchunguzi wa kina na hapa linaibuka na ripoti kamili ya staa mmoja mmoja bila kutoa hukumu hivyo kazi ni kwako.

AUNT EZEKIEL
Ilibainika kuwa ni staa mwenye nyota tano, lakini aliwahi kunaswa usiku mbaya kwenye ukanda wa machangudoa a.k.a Wauza Sukari. Alishapitia mikononi mwa wanaume kadhaa wakiwemo Jack Pemba, Hartmann Mbilinyi na Mwilu Mwilola ‘Silver’ huku kukiwa na madai kuwa kwa sasa anapeana ‘kampani’ na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Dev.

JACQUELINE WOLPER
Ilielezwa kuwa ni miongoni mwa mastaa wanaojiheshimu, lakini dosari kidogo ni ile ya kudaiwa kutoka na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ kabla ya hivi karibuni kuonekana ‘klozi’ na jamaa anayetajwa kwa jina moja la John.

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’
Kwa heshima aliyo nayo, hata waigizaji  wenzake humuita dada Johari. Dosari pekee iliyotajwa na watu walihojiwa na katika uchunguzi huo ni uhusiano tata alionao na mkurugenzi mwenzake wa RJ Productions, Vincent Kigosi ‘Ray’.

BABY MADAHA
Kinachomponza ni kauli na vituko vyake vya kimcharuko huku akitangaza kuwa yuko tayari kutoa penzi kwa mwanaume atayefika dau la Sh. milioni 5. Hilo lilitafsiriwa kuwa ni kujiuza ukiachilia mbali wanaume aliowahi kutajwa ‘kupeana nao kampani’, Dokta Pakir, Mwisho Mwampamba na sasa anadai yupo penzini na mtoto wa kigogo.

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Huku akijiita mcharuko namba moja Bongo, alielezewa kuwa pamoja na umri mdogo wa miaka 18, kitendo cha kutangaza kutoka kimapenzi na wanaume wawili, ndicho kinachomponza na hasa lile tukio la kuchanwa viwembe kisa mume wa mtu.

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Aliwahi kukiri kugawa uroda kwa wanaume wawili tu, jambo lililopingwa na watu wanadai kumfahamu zaidi. Pia kitendo cha kujilegeza kwa wasanii wa Bongo Flava, Ally Timbulo na Elias Barnabas, nacho kilitajwa kumjengea taswira tofauti mbele ya jamii.

RUTH SUKA ‘MAINDA’
Ukiacha historia yake ya huko nyuma, alielezewa kuwa ni msichana anayejiheshimu kwa kuwa hakuwahi kutajwa na msururu mrefu zaidi ya Ray na Hamis Dakota. Pia kitendo cha kuvishwa pete ya uchumba hivi karibuni ni mwanzo wa kujiongezea heshima.

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Uchunguzi uliweka wazi kuwa amekuwa akitamba kutoka na wanaume zaidi ya nane na kuendelea wakiwemo mastaa kama Mr Chuz (aliyezaa naye mtoto mmoja) na Mr Nice. Hana ‘imeji’ nzuri mbele ya jamii.

REHEMA FABIAN 
Kitendo cha kuwalegezea wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Raheem Nanji ‘Bob Junior’ huku kwa sasa akimpamba mpenzi wake Jacob, ndicho kinachosababisha aonekane ndivyo sivyo.

WEMA SEPETU
Anaelezewa kuwa ni msichana asiyetulia na mwanaume kuanzia kwa Steven Kanumba, Jumbe Yusuf, Chalz Baba, Diamond na sasa akiwa anaelea, vimemfanya kuchorwa tofauti katika jamii.

JACQUELINE PATRICK
Pamoja na kuwa na ‘body’ lenye mvuto, anaheshimika kwa kitendo cha kumudu vishawishi vya wanaume, aliwahi kukiri kutoka na wawili tu, mmoja ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Koani, Mafia, Haroub Masoud, Ifraj Haroub na huyu aliye naye kwa sasa ambaye watafunga ndoa ‘soon’.

JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Ni miongoni mwa mastaa wanaodaiwa kuwa micharuko hasa kwa kauli zake zisizochujwa kama kukiri kutoka na wanaume sita ndani ya mwezi mmoja. Aliwahi kutajwa na wanaume kadhaa akiwemo Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’. Ukweli imeji yake si nzuri kwa jamii hivyo alishauriwa kubadilika.

SALMA JABU ‘NISHA’
Ni msichana mwenye heshima, lakini alitiwa doa na ile skendo ya kukiri kubobea katika vitendo vya kisagaji.

ROSE NDAUKA
Anaelezwa kuwa miongoni mwa mastaa wenye heshima, lakini kitendo cha kuvishwa pete na mume wa mtu na ile skendo ya usagaji, anatakiwa avitazame upya.

JOKATE MWEGELO
Ana ‘sivii’ kubwa na heshima tele kwa jamii. Anaelezewa kuwa ni mwanamke anayefaa kuolewa. 

Doa pekee lililojitokeza ni ile skendo ya kupeana kampani na Hasheem Thabeet.

AGNESS GERALD ‘MASOGANGE’
Kwa umbo lake tata, anapewa ‘big up’ kwa kuwa hajawahi kutajwa kutoka kimapenzi na mwanaume yeyote.

LISA JENSEN
Alielezewa kuwa ukiachilia mbali kudaiwa kuwa ‘klozi’ na Steven Kanumba, ameendelea kujijengea heshima kubwa mbele ya jamii lakini akaomba kufunga pingu za maisha.

LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Jamii inamuona mcharuko namba moja kutokana na matukio yake pamoja na mikao ya kihasara inadaiwa ni ya kuwatega wanaume. Mchumba’ke ambaye amekuwa akitangaza kuwa watafunga ndoa ‘soon’ amepewa taadhari ya kumrekebisha. 

Comedy ZONE

Watu wakiwa wamejazana kwenyejazana daladala la kutoka mbagala kwenda kariakoo kwenye siti ya nyuma walikuwa wamekaa msela na sister du....

Msela akawa anatupia mistari kwa sister du kwa sauti ya kunong'oneza(kumtongoza), yule du akawa anamtolea nje.... Mbaya zaidi alikuwa anapayuka kwa sauti kubwa mpaka abiria wakaageuka kuwatazama...

Msela akamwambia tena sister du.... "Mbona mi naongea kwa sauti ndogo wewe unapayuka??!" Sister du ndio kwaaaaaaaanza akawa kachochewa.... "Bwana eee si useme unachotaka usinisumbue..." Tena kwa sauti kubwa zaidi ya mara ya kwanza..

Msela alipoona sasa abiria wamemtolea macho akaamua kumwaga mboga na yeye... "Wee msichana vipi??! Umejamba alafu nakueleza unajifanya mkali... Hutaki tukuambie kama umejamba....??! Dada sio ishu, nasema UMEJAMBA!!!"

Tuesday, October 18, 2011

Steve Jobs: Shujaa wa dunia aliyeendeleza mfumo wa kompyuta...



•    Amefariki  wiki iliyopita
•    Alikuwa madhehebu ya Buddha
•    Baba yake alikuwa Mwislam kutoka Syria
OKTOBA 5, wiki iliyopita ulimwengu ulipoteza mmoja wa watu muhimu katika maendeleo yake.  Ni mtu aliyechangia kiasi kikubwa kuendeleza kompyuta, moja ya vyombo vya “maajabu”   katika maendeleo duniani tangu maofisi ya New York, (Marekani,  hadi vijiji vya wilayani Igunga, Tanzania.

Ni Steve Jobs, Mmarekani aliyefariki akiwa na umri wa miaka 56.  Mtu huyo alikuwa mvumbuzi na mfanyabiashara na mmoja wa wenyeviti waasisi na ofisa mtendaji mkuu wa kampuni la kompyuta la Apple Inc.

Jobs aliyezaliwa Februari 24, 1955, na ambaye hakufanikiwa kupata elimu ya chuo kikuu,  alianza kuonyesha kipaji tangu miaka ya 1970 hadi kuanzisha kompyuta maarufu duniani zinazojulikana kwa jina la Apple na Macintosh.

Alifanya hivyo kwa kushirikiana na Steve Wozniak na Mike Markkul ambapo muda mwingi wa utaalam wake alipitia makampuni ya Pixar na The Walt Disney.

Jobs alikuwa mfuasi wa madhehebu ya dini ya Buddha na alipokuwa mdogo aliasiliwa na  familia ya Clara na Paul Jobs  na kupata jina hilo la ukoo la Jobs na kuwa Steve Jobs.

Baba yake mzazi alikuwa ni Abdulfattah John Jandali, Mwislam mwenye asili ya Syria aliyehamia Marekani akiwa na umri wa miaka 18.  Mama yake alikuwa ni Joanne Simpson, Mmarekani, ambaye Steve Jobs alikuja kumfahamu ukubwani na kuamua kuwa karibu naye.

Hata hivyo, alikataa kurudiana na baba yake mzazi ambaye sasa anaishi huko Reno, Nevada, Marekani.
Alikuja pia kumgundua dada yake aitwaye Mona Simpson, msomi na mtunzi wa vitabu.  Jina lake la kuzaliwa alikuwa ni Mona Jandali.

Mwaka 1991 alimuoa Laurene Powell kwa taratibu za dini ya Buddha ambapo akamzalia watoto watatu.  
Umaskini ulimfanya ashindwe kuendelea  chuo Kikuu huko Reeds ambapo anasema: “Mambo yalikuwa mabaya.  Sikuwa na bweni la kulala, hivyo nililala sakafuni katika chumba cha rafiki yangu.  

Nilikuwa nikikusanya na kuuza chupa tupu za Coca Cola kwa ajili ya chakula.  Nikikosa hivyo nililazimika kutembea kiasi cha  kilomita nane kwenda kupata chakula kizuri kwenye hekalu la Hare Krishna mara moja kwa wiki.”

Kompyuta maarufu alizoongoza kuzibuni ni iPod, iPhone na iPad na kompyuta nyingine nyingi za michezo.
Shujaa huyo wa dunia, aliyekuwa hali nyama, akipendelea zaidi samaki, alifariki nyumbani kwake Palo Alto, California, Marekani saa tisa mchana kutokana na uvimbe kwenye kongosho uliosababishwa na kansa iliyogunduliwa miaka saba iliyopita.

Ameacha utajiri wa dola bilioni saba kwenye kampuni ya Apple Inc na watoto Reed, Erin na Eve kutoka kwa mkewe Laurene, na amemwacha binti Lisa Brennan-Jobs aliyezaa na Chris Ann Brennan hapo kabla.

Comedy ZONE


Binti wa kikatoliki alimpenda kijana wa kiislam so akaamua kuambia wazaz wake kua kuna mvulana kampenda bt ni muislamu,so wazaz wakaamua kufunga na kuomba ili yule mvulana abadli dini...
Baada ya week kupita binti yao alirudi nyumban huku akilia,wazazi wakamuuliza kulikoni akawajibu akawaambia,"maaombi yamezidi sana maana yule muislamu amekua padre..".

Juma Nature, Barnaba na Roma wafunika tamasha la miaka 50 ya uhuru la Airtel Mbeya...



Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Barnaba Boy, kutoka kundi la THT akitumbuiza mamia ya wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea lililoandaliwa na Kampuni ya simu ya Mkononi ya Airtel na kufanyika katika viwanja vya Luandanzove mjini Mbeya mwishoni mwa wiki, Airtel pia ilisherehekea uzinduzi rasmi wa minara 20 katika vijiji ishirini ili kutoa mawasiliano bora mkoani Mbeya. Pichani juu: Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Juma Nature,  akitumbuiza mamia ya wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea lililoandaliwa na Kampuni ya simu ya Mkononi ya Airtel na kufanyika katika viwanja vya Luandanzove mjini Mbeya mwishoni mwa wiki. Airtel pia ilisherehekea uzinduzi rasmi wa minara 20 katika vijiji ishirini ili kutoa mawasiliano bora mkoani Mbeya.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Roma, akitumbuiza mamia ya wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea lililoandaliwa na Kampuni ya simu ya Mkononi ya Airtel na kufanyika katika viwanja vya Luandanzove mjini Mbeya mwishoni mwa wiki, Airtel pia ilisherehekea uzinduzi rasmi wa minara 20 katika vijiji ishirini ili kutoa mawasiliano bora mkoani Mbeya.

Airtel yafanya tamasha ya miaka 50 kusherehekia uzinduzi wa huduma za wa Mawasiliano                  vijiji 20 Nyanda za Kusini
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imefanya tamasha la wazi mkoani Mbeya lililojumuisha wasanii mahiri  akiwemo Juma nature na kundi lake la  wanaume halisi ili  kusherehekia miaka 50 ya uhuru pamoja na uzinduzi wa huduma za mawasilino ya simu za mkononi katika vijiji 20 vya Nyanda za Kusini.

Vijiji vilivyofaidika na huduma za mawasiliano  ni Kaulolo, Nsenkwa,Mtakuja,Inyonga na Kamsisi mkoani Rukwa kwa Mkoa wa mbeya ni vijiji vya OldVwawa,Isangu,Ilolo,Ilembo,Mwantengo,Hasamba,Ukingani  Majengo, Mpangala,Kinyika,Ndapo,Nhungu,Matamba na Mahanji  wakati Mkoani Iringa ni Kibena, Tea estate.

Tamasha hilo la aina yake lililowavutia maelfu ya wakazi wa Mbeya  lilifanyika katika viwanja vya Rwandanzove ambapo msanii wa kwanza kupanda jukwaani na kuburudisha alikuwa ni  mkali wa Zuku na R&B Barnaba boy ambaye aliburudisha sana watu na vibao vyake vikali lakini ilikuwa shangwe pale alipoachia bembeleza na natumaini

Mara baada ya burudani hiyo alipanda mchekeshaji maarufu King Majuto na kutoa burudani ambayo ilienda sambamba na wananchi kusajili namba zao mara tu wanapohamia Airtel.

Burudani ya shangwe za uhuru wa kuongea kwa kuhamia airtel ilinoga baada ya jukwaa kuvamiwa na mkali wa miondoko ya bongo flava Juma Nature na wanaume halisi na kuachia vibao vinavyobamba katika burudani ikiwa ni kama” mtoto iddi”mega mixing ya yaleo kali, ah wapi, party la kijanja 770, hiligame, na hakuna kulala pia hayo Jumanature alipanga mashairi yanayoelezea  juu ya miaka 50 ya uhuru ambayo yalileta amasha na mwamko kwa wakazi wa mbeya.

Mwisho jukwaa lilimalizwa na mwanaharakati msanii wa hip pop Roma ambaye alimwaga mashairi yaliojaa vina vyakuwapa wananchi wa mbeya matumaini na pole kwa wale wanaopigwa nondo na watu wasiojulikana kwa mambo yanayosemekana ni yakishirikina yalioanza hivi karibuni huko mbeya

Poleni watu wambeya mnaopigwa nondo kwa imani za kishirikina ili watu wauze mabucha…. Yaliseme baadhi ya mashairi ya msanii huyo.

Pia aliwaomba wananchi wote waliojaa kiwanjani hapo kuinamisha kichwa chini kwa sekunde chache kama ishara ya kumuenzi baba wa taifa na kasha akaanza na kibao chake cha mr president, na kuendelea na pastor, Tanzania, mechi za ugenine na kumaliza na nyimbo iliyozua gumzo zaidi ya mathematics.

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alifunga burudani hizo kwa kusema “Airtel inaendelea kupanua mtandao na kuwapatia wateja wake huduma bora kwa kuwafikia wananchi wengi na kuboresha huduma hasa katika vijiji mbalimbali nchini.

“Mkakati wetu wa kupanua mawasiliano vijijini unaendelea kwa kipindi chote cha Mwaka huu lengo letu ni kuhakikisha tunawafikishia wananchi wote huduma ya mawasiliano yenye utulivu zaidi kutatoa uhuru wa mawasiliano zaidi  kwa wateja  kuendelea kufanya mawasiliano yenye manufaa yatakaowafanya wafurahie kutimiza miaka 50 ya uhuru wakiwa na miundombinu ya mwasiliano yanayojitosheleza.

Comedy ZONE

Mazoea ni mabaya sana.. cku 1 masai m1 aluienda chooni na kopo kwa nia ya kujisaidia haja kubwa kwa bahati mbaya aliweka maji kwenye kopo lililotoboka bila kujua, akiwa choon maji yote yakamwagika alimaindi sana ila akapotezea akasepa hivohivo..cku ya pili akachukua kopo tena bt this tym lilikua zima ila hakujua sasa ili kulikomoa akaona koja atawaze kwanza then ndo akajisaidia nakusepa huku akisema "leo nimekuwesa"

Abiria 30 wanusurika Kifo katika ajali mbaya...



Pichani ni gari hilo lililopinduka.

AJALI ya gari ambayo hufanya ruti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya mpaka mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini,  ambayo imetokea kwenye mteremko wa Mbalizi ambapo zaidi ya abiria thelathini wamenusurika kifo, baada ya gari kushindwa kupandisha mlima hali iliyopelekea kupinduka.

Tukio hili limetokea siku ya Jumapili. Baada ya kupinduka kwa gari hiyo ambayo hufanya ruti ya kusafirisha abiria kutoka Mwanjelwa jijini Mbeya hadi mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini hatimaye lilinusurika kutumbukia bonde la mtoni Mbalizi tukio lililotokea siku ya Jumapili.

Jeshi la polisi Usalama barabarani Mbeya linanapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini magari yenye kasoro kwa lengo la kuepukana na ajali zisizokuwa za lazima.

Monday, October 17, 2011

Comedy ZONE

BANGI................
Mvuta bangi m1, alipigiwa cmu na demu wake:
Demu=honey
Jamaa=vp?
Demu=upo wp
Jamaa=home
Demu=km umelala naomba uniote mpenzi wangu
Jamaa=cjalala
Demu=!!??, km unakula nirushie chakula chako
Jamaa=cli
Demu=!!!??bac nirushie maneno ya hubah HABIBY WANGU
Jamaa=nipo chooni, nikurishie mavi au mkojo????
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...