Monday, October 17, 2011

MY GOD! MISS AFUMWA AKISAGANA



MY God! Miss Ruvuma ‘hamnazo’ 2005 ambaye alishiriki kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huo na kuangukia pua, Isabella Mpanda ‘Bella’ amefumwa ‘laivu’ akifanya vitendo vya kisagaji na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Jack..

Bella asiyekuwa na tone la aibu alinaswa na kamera yetu akijihusisha na uchafu huo wa kufedhehesha ndani ya Ukumbi wa Mzalendo Pub Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilikuwa ikifanya makamuzi.

NI SINEMA YA BWERERE
Katika tukio hilo, wakati Wazee wa Kizigo wakikamua stejini, shuhuda wetu aliwapiga chabo warembo hao wakiwa wamejibanza kwenye mwanga hafifu nyuma ya ukumbi huku wakishikana sehemu nyeti kwa staili ya ‘baba na mama’.

Kwa mujibu wa mkanda wa picha unaoshikiliwa, Bella mwenye kupenda kuandikwa magazetini kwa matukio machafu, alionekana kucheza nafasi ya mwanamke huku Jack akichukua uhusika wa mwanaume katika sinema hiyo ya bwerere.

Katika tukio hilo lisilovumilika, nunge hizo mbili zilionekana zikishikana sehemu nyeti na baadaye ‘zilidendeka’ bila kujali watu waliokuwa wakiwatemea mate chini kwa kushindwa kuwavumilia.

BELLA ALEGEA KAMA MLENDA
“Ama kweli dunia imefika ukingoni, heri hata enzi za Firauni tunazozisoma kwenye vitabu. Huyu Bella amezidi, hafai kanisani wala msikitini. Angalia alivyolegea kwa mwanamke mwenzake utadhani mlenda wa bamia,” alisikika dada mmoja shabiki mkubwa wa Extra Bongo.

Baada ya ‘kuwafotoa’ picha za kutosha kwa ajili ya ushahidi wa uchafu wao, paparazi wetu aliwafuata ili kupata mzani wa tukio hilo ambapo mbali na kupigwa na butwaa kwa aibu wakijua kuwa ishu ‘imesanuka’, wawili hao waliokuwa wamekumbatiana waliachiana, wakawa wanategeana kuzungumza.

‘Polisi’ wetu alipoendelea kuwabana, Bella alifyatuka: “Hebu futika mbele yetu, nani amekutuma kutufuatilia kwenye ‘praiveti’ yetu? Ondoka kabla hatujakuitia mwizi.”

NENO LA RISASI MCHANGANYIKO
Hakuna haki za binadamu kwa watu wasiokuwa binadamu. Bella anapaswa kuwa kioo cha jamii kwani hivi karibuni alitamba kuzaa na mume wa mtu hivyo atamfundisha nini mwanaye ilihali yeye mwenyewe hana maadili? Anapaswa kujirekebisha haraka kwani kama hakufunzwa na mamaye, atafunzwa na ulimwengu.

Comedy ZONE

Ndani ya ndege kuna abiria tatu. Mrusi,Mjamaica, na M-bongo. Wamefika anga za juu pilot akawauliza wahisie wapo wapi!
Mrus akatoa mkono dirishani dah bonge la baridi akasema hii Moscow bila shaka.
Mjamaica akatoa pua nje(anayo ndefu) akaskia harufu ya marijhuana akasema hii Kingstone bila shaka.
M-bongo akatoa mkono dirishani fasta akaurudisha ndani wenzio wanamwuliza wapi? Akajibu hii ki2 Manzese hii. Wakahoji Kwa nini? Akajibu Wameshaniibia SAA mkononi ndan ya sekunde. Teh teh teh

BSS 2nd CHANCE: Alichotendwa Rodgers Lucas mmmh.....


                                                                Haji Ramadhan.

NO! No! No! Hapana! Haiwezekani! Hayo yalikuwa makelele yaliyosikika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita baada ya kutangazwa mshindi wa Shindano la Bongo Star Search ‘Second Chance’ 2011, Haji Ramadhan...

Kabla ya kutangazwa kwa Haji aliyekomba Sh. milioni 40, alianza kutangazwa mshindi wa tatu, Waziri Salum ambaye alilamba Sh. milioni 5 na wa pili, Rogers Lucas aliyeondoka na Sh. milioni 10 huku mrembo pekee aliyekuwa ameingia kwenye nne bora, Bella Kombo akiambulia cheti pekee.

Awali ilielezwa kuwa Rogers ndiye aliyekuwa akikimbiza kwa kupigiwa kura nyingi hivyo baadhi ya wadau waliamini angeibuka kidedea, lakini matokeo yakawa ndivyo sivyo.

“Alichotendewa Rogers siyo ‘freshi’ kabisa. Ndiye msanii mkali kuliko wote kwani ukiachilia mbali kutunga, ana sauti nzuri na anajua kutumia vyombo vya muziki kama gitaa,” alisema mdau mmoja wakati akitoa maoni yake juu ya ushindi wa Haji.

Aliongeza: “Majaji hawakuwa ‘fea’ kwa sababu walikuwa wakiwakatisha tamaa baadhi ya washiriki na kuwapongeza ambao hawaimbi bali wanapiga makelele tu na kukata viuno.

“Kwa jumla ni kazi nzuri, lakini majaji wanatakiwa kuboresha baadhi ya vitu hasa kwenye ukosoaji. Wanapaswa kumwambia mshiriki mahali alipokosea na siyo kuponda au kusifia tu.”

Mdau mwingine aliyezungumza alisema: “Haji? Aah! Wapo wanaomkubali lakini kwa upande wangu naamini hafui dafu kwa Rogers.”

MSHINDI ALIJULIKANA KABLA
Baada ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Bench Mark Production inayoratibu shindano hilo, Rita Paulsen ‘Madam’ kupanda jukwaani, aliwataka wadau kusema mshindi ni nani ambapo katika hali ya kuonesha kuwa mshindi alijulikana kabla, kundi la watu lilijibu kwa sauti kuwa ni Haji.
Hata hivyo, Madam hakuwa na haja ya kufungua bahasha ili kuona jina la mshindi hivyo akamtangaza jamaa huyo.

VIBWEKA VYA MASTAA BONGO
Kama ilivyo ada, mastaa wa Kibongo hawakuwa nyuma katika kuonesha vibweka vyao.

LULU KAMA KAWA, FULL MCHARUKO
Staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alizama ukumbini hapo akiwa na dada yake na kwenda moja kwa moja katika viti vya VIP.

Kama kawa, kama dawa, Lulu aliingia akiwa mpole asiye na maneno mengi, ingawa hali hiyo ilibadilika ghafla baada ya Haji kushuka  na kibao cha Dushelele cha Ali Kiba ambapo alinyanyuka na kuanza kukata mauno kimcharuko.

Badaye alichanganyikiwa kabisa alipopanda stejini msanii kutoka Nigeria, Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’ ambapo alinyanyuka na kwenda kuchizika mbele ya steji huku akipiga mayowe ya kufa mtu.

UWOYA ASHANGAZA WATU
Irene Uwoya alishangaza watu kutokana na muda mwingi aliokuwa ukumbini hapo kuonekana akiwa ametulia kwenye kiti chake huku akiwa amejiinamia, jambo ambalo wengi walihoji ni kipi kilichomsibu kwani siyo kawaida yake.

ANTI LULU AANIKA UTAMU WAKE
Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ ni mtangazaji ambaye katika siku za usoni amekuwa akifanya vituko vya hapa na pale ikiwa ni pamoja na kulewa ovyo.
Naye hakuwa nyuma kwani alivalia nguo iliyoanika sehemu kubwa ‘tamu’ ya mwili wake huku akipagawa na wasanii wote waliopanda jukwaani.

MBONI, JACK PATRICK SHUGHULI YAO
Kwa upande wao mastaa Mboni Masimba na Jacqueline Patrick walikuwa wakijiachia vilivyo utadhani shuguli ilikuwa yao.
Walishangilia na kuserebuka kwa raha zao na kali kuliko walikuwa wakishangilia kila tukio.

Full Mapicha ya BSS 2nd CHANCE...

Jumanne Iddy akitoa vitu vyake...

Peter Msechu palikuwa hapatoshi...

 Msanii wa Hip Hop toka Uganda... NAVIO...

 Gwiji toka Rwanda ALPHA

 Mshindi wa BSS 2010 Mariam Mohamed akitoa vitu vyake...

Kubwa lao, Joseph Payne...

 Mashabiki wakijiachia...

 Top 4 ya BSS 2011...

 Warembo jukwaani wakionyesha briefcase zenye fedha...

 Mr. Flavour in the House...

 Full gambe...

 Katika dada... Kwa raha zako...

Tunda man mjengoni....

Castal lite kwa wingi mezani....

Masister duu kwa wingi tuuu... Masharobaro pembeni...

 Mizuka inapopanda....

 Warembo katika mzuka...

 Full kujiachia na Mr. Flavour...

 Wera wera... Lulu akikata kiuno...

Sssssshhh..... Mambo bado....

 Jumanne Iddi Kazini....

 MC Godwin Gondwe akiwajibika...

 Mshiriki Waziri Salumu akitoa burudani...

 Mshiriki Rodjer Lucas akitoa cheche zake....

 Bella akiimba kwa hisia...

 Mshiriki Haji Ramadhani akikata mauno...

Sharobaro in da house....

"Hapa hakiachwi kitu hapa...." 

 Mr. Flavour all da way from Nigeria....

 Mshindi wa tatu Waziri Salum akipokea million 5 zake...

 Mshindi wa pili  Rodger Lucas akipokea million 10 zake...

 "Huuuuuuuuuureeeeeeeh..."

Mshindi akikumbatiwa na mnenguaji wa TWANGA PEPETA...

Chukua hiyoo.......

 Na mshindi wa kwanza wa BSS 2nd chance ni....
Haji Ramadhani akijinyakulia million 40....

Kwenye one n two si mwingine bali ni mtu mzima Dj. Choka......
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...