Tuesday, July 31, 2012

DIAMOND KUJITOSA KWENYE TAARAB...???


BAADA ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, msanii nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema anafikiria kujitosa katika muziki wa taarab. Diamond alisema Jijini Dar es Salaam wiki hii kuwa,amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab.

 Mshindi huyo wa tuzo mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema, anajua uamuzi wake huo utawashangaza mashabiki wengi, lakini ni jambo la kawaida kwa msanii. 
 Diamond alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa nchini.
 
Diamond alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki kutokana na kipaji alichonacho katika fani hiyo, ambayo imempatia umaarufu mkubwa, Kutokana na kipaji chake hicho,Diamond alisema hakuna kitu anachoshindwa kukifanya katika fani ya muziki.
 
Alisema bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa anafanya tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea mafanikio kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva. 
 
Alisema anaweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha kuimba nyimbo aina zote, hivyo endapo atafikia muafaka anaweza kufanya muziki wa taarabu. 
 Diamond alikiri kuwa, muziki wa kizazi kipya umemfanya ajulikane sehemu nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na kupata manufaa mbalimbali kimaisha kwa kuishi kwenye nyumba nzuri na kumiliki magari ya kifahari.

DAWA MPYA YA UKIMWI YAANZA KAZI



DAWA mpya inayokinga na kuua kwa kasi virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, tayari imeshaanza kutumika, hii ni kwa mujibu wa ripoti za mitandaoni.
Dawa hiyo ambayo toleo lake la kwanza ipo kwenye muundo wa vidonge, inaitwa Truvada na tayari imekwishaanza kufanya kazi nchini Marekani.
Kitendo cha Truvada kukubalika na Mamlaka ya Usimamizi wa Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA), kinatoa picha kuwa sasa vidonge hivyo vinaweza kuuzwa sehemu yoyote duniani.
Kamishna wa FDA, Margaret Hamburg, amesifu Truvada na kueleza kwamba itapunguza wastani wa maambukizi mapya pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Hamburg alisema kuwa hivi sasa nchini Marekani kumekuwa na kasi ya maambukizi mapya, kwani kila mwaka kumekuwa na wastani wa watu 50,000 wanaobainika kupata Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Watafiti waliogundua Truvada wanaeleza kuwa dawa hiyo kwa sehemu kubwa inakinga VVU na upande mwingine inasaidia kuua virusi vya Ukimwi kwa mtu ambaye tayari amekwishaathirika.
Hata hivyo, FDA na watafiti hao, hawajaeleza kama Truvada inatibu moja kwa moja, isipokuwa wanasisitiza: “Inamkinga mtu kupata maambukizi mapya, inamsaidia mwathirika kwa kuua VVU pamoja na kumkinga dhidi ya magonjwa nyemelezi.”

INAFIKAJE TANZANIA
Nchini Marekani, imeelezwa kuwa inabidi serikali ya nchi hiyo ifanye juu chini kugharamia usambazaji wa dawa hiyo ili iwafikie wananchi wa kawaida kwa urahisi.
Imebainishwa kuwa usambazaji wa Truvada kwa mwaka unaweza kugharimu Dola za Marekani 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 15 za Kitanzania.
Umetolewa wito kuwa serikali zinatakiwa zishughulikie upatikanaji wa dawa hizo na kuzisambaza ili wananchi wake wazipate madukani au kwenye vituo vya afya kwa urahisi.
Limetolewa angalizo kwamba endapo wafanyabiashara wataingilia kati na kununua haki za kusambaza dawa hizo, itasababisha wananchi wa kawaida wanunue Truvada kwa bei kubwa mno ambayo pengine wasio na uwezo wanaweza kushindwa kumudu.

SERIKALI YA TANZANIA INASEMAJE
Mwandishi wetu alijitahidi kwa njia mbalimbali kumpata Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi ili aweze kuzungumzia jinsi Serikali ya Tanzania ilivyojipanga kuhakikisha dawa hiyo inafika nchini lakini hakupatikana.
Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema wikiendi iliyopita kwamba hawezi kuzungumza chochote kwa sababu alikuwa ‘bize’ na watendaji wengine kuandaa kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni.
Kwa mujibu wa Mwamwaja, Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ilitarajiwa kusomwa jana, hivyo akabainisha kwamba si yeye tu, bali watendaji wakuu wote wa wizara hiyo walikuwa bize.

TRUVADA ILIFANYIWA UTAFITI TANZANIA
Mtafiti wa VVU, Connie Celum wa Chuo Kikuu cha Washington, mjini Seattle, Marekani, kwanza alieleza ugumu wa usambazaji wa dawa hiyo endapo serikali hazitaamua kusimamia kisha akaeleza kwamba Truvada imefanyiwa utafiti karibu mabara yote.
Celum alisema kuwa baada ya Truvada kuendelezwa na Taasisi ya Gilead Sciences kwenye Jiji la Foster, California, ilifanyiwa utafiti Afrika Mashariki (Tanzania ikiwemo) na kusaidia kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 75.

ONYO LATOLEWA
Hata hivyo, baadhi ya watafiti wamesema kuwa pamoja na Truvada kuonekana ni mkombozi dhidi ya Ukimwi kwa sasa lakini haitakiwi kutumika kiholela.
Wamesema kuwa dawa hiyo imeunganishwa kutoka kwenye mkusanyiko wa dozi za kupunguza makali ya virusi, hivyo inaweza kumuathiri mtumiaji.
Imeshauriwa kwamba kabla ya kutumia Truvada ni vizuri kupimwa na kuthibitishwa na daktari kwamba mwili wako una sifa za kutumia dawa hiyo.

Thursday, July 19, 2012

Ripoti ya kuzama kwa meli Zanzibar

Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina Star Gate ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar. Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali. Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar. Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar. Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800. Mwandishi wa BBC mjini Dar Es Salam, Aboubakar Famau anasema kuwa meli hiyo MV Skagit ilianza kuzama saa sita saa za afrika mashariki ikiwa inaelekea bara. Safari kati ya bara na pwani huchukua saa mbili. Inaarifiwa huenda watoto thelathini na moja walikuwa kwenye meli hiyo. Afisaa wa usalama katika bandari ya Zanzibar alifahamisha shirika la habari la Reuters kuwa meli hiyo sasa imebiruka. "maiti kumi na wawili pamoja na manusura kumi tayari wameodolewa baharini kufikia sasa. Shughuli za uokozi zinaendelea ingawa kuna changamoto ya hali mbaya ya hewa." hii ni kwa mujibu wa waziri katika ofisi ya rais Mwinyihaji Makame, Kivukio kilichoko kati ya Dar es Salaam na Zanzibar huwa na shughuli nyingi sana na huvutiwa sana na watalii pamoja na wenyeji wa Tanzania.

Fumanizi la mwaka!!!!

USIOMBE yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’, Lulu John (mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe (siyo Mr. Nice), Risasi Mchanganyiko linafunguka. Lulu alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita. SINEMA ILIKUWA HIVI Kwa mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko ya kusaka bingo, alitonywa na mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif yupo kwenye nyumba hiyo ya wageni akiigagadua amri ya sita nje ya mkataba. Lulu, baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje kapu’ ndipo akakodi bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye siyo mgeni wa uwanja huo wa mechi za kitandani. Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio. MPAKA CHUMBANI Aliendelea kusema kuwa baada ya kutimba mahali hapo alikwenda moja kwa zote hadi kwenye chumba walichojichimbia wawili hao na kuanza kubamiza mlango huku akipiga mayowe ya kuomba msaada. WENGINE WADHANI WAMEFUMANIWA Huku akizidisha kupiga kelele akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu za watu wengine waliokuwa wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine ambao walitoka kwa kihoro wakidhani wamefumaniwa wao. MUME ATIMKA NA NGUO YA NDANI Aliendelea kusimulia mkasa kuwa watu walianza kujaa nje ya chumba hicho ndipo Abdulatif akafungua mlango kwa kasi na kutimka kama mkizi akiwa na nguo ya ndani pekee kisha akaruka fensi. WATU WEWEEE! Alisema kuwa wakati anachomoka nduki alimgonga kikumbo Lulu na kumwangusha chini huku akimwacha akigaragara ambapo watu walikuwa wakimkimbiza wakisema: “Weweee.” VITA Baada ya kunyanyuka na Abdulatif kumchomoka hivihivi ndipo vita kuu ikaanza dhidi ya mgoni wake. ANG’ATWA PUA Alisema kuwa ngumi za uhakika zilipigwa hadi yeye (Lulu) akang’atwa pua ambapo alitokwa na damu chapachapa usoni huku aliyefumaniwa akitafuta njia ya kujisitiri baada ya kuchaniwa nguo na kubaki mtupu. Baada ya hali kuwa mbaya, Lulu alisema walitokea wasamaria wema na kuwatuliza ambapo yeye alikimbilia Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kumfungulia mgoni wake shitaka la shambulio la kudhuru mwili lenye jalada la kesi namba OB/RB/12675/2012. Kwa mujibu wa Lulu, kitendo cha kumfumania mwanaume huyo kimemuumiza kwani amekuwa akimtunza kwa hali na mali na hakuweza kuamini kama angeweza kumsaliti. Juhudi za kumpata Abdulatif hazikuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mitamboni hata hivyo zinaendelea. KWA NINI USIOMBE YAKUKUTE? Lilikuwa ni tukio la aina yake ambalo halikuishia pale gesti tu bali liliingia mtaani ambapo vitendo vya Abdulatif kukimbia akiwa mtupu na Lulu kung’atwa pua viligeuka gumzo na kila mtu akimuomba Mungu asikutwe na kasheshe kama hilo.

Saturday, July 14, 2012

Anti Ezekiel aolewa Dubai na Mimba ya mbongo

SIKU chache baada ya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kuripotiwa kufunga ndoa mjini Dubai, mchumba wa staa huyo aliyetambulika kwa jina moja tu la Jeff amesema kuwa, anashangazwa na Aunt kuolewa huku akiwa na ujauzito wake, Amani linashuka na mistari ya habari hii. Akizungumza na Amani jijini Dar hivi karibuni, Jeff amesema kuwa taarifa za kuolewa kwa Aunt alizipata akiwa nchini China na kushtuka sana. “Kinachonishangza ni huyo jamaa anafungaje ndoa na mwanamke ambaye ana ujauzito wangu wa miezi sita ambao aliondoka nao kwenda Dubai?” alihoji Jeff. Jeff aliendelea kutiririka kama mtu alikuwa akiimba mashairi ya Muziki wa Injili kuwa, kingine kinachomuumiza ni tabia ya Aunt kumuomba fedha za matumizi akiwa Dubai huku akijua kwamba amefunga ndoa na mtu mwingine. “Wanawake ni mama zetu lakini ni wauaji wakubwa, inakuwaje anagawa mimba ya mtu kwa mwanaume mwingine halafu mbaya zaidi nilipokuwa China kila wiki alikuwa akiniomba fedha za matumizi nami nikawa namuagiza aende sehemu kuchukua kumbe ni mke wa mtu!” alishangaa Jeff. Juhudi za kumpata Aunt ili kuthibitisha madai hayo ya ujauzito hazikuweza kufua dafu baada ya simu yake anayoitumia huko Umangani kutokuwa hewani. Jambo lingine lililomshtua Jeff ni kusikia kuwa aliyemuoa Aunt huko Dubai anaitwa Sunday Dimonte kwani msanii huyo ‘alisevu’ namba yake kwa kutumia jina hilo. “Nilipomuuliza kwa nini ananisevu kwa jina la Dimonte, Aunt aliniambia kuwa jina hilo lilimaanisha mpenzi kwa Lugha ya Kifaransa,” alisema kwa masikitiko Jeff.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...