Friday, September 30, 2011

Kwa amani ya penzi 100%, uaminifu uanzie kwako...





Katika hili niseme tu kwamba, huu ni ulimbukeni uliopitiliza, kuridhishana huko kimapenzi kuna madhara makubwa na wale wanaoendekeza mchezo huo, ipo siku watajuta na kutoa machozi huku wakikosa watu wa kuwabembeleza.

Tubadilike jamani, tuache kufuata mkumbo kwa kufanya yale ambayo yanahatarisha maisha yetu eti kwa kisingizio cha kuogopa kuachwa au kusalitiwa.

Baada ya kugusia kidogo mada hiyo ya wiki iliyopita sasa nirejee kwenye mada yangu ya wiki hii.
Nazungumzia suala la uaminifu ambalo ni nguzo muhimu katika uhusiano ulio ‘siriasi’.

Kila mmoja atafurahi kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye ni muaminifu kwa sababu hakuna anayefurahi kusalitiwa.

Kila mtu anataka kufurahia penzi lake peke yake na wengine waishie kuona tu kama siyo kula kwa macho. Lakini sasa, uaminifu siku zote ni lazima uanzie kwako. Nasema hivyo nikimaanisha kwamba, itakuwa ni vigumu kutarajia kuwa na mpenzi ambaye ni muaminifu wakati wewe siyo muaminifu.

Unataka mpenzi wako asitoke nje ya ndoa wakati wewe mwenyewe una mademu kibao huko nje, inakuja kweli? Itakuwaje jambo la kukuuma ukisikia mpenzi wako anakusaliti wakati wewe kusaliti ni sehemu ya maisha yako ya kila siku?

Tambua unavyoumia wewe ukisikia penzi lako linamegwa, ndivyo anavyoumia mpenzi wako hivyo ni bora ukajiangalia kabla ya kumgeukia mwenzako.

Kwa nini mada hii?
Yupo rafiki yangu mmoja ambaye aliwahi kunieleza jinsi anavyoumia kumuona mkewe akiwa anapiga stori na wapangaji wenzake wa kiume. Jamaa anasema anahisi mkewe anaweza kushawishika kumsaliti kutokana na ukaribu wao.

Cha ajabu sasa mwanaume huyo ni kiwembe kupita maelezo. Mara nyingi nimekuwa nikitumia muda wangu kumsihi abadili tabia, atulie na mke wake ambaye ni mzuri kuliko hata hao mademu lakini amekuwa mgumu kunielewa. Kila demu mzuri anayekatiza mbele yake anataka amuonje.

Sasa hebu jaribu kuangalia, jamaa ana wivu na mkewe kwa sababu ya ukaribu tu na wanaume lakini yeye ni mwingi wa habari na wengi wanajua.
Hivi huyu anatarajia awe na hisia kwamba mkewe hamsaliti wakati yeye ni msaliti aliyebobea?

Inawezekana kweli mama huyo wala hana mpango wa kumsaliti mumewe lakini mwanaume huyu anahisi anaweza kusalitiwa kutokana na tabia zake za kumsaliti mkewe.
Yaani anahisi anavyomfanyia ndivyo anavyoweza kufanyiwa, kitu ambacho kinaweza kuwa hakina ukweli.
Ndiyo maana nikasema, uaminifu uanzie kwako.
Jenga mazingira ya kumfanya mpenzi wako akuamini na yeye ‘automatikale’ atafanya hivyo.

Wanaosaliti ndiyo wanaosalitiwa,
uchunguzi usiyo rasmi uliofanyika unaonesha kuwa, wanandoa ambao siyo waaminifu ndiyo wanawashawishi wenzao kuangalia uwezekano wa kutoka nje ya ndoa.

Kwa mfano, mume anarudi nyumbani akitokea kwa kimada, mkewe anamhitaji faragha anaambiwa amechoka.
Baadaye mke anapata umbeya kuwa, mumewe ana ‘kitu’ kingine kinamzuzua. Katika mazingira haya ndipo unakuta baadhi ya wanawake ambao si wavumilivu huangalia namna ya kulipiza kisasi kwa kutafuta ‘vidumu’.

Hujawahi kusikia mwanaume anatoka kwenda kwa wanawake mke naye anatoka kwenda kwa mabuzi? Hujawahi kusikia au kusimuliwa mke kaenda kumsaliti mumewe gesti akakutana uso kwa uso na mwenza wake akiwa na kimada? Hiyo inaashiria kuwa, wapenzi na wanadoa wanarithishana mambo mazuri na mabaya.

Ndiyo maana wataalam wa mambo ya mapenzi wanasema, kama wewe ni bingwa wa usaliti basi tambua na wewe unasalitiwa lakini hujui tu. Lakini ukitulia, unakuwa na asilimia flani ya kumfanya mpenzi wako atulie.

Ushauri wangu
Tulia na wako ambaye moyo wako umeridhika kuwa naye. Mpende kwa maana halisi ya kumpenda, tena kwa asilimia zote.
Tamaa za kijinga ziweke pembeni.
Kuwa muaminifu kwake ili iwe chachu ya yeye kutulia lakini nikuhakikishie tu kwamba, kama wewe si muaminifu kwa mwenza wako ni vigumu kutengeneza maisha ya furaha. 

Comedy ZONE

Sharobaro kakutana na Binti wa kilokole, akamuaproach demu akakubali, sharo alimwambia demu km yy Baba yake ni mchungaji
Cku m1 demu alimualika Sharobaro kwenye maombi Sharo akakubali, Demu akaona itakuwa c vizuri kumualika mtoto wa mchungaji kwenye maombi bila ya kumpa hata nusu saa ya kuomba
Demu akamuomba Baba mchungaji kabla ya wa2 kuanza shughuli ya maombezi Boyfrnd wake awe wa kwanza kuombea wa2 kwa mungu,
Sharobaro alipewa nafac na aliombea wa2 km ifuatavyo:
Dingi ye2 uliye majuu, jina lako lipewe maflag ya kufa m2, ufalme wako utuibukie kiaina magetoni, unachotaka kifanyike geto na maskani kwako, u2shushie mabaga, mapiza, masosej, chipc na mazagazaga kibao, 2chukulie poa km 2navyowachukulia cc wanao2zingua, uc2tie ktk manamna gn vp, na u2pe fedha yako huko paradiso, amen,
2tafanikiwa men,,,,,,
Waumin=!!!!!!????????
Demu=alizimia

Isha: Akha! Sina matiti...



MWIMBAJI na mtunzi mahiri wa Kundi la Taarab la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan ‘Mashauzi’  (pichani), ameshtuka na kusema katu ukubwa wa matiti yake hautokani na madawa ya kukuza viungo yanayotoka China...

Mashauzi aliyasema hayo Alhamisi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar katika moja ya shoo zake.

Akiwa amevalia nadhifu stejini, siku hiyo, Mashauzi alionekana kukonga nyoyo za mashabiki wake hususan alipoimba kibao cha Mama Nipe Radhi.

Baada ya kumaliza wimbo huo na kushuka, ndipo paparazi wetu alimfuata na kumbana akitaka kujua siri ya ukubwa wa matiti yake kwa sababu kuna watu wanamtuhumu kutumia dawa za Kichina.

Akafunguka: “Kimsingi wengi hufikiri hivyo, lakini msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, haya ni matiti yangu ya kuzaliwa, ila kuna wanawake wanavutiwa na ukubwa wake.

“Sikatai kwamba wapo wenzangu na miye wanaotumia Mchina kukuza matiti, wengine hata makalio lengo waweze kuwa na soko hapa mjini, mimi sina muda huo na siwezi kumkosoa Mola kwa uumbaji wake,” alisema Mashauzi.

Comedy ZONE

Mmasai alienda kwa mara ya kwanza kuchoma sindano hospitalini...

Alipoanza kuchomwa ghafla akamuuliza nesi, "Uuuuuuwi, we mama yoyo, bado jaona tundu huko nyuma mpaka natoboa ingine?!"

Kanumba, Ray: Hatumtaki Aunt....


Masupastaa wawili wakubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Steven Charles Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’ wanadaiwa kuchochea kumpiga chini mcheza sinema ‘seksi’, Aunt Ezekiel Grayson kutumika katika muvi zao kwa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha ZE UTAMU ndani ya sanaa hiyo, kuna kikao kilichokaa katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar kikiwahusisha waigizaji hao kilichofikia uamuzi huo huku sababu ikimumung’uywa.

ZE UTAMU lilipododosa ‘sosi’ ya ishu hiyo ya kufungiwa kwa staa huyo namba moja kwa mauzo ya filamu, chanzo hakikuwa tayari kuweka bayana mkanda kamili.

“Uamuzi uliofikiwa kwa mara ya kwanza ulikuwa ni kumfungia kwa mwaka mmoja, lakini ghafla waliibuka baadhi ya wasanii wakasema kama ana kosa asamehewe au afungiwe japo miezi mitatu.

“Wadau walipoanza kugawanyika, muafaka haukufikiwa lakini suala la kufungiwa likabaki palepale na wasamabazaji wa filamu wa Steps Entertainment wakapelekewa taarifa,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Baada ya kuzitia kibindoni habari hizo, ‘vuvuzela’ wa UTAMU alimvutia waya Afisa Uhusiano wa Steps Entertainment, Seles Mapunda ambapo alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini akabainisha kuwa anachojua yeye siyo kwa mwaka mmoja bali ni miezi mitatu.

Walipotafutwa Kanumba na Ray kwa nyakati tofauti hawakuwa tayari kutoa ushirikiano.

Kwa upande wake Aunt alisema hajui chochote juu ya yeye kufungiwa. Kwa mujibu wa mashabiki wa filamu za Kibongo waliozungumza na gazeti hili walikuwa na haya ya kusema:

“Duh makubwa! Yaani ina maana Aunt hatutamuona tena kideoni? Inabidi Kanumba Ray wafikirie upya uamuzi wao kwani Aunt ni jembe kwenye filamu.”

Comedy ZONE

MIELEKA NOMA.....! Mtoto aliamka usiku baada ya kuckia mechi kati ya baba na mama kupamba moto-Mtoto akamkuta baba yupo juu, miguu ya mama ameipeleka mbele usawa wa kichwa, yeye akajua ile ni mieleka Live bila refa akaamka.....kuchungulia mabega ya mama yote yamegusa godoro akaanza kupiga godoro huku akihesabu.....PA! Moja,PA! Mbili. PA! Tatu! Akamshika mkono baba na kumwambia umeshinda....!!!

Mcharuko...



Na Richard Bukos

Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Rose, hivi karibuni alinaswa akicheza muziki kihasarahasara kiasi cha kuwafanya baadhi ya wadau kumpachika jina la Jimama Mcharuko.

Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilijiri ndani ya Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa inaporomosha burudani pande hizo.
Awali, mama huyo alitinga maeneo hayo akiwa ndani ya gari lake aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T 108 AWP na moja kwa moja alikwenda kwenye meza kuu ya kuuzia vinywaji ‘kaunta’.

KINYWAJI KINAKOLEA
Baada ya mwanamke huyo kuketi, aliagiza kinywaji na kuanza kukigida kwa staili ya aina yake hadi akawa tilalila ambapo baadaye alijitupa kwenye ‘dancing floor’ na kulirudi sebene huku akianika baadhi ya sehemu zake nyeti.
Stali yake hiyo ya uchezaji iliwafanya baadhi ya wanaume waliokuwa ukumbini hapo kumkodolea macho huku wengine wakitokwa na udenda kutokana na jinsi alivyokuwa akijianika.

AWATUZA WASANII KWA FUJO
Kama hiyo haitoshi, Rose alipanda jukwaani kwa mbwembwe na kuwatuza wanamuziki huku akijigamba kuwa yeye ni pedeshee wa kike na kuhusu kucheza sebene hakuna anayeweza kumshinda.

Aidha, kila aliyekuwa akimtuza alimkatia mauno na wakati mwingine kujiangusha chini kisha kujigalagaza kama aliyepandwa na mzuka kupita maelezo.

Kufuatia mambo aliyokuwa akifanya mama huyo ukumbini hapo, paparazi wetu alimfuata kwa lengo la kumhoji sababu ya yeye kucheza kihasara kiasi kile ambapo kutokana na jinsi alivyokuwa ‘bwii’, zoezi hilo lilishindikana.

ANASWA AKIWA FRESH
Kama Waswahili wasemavyo, milima haikutani ila binadamu hukutana, juzikati paparazi wetu alikutana na Rose ndani ya Ukumbi wa Meeda ulipo Sinza Mori, Dar es Salaam akiwa kwenye mishemishe zake.

Alipobanwa sababu ya siku ile kucheza kihasara kiasi cha kuanika nyeti zake wakati anaonekana ni mke wa mtu alisema:
“Nilikuwa na furaha sana, yaani we acha tu, kwa sasa sina kizuizi cha kujirusha kwani mchumba wangu ameshanivisha pete na yuko nje ya nchi, hana mpango wa kurudi leo wala kesho.” 

Thursday, September 29, 2011

Kanumba, Internet, Sharapova waumbuka...



ILIKUWA ni bonge la ‘pati’, sherehe au tafrija kama siyo burudani ndani ya Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam wakati Bendi ya African Stars ‘International Twanga Pepeta’ ilipokuwa ikiburudisha katika Usiku wa Mastaa.

Katika burudani hiyo, iliyofanyika Jumamosi iliyopita wasanii Steven Kanumba (pichani) na wakatanyonga wa bendi hiyo, Lilian Tungaraza ‘Internet’ na Asha Said ‘Sharapova’ waliumbuka baada ya shampeni kuwagomea kufunguka.

Ilichukua muda mrefu shampeni za mastaa hao kuweza kufunguka huku umati wa watu waliohudhuria usiku huo ukiwa umeshakata tamaa.

“Hivi vitu vinataka mazoea, inaonekana Kanumba, Internet na Sharapova hawana uzoefu wa kufungua shampeni,” alisema staa mmoja usiku huo.






Naye mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Redio ya Times ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida wa G’ aliweza ‘kuharibu vibaya vibaya’ baada ya kufungua shampeni yake kwa mbwembwe na kuufanya umati umshangilie.

Mkurugenzi wa Twanga, Asha Baraka aliwashukuru mastaa wote waliohudhuria na kuwataka kuwepo kwa wingi siku ya uzinduzi wa albamu ya 11 ya bendi yake katika Viwanja vya Leaders usiku wa Septemba 6 mwaka huu.

Comedy ZONE

Dogo wa miaka mi5 aliambiwa aanzishe sala baada ya kula mbele za wageni na familia nzima... Sala ilikuwa hivi.... "Nakushuru kwa hawa wageni waliokuja na kumaliza chakula changu, naomba Mungu ucwalete tena, naomba umbariki yule kijana anayecheza mieleka kitandan na dada kila cku mchana kukiwa hamna watu na kumlisha sausage iliyoko ndani ya suruali yake ili cku dada ashibe... Pia naomba uwasaidie wadada walio uchi ndan ya cmu ya baba wapate nguo, mwisho wabariki wale wanaume wanaokuja kulala na mama wakati baba amesafiri nao wapate nyumba zao na vitanda... Ameeen!!!"

CABO SNOOP JUKWAA MOJA NA KINA SHAGY



Mwanamuziki anayetamba na wimbo wake wa Prakatumba, Cabo Snoop kutoka Angola, yuko nchini Nairobi kwa shoo maalum ya Tusker itakayowakutanisha na kina Shaggy na Eve. Pichani juu na chini Cabo akiwasili na kuongea na wanahabari Uwanja wa Kimataifa wa Jomo kenyata Kenya jana. Shoo inafanyika Jumamosi hii.


Warembo wa Tusker wakiwa tayari kuwapokea wageni wao Uwanja wa Ndege jana Nairobi. 

Comedy ZONE


Mrs alikua jikoni buzy mume akataka kumsuprise mkewe,
akaingia chumani akabadilisha sim card,akampigia mkewe.
Mr>hallow darling!
Mrs bila kujua nani.
Mrs>kata piga baadae hili guruwe lipo ndani...

Sintah na Nature tena........


Kweli adui mpenzi ni laini kwa nyama ya ulimi, wawili wanaopendana kwa dhati hawaachani ila hupumzishana kupisha hasira ziishe, kuhusu mastaa Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na Christine John Manongi ‘Sintah’ ni stori ya MV Mapenzi.

Habari zinasema kuwa Nature na Sintah hivi sasa hawana bifu, wamesahau tofauti zao, wapo pamoja hivyo kuibua ‘ndogo ndogo’ kwamba wamerudiana tena baada ya bifu la miaka tisa.

The 5star BLOG inajua kuwa Nature ni mume wa mtu lakini limenasa mazungumzo yake na Sintah ambayo yanatengeneza picha kuwa ama wamerudiana kweli au kuna kitu kinaendelea kati yao.
Chanzo chetu cha kwanza kabisa kiliandika SMS: “Wanaogombana ndiyo wanaopatana, Sintah na Nature sasa mambo yao ni bambamu.”

Katika kuifanyia kazi SMS hiyo, UTAMU ilimpigia simu ‘sosi’ huyo na neno lake likawa: “Nyie fuatilieni mtajua. Nature si aliwahi kuimba kwamba inamuuma sana? (Inaniuma Sana), basi kwa taarifa yenu, hivi sasa haimuumi chochote.”

BLOG hii iliendelea kufanya kazi kwa kuwasiliana na mtu wa karibu na Sintah ambaye baada ya kuombwa aseme anachokijua, kwanza alicheka kisha alijibu: “Mnachelewa sana kujua, Sintah na Nature kwa sasa siyo maadui.”




Hata hivyo, ilipombana ‘sosi’ huyo aeleze uadui wao umeishaje, alisema: “Hayo mambo nadhani Sintah au Nature ndiyo wanapaswa kueleza. Ila najua hivi sasa wanawasiliana vizuri, hawana uadui tena. Kuhusu kwamba ni wapenzi, hilo nakataa.

“Nature ana maisha yake na mke wake. Hana uhusiano wa kimapenzi na Sintah hivi sasa, ila wanawasiliana kama marafiki, zaidi kama wasanii.”

Wakati gazeti hili likiendelea kusaka kiini cha ukweli, ‘sosi’ mmoja alimueleza mwandishi wetu: “Sikuamini kama Nature anaweza kurudiana na Sintah, nimepewa taarifa za uhakika kabisa kuwa wale ni wapenzi, nashangaa kwa sababu najua Nature ni mume wa mtu, Sintah pia alikuwa na wake, jamani hawa mastaa!”

MAZUNGUMZO YANOGA
Uchunguzi wa umebaini kuwa Nature na Sintah hivi sasa wanawasiliana kwa kiwango ambacho kinadhihirisha jinsi wanavyoelewana.

Makachero, walifanya kazi yao kikamilifu na kunasa mazungumzo ya hapa na pale kati ya mastaa hao lakini kile hasa walichokuwa wanaongea kinabaki sirini. 


KIPI KIPO KATIKATI?
Sintah alipozungumza na BLOG hii alisema: “Sijawahi kuwa na uadui na Nature, sihitaji kuzungumza yaliyopita lakini kwa sasa ni kweli tunawasiliana vizuri kwa sababu tunataka kufanya kazi pamoja.

“Kuna filamu tunacheza pamoja, inaitwa Sitaki Demu. Kwa hiyo mimi na Nature ni marafiki kikazi. Kuhusu mapenzi hapana, namheshimu sana Nature, yule ni mume wa mtu, namheshimu sana mke wake. Nami nina mtu wangu, nampenda na kumheshimu sana.”

Nature alisema: “Tunatengeneza filamu, kwa sasa tumesimama, Sintah yupo busy na kazi zake, akishakaa sawa tutakamilisha filamu. Ni kazi tu, hakuna kingine.”



UNAKUMBUKA SITAKI DEMU?
Nature na Sintah walizama kwenye penzi zito mpaka kutangaza kufunga ndoa lakini mwaka 2002 waliachana, huku mwanamuziki huyo akimtuhumu mwenzake kwa kutokuwa mwaminifu.

Baada ya kuachana, kikapita kipindi cha bifu ambapo Nature alidaiwa kurekodi nyimbo mfululizo akieleza madudu ya Sintah. Ngoma hizo ni Sitaki Demu (Original na Remix) pamoja na Inaniuma Sana.

Mwaka 2003, wakati Nature akiwa kwenye ziara ya muziki Mwanza, Sintah alipanda jukwaani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kucheza wimbo Sitaki Demu.

Nature ambaye alikuwa anaimba, baada ya kumuona Sintah akicheza jukwaani alisusa kuimba, hivyo kutibua shoo hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na Prime Time Promotion ambayo ni kampuni tanzu ya Clouds Media Group.


Wakati huo, Sintah alikuwa mtangazaji wa Redio ya Watu, Clouds FM, Mwanza na kutokana na tukio hilo la kuhusika kuharibu shoo ya Nature, menejimenti ya redio hiyo, chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Joseph Kusaga, iliamua kumfukuza kazi.

Comedy ZONE


Muislamu na baniyani (muhindu) walikamatwa na kufungwa jela miaka kibao. Walijibidiisha kusali na kuomba kila leo angalau siku moja wawe huru. Muislamu alimuomba ALLAH, ilhali muhindi SANAMU wake aliyekuwa naye pale jela. Dua ya muislamu ikatakabaliwa akaachiliwa. Muislamu alipokuwa anatoka jela, muhindi akamfuata na ikawa hivi:
Muhindi: Bana hii mambo namna gani, kila siku sisi omba pamoja, wewe toka mimi bado toka...............Mimi hapana elewa
Muislamu: Bhai wewe na Mungu wako nyote mpo jela nani atamtoa mwenziwe?

WOLPER: maisha yangu fedha mbele




MSANII wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe amekiri kuweka fedha mbele katika maisha yake huku akidai kuwa, hicho ndicho kilichomtoa Moshi kuja jijini Dar es Salaam.
Akizungumza juzikati jijini Dar,  Wolper alisema, linapokuja suala la fedha huwa hataki utani kwani lengo lake ni kutimiza ndoto zake na si vinginevyo.
Mimi ni Mchaga bwana, nimekuja Dar es Salaam  kutafuta fedha na siyo kutafuta mambo mengine,  hivyo niachwe nizisake kwa njia nizijuazo.
Ndiyo maana niko tayari kumpeleka polisi yeyote atakayenizingua katika suala la ‘mshiko’,” alisema Wolper.

Comedy ZONE

Mmasai alienda kwa mara ya kwanza kuchoma sindano hospitalini...

Alipoanza kuchomwa ghafla akamuuliza nesi, "Uuuuuuwi, we mama yoyo, bado jaona tundu huko nyuma mpaka natoboa ingine?!"

AGNESS WA MASOGANGE ANUSA KABURI


MREMBO anayedatisha katika video za nyimbo mbalimbali za Kibongo na mcheza filamu anayekuja kwa kasi, Agnes Gerald ‘Masogange’ ameponea chupuchupu kufa kwenye ajali mbaya ya gari na sasa hatamaniki midomo.

Tukio hilo la kumpa pole, lilitokea wiki iliyopita, maeneo ya Sinza Kwaremmy jijini Dar es Salaam.

Masogange ambaye hivi karibuni ameanza kujipenyeza kwenye  filamu, alikutwa na ajali hiyo  akiwa ndani ya taksi akitokea nyumbani kwake Sinza Makaburini kwenda Kwaremmy kwenye mgahawa wa chakula wa Fast Food kutafuta mlo wa jioni.


Msanii huyo alisema kuwa ni wakati gari hilo likiwa linatafuta maegesho nje ya mgahawa huo ghafla  lilitokea gari lingine lililokuwa katika mwendo wa kasi na kuligonga gari alilokuwemo.

Alisema alipata mshtuko na msukumo mkubwa  uliomfanya ajigonge midomo kwenye kioo na kupasuka.

Aliongeza kwamba, mbaya zaidi baada ya ajali hiyo watu walilizunguka taksi wakiwemo vibaka ambao walitumia mwanya wa ajali  kumkwapulia  simu yake ya mkononi na fedha alizokuwa nazo (hakutaja kiasi).


“Baada ya  kupata mzinga mimi nilijigonga kwenye kioo cha mbele cha gari  na kupasuka midomo. Baada ya hapo vibaka waliniibia simu na fedha, wakatimka,” alisema Masogange.
Hata hivyo,  Masogange alisema wasamaria wema walimchukua na kumpeleka  Kituo cha Afya cha Serikali Palestina, Sinza ambako alishonwa nyuzi tano.

 Akasema kwa taabu: “kikubwa kwa sasa namshukuru  Mungu kwa kuwa ilikuwa ajali mbaya ambayo ingeweza kukatisha maisha yangu.”

Comedy ZONE

Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.
"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"
"endelea"
"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kuitisha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"
"utasamehewa"
"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo?"
- kimya........
"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"
- kimya.........
Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.
"sasa baba mbona umenikimbia?"
padri kwa taabu akajibu
"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"

MLELA NA AUNTY...



MUIGIZAJI mwenye sauti ya kiume katika filamu za Kibongo, Yusuf Mlela ameiminyia mavumbini skendo inayomtafuna kwamba anatoka kimapenzi na msanii mwenzake, Aunt Ezekiel Grayson (pichani).
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Mlela alisema kuwa, anawashangaa wazushi wanaoneza madai hayo lakini akasema anajua ni kutokana na jinsi wanavyogandana na msanii huyo kama kumbikumbi maeneo mbalimbali.
Aliongeza kuwa, licha ya kwamba Aunt ni msanii mwenzake lakini pia wameshibana ile mbaya, akaomba watu wasiwatafsiri vinginevyo.
“Unajua mimi na Aunt wote tunaishi kwa kutegemea sanaa, hicho ndiyo kitu kinachotufanya tuwe karibu, zaidi ya yote huwa tunakuwa kampani moja tunapokwenda disko au kwenye sherehe mbalimbali, ila kila mmoja ana mtu wake,” alisema Mlela.






Alipobanwa kuhusu kualikwa kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2011 na kadi yao kuonekana kama ya Mr & Mrs huku wakiingia ukumbini hapo kama wanandoa, Mlela alijitetea:
“Watu wanaotualika kwenye sherehe zao ndiyo walitupa kadi moja. Hata siku ile ya Miss Tanzania tulipewa kadi ya mwaliko moja tu ikiwa na majina yetu, ndiyo maana ulituona vile.”
Mbali na Miss Tanzania 2011, katika harusi ya msanii mwenzao, Irene Uwoya iliyofungwa jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wawili hao pia walikuwa beneti hali iliyoibua maswali kibao kwamba huwenda wawili hao ‘wanaduu’.

Comedy ZONE

Kuna jamaa mmoja alikuwa anajisaidia haja ndogo sehemu ambayo hairuhusiwi, wakati akikamilisha zoezi lake hilo, mgambo wa jiji alitokea na kutaka kumkamata.
“Samahani ndugu unajisaidia sehemu isiyoruhusiwa, kwa nini?”
“Nioneshe choo.”
“Unajitia jeuri siyo, maliza kujisaidia uzungumze na jamhuri.”
“Poa.”
Jamaa baada ya kuelezwa vile aliacha alipokuwa akikojoa mwanzo na kusogea mbele kukojoa sehemu nyingine, jambo lililowafanya mgambo wa jiji kuhoji:
“Wewe vipi mbona unazidi kuchafua mazingira, huoni kama unaongeza kosa?”
“Si ndiyo nizungumze vizuri na jamhuri?”
Mgambo wa jiji alizidi kukasirika na kumsubiri jamaa kwa hamu, jamaa alipomaliza kujisaidia alimgeukia mgambo aliyekuwa na rungu mkononi.
“Haya, mlete jamhuri nizungumze naye nimuulize vyoo vipo wapi?”
Jamaa alipotaka kumkamata, aligoma, ilibidi kiongozi wao asogee na kutaka kujua kulikoni. Mgambo alimwambia kiongozi wake kamkuta jamaa anachafua mazingira. Jamaa alijitetea:
“Mkuu nimemkuta kijana wako akijisaidia hapa na mimi nikajisaidia pembeni yake, sasa nashangaa ananikamata.”
“Muongo?” Mgambo alijitetea.
“Kama nadanganya huo mkojo mwingine wa nani?”
Mkuu wa mgambo alipoangalia kweli aliona kuna sehemu mbili ambazo zote zilikuwa bado mkojo mbichi.
Aliamini kabisa yule jamaa anasema kweli na kuamua kumuachia. Jamaa aliondoka huku akichelekea moyoni kwa kumzidi akili mgambo wa jiji. Kweli akili ni nywele.

Sunday, September 25, 2011

Ukahaba Dar...




Biashara haramu ya ngono ikihusisha watoto wadogo na wanafunzi imeshamiri nchini na inalijengea taifa picha ya aibu mbele ya jamii pana ya kimataifa, ze UTAMU Jumamosi lina ripoti kamili ya madanguro, gesti na hoteli maarufu zinazoendesha ‘unyambilisi’ huo jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi wa blog hii umebaini kuwa, nyuma ya biashara hiyo kuna vigogo ambao wanajitajirisha kwa kuwauza watoto wa kike wa kati ya miaka 11 hadi 14 ambao wanaelezwa kuwa na soko zaidi ukilinganisha na wale wenye umri ulioyoyoma.
Kwa wiki kadhaa chumba chetu cha habari kimekuwa kikipokea ujumbe mfupi kutoka kwa watu walioomba hifadhi ya namba zao kuwa kuna wafadhili wa biashara hiyo ambao huwachukua wasichana wadogo vijijini kisha kuwamwaga jijini Dar kwa ahadi ya kuwatoa kimaisha, lakini huishia kuwafanyisha biashara hiyo haramu inayostahili kupingwa kwa nguvu zote.
Ilifahamika pia kuwa, kuna baadhi ya watu huwashawishi wanafunzi wa kike jijini Dar ambao huaga kwao kuwa wanakwenda shuleni, lakini huishia kwenye madanguro, gesti na hoteli maarufu kwa ajili ya kuuza miili, hivyo kuwafanya wazazi kuwa na matumbo joto wanapowabaini.
Ze utamu Jumamosi lilifanya mahojiano na wasichana hao wadogo wanaojiuza sehemu mbalimbali jijini Dar ambapo walikuwa na haya ya kusema:
WA KWAZA (SINZA): “Huwa natoroka shule na kwenda kujiuza kwa wanaume ili kujikimu kimaisha. Fedha ninayopewa ya matumizi huwa haitoshi.”
WA PILI (BUGURUNI): “Kawaida nafanya mapenzi na wanaume 5 hadi 6 kwa usiku mmoja.
WA TATU (KINONDONI): “Malipo kwa tendo moja ni 10,000. Saba za tajiri, tatu za kwangu.
WA NNE (TEMEKE): “Kazi ni ngumu lakini kwa sababu ni shida, nafanya.”
RIPOTI YA BBC
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC iliyoibua mjadala hivi karibuni na kuwaweka watu presha juu, watoto wanaojihusisha na biashara hiyo walieleza jinsi walivyodanganywa kuzamia jijini Dar kufanya kazi nzuri za kuwapatia mkate wao wa siku, lakini wakaishia kwenye biashara ya ukahaba.
Watoto hao walieleza kuwa, kutokana na ugumu wa maisha vijijini walipata matumaini kuwa jijini kuna matunda, lakini walipofika wakawa wakifugwa kama watumwa kwa kazi moja tu, kuuzwa kwa wanaume wapenda ngono za rejareja.
Katika mjadala huo ulioendeshwa kwa siku tatu, vitoto hivyo vibichi viliweka wazi kuwa wanapochukuliwa na wanaume hulipwa Sh. 50,000 lakini huambulia Sh. 10,000 kwani fedha nyingine huchukuliwa na tajiri.
MMILIKI WA DANGURO
ALIRITHI KWA BIBI YAKE
Kwa mujibu wa mmoja wa wamiliki wa madanguro hayo machafu (jina tunalo),  biashara hiyo alirithishwa na bibi yake kwa hiyo haoni hatari kwa sababu hakusoma hivyo kazi hiyo anaiona ni halali.
Bila aibu, mwanamke huyo mchafuzi aliendelea kubwabwaja kuwa ana ‘kocha’ maalumu wa kuwafunza watoto hao namna ya kujituma wanapokuwa ‘kazini’ na wanaume.
GESTI, HOTELI NA MADANGURO
HATARI NI HAYA
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Jamii Forums ulibaini kuwepo kwa gesti, hoteli na madanguro hatari sehemu tofauti jijini Dar.
Ilibainika kuwa sehemu hizo ni pamoja na hoteli maarufu zilizopo Sinza Madukani, Sinza-Mori, Sinza Afrikasana,  Ubungo External, Makuburi, Mbezi, Majumba Sita-Ukonga, Uwanja wa Taifa, Saba Saba, Kawe, Kunduchi, Buguruni na Magomeni.
Pia, kuna hoteli maarufu za nyota tatu katikati ya jiji maeneo ya Posta na Kariakoo katika viunga vya Mnazi Mmoja zinazofanya biashara hiyo hasa kwa wanandoa wanaofanya kazi maeneo hayo ‘wanaocheza nje kapu’ kwenye ndoa zao.
WAZIRI SOFIA SIMBA ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba (pichani), mbali na kukiri kuwepo kwa hatari hiyo, alidai kuwa wizara yake inajitahidi kutekeleza na kulinda maslahi ya watoto ingawa hakueleza jinsi wanavyokabiliana nayo.
KUTOKA ZE UTAMU BLOG
Ukweli ni kwamba hali ni mbaya kupita maelezo.
Tunatoa wito kwa idara zote zinazohusika kunusuru kizazi cha kesho kwa kuwaepusha na mateso wanayoyapata huku janga la ukimwi likichukua kasi. Pia, tunaiomba jamii kupinga kwa nguvu zote kwa kuripoti kwenye vyombo husika uwepo wa biashara hiyo haramu.

Comedy ZONE

Tajiri ambaye alikuwa anajulikana sana maeneo flani, alikuwa anamuozesha bint yake,
Wa2 wengi waliikamia haruc hiyo, tajiri nae kwa kujiproud aligawa card kwa kila m2
Siku ya sherehe ilipowadia wa2 walihudhuria
Muda wa msosi ulipofika wakapitishiwa mafuta ya kula ndio maji ya kunawa,
wa2 wakaulizana, maji ya kunawa mafuta ya kula je huo msoc itakuwaj???????
Mara zikapitishwa sahani, wa2 wakaanza kuangaliana usoni?????????
Kufunua mafenec, wa2 wote hoii!!

TWANGA PEPETA, EXTRA BONGO ZARINDIMA DAR

 Sehemu ya watu waliofurika.

 Wadau waliokosa viti wakiwa wamesimama.

BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ usiku wa kuamkia leo imefanya onyesho maalum la kuwaburudisha mashabiki wake na mastaa mbalimbali katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam. Katika onyesho hilo bendi hiyo ilitangaza uzinduzi wa albam yake ya 11 utakaofanyika Novemba 6 mwaka huu. Yafuatayo ni baadhi ya baadhi ya matukio yaliyojiri kwenye onyesho hilo.

 Msanii wa filamu, Steven Kanumba ‘The Great’ akifungua shampeni kuwatakia afya njema waliohudhuria ukumbini.

 Mfanyabishara maarufu jijini Dar, Pius Ruta ‘Mzee wa Pamba’, amkimtunza mwanamuziki wa Twanga, Dogo Rama.

 Mashabiki wakisugua kisigino.    

Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ usiku wa kuamki leo imefanya makamuzi kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar es Salaam.
 Mnenguaji wa bendi hiyo, Mwantum Athuman (mwenye blauzi nyeupe) akiserebuka na mashabiki wa bendi hiyo.

Kutoka kushoto ni wanenguaji Aisha Madinda, Otilia Boniface na Mwantum Athuman wakikamua.

Jinsi ya kuishi na wafanyakazi wenzako

NAMSHUKURU Mungu kwa rehema na fadhila zake katika maisha yangu kwani amekuwa ngao na nguzo yangu kuu.

Ahsanteni sana wadau na wasomaji wa kona hii ya Jitambue kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkiuonesha kwani napokea simu nyingi za ushuhuda wa kujikomboa baada ya kusoma makala mbalimbali za kona hii.

Leo nimeona ni vyema tujikumbushe jinsi ya kuishi na wafanyakazi wenzetu katika Nyanja na ngazi tofauti. Kumekuwa na tatizo kubwa kwa baadhi ya watu namna ya kuishi na wafanyakazi wenzao hasa katika ofisi kubwa zinazojumuisha watu wengi.

Kabla ya kutoa dondoo za jinsi ya kuishi vizuri na wafanyakazi wenzako, naomba nitoe ufafanuzi mfupi ambao utakusaidia kukabiliana na vikwazo vya hapa na pale katika kuishi na watu wa rika mbalimbali katika jamii.

Kwanza ifahamike kuwa, popote palipo na mkusanyiko wa watu wengi, basi kuna mrundikano wa tabia, mila na desturi tofauti. Yaani kila mtu ametoka katika familia yenye malezi tofauti na ya kwao hivyo katika utofauti wa mambo hayo, ni lazima kutakuwepo na migongano ya hapa na pale kwani kila mmoja ana amini alichojifunza nyumabani kwao.

Hivyo basi, unapokuwa ofisini unakutana na watu wa aina hiyo. Watu ambao mnatofautina mambo mengi ikiwemo uelewa, vipaji na ustaarabu.
Hivi ndivyo unapaswa kuishi na wafanyakazi wenzako:

Soma Mazingira
Unapokuwa ofisini na wafanyakazi wenzako, jitahidi sana kusoma mazingira ili ujue ni mambo gani hayatakiwi na ni yapi yanatakiwa kufanyika na kwa wakati gani. Hii itakusaidia kuepuka baadhi ya migogoro na wafanyakazi wenzako.

Ninaposema kusoma mazingira ninamaanisha kuwa, kuna baadhi ya mazingira ndani ya ofisi ambapo watu hawapendi kuchangia vifaa kama kompyuta na vingine. Sasa unapoingia na utaratibu wako pasipo kusoma na kuyajua mazingira hayo, unajikuta moja kwa moja unavunja taratibu za kiofisi kwa sababu tu hukusoma mazingiara tangu awali.

Tambua udhaifu na uimara wa wafanyakazi wenzako:
Kila binadamu ana udhaifu na uimara wake. Katika mazingira unayofanyia kazi, jitahidi sana kumsoma kila mfanyakazi mwenzako ili ujue ni kwa namna gani utaweza kuishi naye.
Kuna baadhi ya watu hawapendi utani, wengine wanapenda sana utani na wengine huonekana wamenuna hata kama wanafuraha. Hivyo ni lazima kuwasoma mmoja mmoja.

Katika maofisi, utakutana na wafanyakazi ambao ni waongeaji, wengine wakimya, wengine wanapenda kucheka pasipo na sababu ya msingi na kila aina ya tabia ambapo ni lazima kila mtu amjue mwenzake ana kasumba na tabia zipi.

Tumia lugha na maneno ya heshima
Epuka sana tabia ya uropokaji usiozingatia lugha nzuri hasa lugha za mitaani. Vijana wengi sana wanashindwa kutofautisha mazingira ya ofisini na mitaani ambpo utakuta maneno anayoyatumia mitaani ndiyo anajaribu kuyatumia hata katika mazingira ya ofisini kwa wafanyakazi wenzake. Jambo ambalo si sahihi.

Kama unashida na mfanyakazi mwenzako, basi mfuate kwa utaratibu kisha muite kwa jina lake ndipo umueleze shida yako.

Katika hili zingatia maneno ya samahani kabla ya kumueleza shida yako.
Na inapotokea umemkosea mfanyakazi mwenzako kwa namna moja au nyingine, basi ni busara kama utamtaka radhi na kutorudia kosa lile.

Sasa utakuta mtu anashida na mfanyakazi mwenzake lakini jinsi anavyomuita na kumueleza, utadhani anamuamrisha mwanaye.

Epuka sana madeni kwa wafanyakazi wenzako na kama ikitokea umekopa fedha kwa mfanyakazi mwenzako basi jitahidi kurejesha kwa muda muafaka, na tena katika hali ya ustaarabu. Pia jitahidi kutoa misaada kwa wenzako wanapopatwa na matatizo.

Kuna wale wenzangu na mimi ambo wao hupenda kusaidiwa tu lakini siyo kusaidia wenzao! Hii ni hatari sana. Jitahidi kuwa karibu na wafanyakazi wenzako kwa kila hali. Kama ni matatizo basi shirikiana nao.

Umekata tamaa ya maisha? Tiba ni hii hapa...

KUPANDA na kushuka ni hali ya kawaida katika maisha ya mwanadamu. Siku zote dira ya kuishi inapatikana katika kanuni hii inayoacha giza la maisha ya kesho.

Pamoja na kuwepo kwa mambo hayo mawili katika maisha yetu, imebainika kuwa kukosa limekuwa ni jambo baya linalokatisha tamaa watu wengi. Ingawa kukosa ndiyo njia sahihi ya mwandamu kujifunza, lakini si wote wanaopenda kujielemisha kupitia kwayo.

Kukosa, limekuwa ni suala la aibu na lenye kukatisha tamaa ya kuendelea kuishi. Si wasomi wengi wanaofurahia kushindwa mitihani yao na wachache kati ya watafuta kazi wanaoridhika na majibu ya HAPA HAKUNA KAZI, pindi wanaposaka ajira.

Bila shaka hii ni changamoto kubwa katika maisha ya wengi, machozi ya wanadamu yanadondoka chini pale suala la kushindwa kufanikiwa katika jambo fulani linapotokea. Wasiopata usingizi na wanyonge wa kauli wanatoka katika makundi ya waliojaribu mara nyingi kupata wachumba, kutafuta kazi, kufanya biashara, kutafuta utajiri, kulima na kujikuta wakipata jibu la kukosa.

Mpaka sasa tafiti zinaonyesha kuwa, dunia imepoteza watu wengi kwa sababu ya ukataji tamaa, hii ina maana kwamba, wengi hatufahamu mantiki ya kukosa katika harakati za maisha yetu. Lakini ukweli unabaki kuwa mafanikio hayana maana kama kutofanikiwa hakutakuwepo.

Mara nyingi mafanikio makubwa ya kimaisha hutokana na kushindwa. Watoto wanapoanza kutambaa au kutembea huanguka na kuumia, lakini kwao si apizo la kutorudia tena kupiga hatua, bali ni zingatio la umakini zaidi juu ya nguvu na mbinu za kutembea bila kudondoka wakati ujao. Hivi ndivyo inavyompasa mwanadamu anayetafuta na kukosa, yaani ajaribu mara nyingi na asikate tamaa.

 Lakini kwa kuwa ukataji tamaa mara nyingine si kitu cha kupenda na hasa linapokuja suala la kuzama kwa matumaini yaliyokusudiwa na mhusika, ndiyo maana nimeona ni muhimu kuandika mbinu kadhaa za kumsaidia mtu aliyejaribu na kujikuta katika hali ya kukata tamaa.

KWANZA: Jifunze kuwa mtu mwenye kutegemea mafanikio bila kujali kama una kitu au huna. Ukilala na kuamka itazame kesho kuwa ndiyo siku ya kufanikiwa kwako. Usikubali kuwa  na mtazamo wa kutofanikiwa, kwani mawazo ya aina hiyo yatakuondolea ujasiri wa kujaribu na kujikuta unazidi kudidimia katika matatizo. Kumbuka waliofanikiwa si miungu ni watu kama wewe!

PILI: Ukikabiliwa na mawazo ya kukosa jipe muda wa kupumzika, kwa kusikiliza muziki na nyimbo uzipendazo. Fanya mazoezi ya viungo na utembelee sehemu zinazokuvutia, ukifanya hivyo utaiongezea akili yako nguvu ya kufikiri vema na kupunguza uwezekano wa mawazo ya kukata tamaa kukua na kukunyonya nguvu za kujaribu tena.

TATU: Zungumza na rafiki zako mara kwa mara juu ya yale ambayo unaona hayaendi sawa. Usiwe mtu mwenye kukaa peke yako chumbani, kwani utaipa uhuru mkubwa akiri kupembua na kuzalisha mawazo hasi mengi ambayo yatazidi kulikuza tatizo lako. Waswahili husema; akili isiyo na mawazo toka nje ni nyumba ya shetani.

NNE: Kaa chini na ufikiri zaidi kwa nini hukufanikiwa ulipojaribu.
lengo la kufanya hivyo lisiwe katika kujihukumu, bali kukusanya nguvu zaidi za kujaribu kwa mara nyingine. Ikiwa ulifeli mtihani, jiulize ni kwa kiwango gani ulisoma, ili kama kuna mahali hukujituma, wakati mwingine uongeze bidii.

TANO: Jiamini mwenyewe na usifikie hatua ya kujihukumu na kujiona hufai miongoni mwa jamii. Usijilinganishe sana na waliokuzidi kimaisha na kutamani kuwa kama wao kwa tukio la mvumo kama kulala masikini kuamka tajiri. Usipojiamini na kujipenda mwenyewe huwezi kufanikiwa kabisa. Fahamu wewe ni bora kuliko yule unayemuona mbele yako.

SITA: Kumbuka kuwa tunajifunza kutokana na makosa, kwa maana hiyo ukiona umeshindwa kufikia malengo, tambua kuwa umejifunza siyo kwamba umekwama. Katika kushindwa zidi kupata ujuzi na kujisahihisha. Ukizingatia hayo utajikuta kesho ya furaha inakuja mbele yako. 

Comedy ZONE

Kulikuwa na mzee mmoja mkali kishenzi ila alikuwa hajui kiingereza kabisaa... Mwanae anayesoma international schol alikuwa na demu wake ambaye one day demu akaenda kumcheki mshkaji kwao...

Kufika akamkuta jamaa kakaa sebuleni na mdingi wake... Yule kijana baada tu ya demu kusalimia akamwambia yule demu wake...

''Aahaaa, ndo umekuja kufata kile kitabu cha 'Speak english my father doesn't know?!''

Demu akamjibu, "Ndiyo na naomba uniazime kile kitabu cha story cha 'what about our promise?'

Kijana akajibu, "Kile cna kipo cha 'Wait for me under the coconut tree outside".

Daah, dingi kusikia hivyo akanyanyuka na kumpa dogo mwekundu na kumpongeza kwa kupenda kusoma vitabu then akaelekea zake chumbani....
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...